A message to my Ex!

A message to my Ex!

Be strong mumie,
Kuna faida ya kumuombea mema aliyekuumiza, Zidi kumuombea kila lenye kheri likawe naye, Nina ushuhuda na kumtakia mtu aliyekuumiza mema!

Pia nimejifunza ukimtakia mtu mema, Mema yanakurudia pia.!!
 
Pole sana mamy inaonekana unampenda sana ex wako pamoja na alivyokuacha bila kutegemea mimi naendelea kukupa pole tu mpenzi utampata mwanaume wa kufanana na wewe huwezi juwa nini Mungu amekuepusha nae

Sante wa kwetu, shukuru kwa kila jambo wanasema watu
 
Be strong mumie,
Kuna faida ya kumuombea mema aliyekuumiza, Zidi kumuombea kila lenye kheri likawe naye, Nina ushuhuda na kumtakia mtu aliyekuumiza mema!

Pia nimejifunza ukimtakia mtu mema, Mema yanakurudia pia.!!
Hichi ndo nachofanya nami nimejifunza sana kupitia kuombea wengine
Thanks alot
 
Habari za siku nyingi? Naimani uko salama na unaendelea na majukumu yako ya kila siku. Mimi mzima kabisa wa afya ya mwili na akili..

Its been 5mnths now since u went away, haikuwa rahisi kukubaliana na ukweli kwamba ulipita, umeenda, umeniacha! Japo mpaka leo sijaelewa sababu hasa ya kwenda bila kuaga, lkn wakati mwingine nahitimisha tu kwamba "HUKUNIPENDA"! aidha ulikuwa safarini ukahitaji kituo upumzike kidogo alafu uendelee na safari, ama ulikuwa na mategemeo fulani ukayakosa, yote heri nimeshukuru.

Muhimu tu ni kwamba nimekubali matokeo, nimesonga mbele. Nilifanikiwa kurudi mjini na kufanyia kazi moja ya maengo yetu tuliyokuwa tumepanga. Nimepata sehemu nzuri nimefungua mgahawa, nimeona nianze na hii kwanza alafu baadae niweke vinywaji. 😊😊 si mkubwa bali kwa uwezo wangu naona ni hatua aisee. Pia ule ukarabati nimefikia hatua za mwisho, Mungu akinijaalia uzima nadhani mwezi ujao itakuwa nimemaliza kabisa.

Vp wewe unaendeleaje? Umefikia wapi na mpango wako ule? Na ile mashine uliipata? Naamini Mungu wetu ni mwaminifu atakuongoza ukafanikishe kila ulilopanga, na kama tayari hongera sana sana!

Kitu nilichojifunza ni kusamehe, kukubali matokeo na kusonga mbele. Zaidi sana kuwaombea wengine. Nakushukuru kwa yote ambayo umenifunza, umenishauri na nakutakia kila lenye heri katika maisha yako na mahusiano yako mapya... uwe na usiku mwema.

Yours, zuriel!
jamaa fala kweli huyo,,,anaanzaje kwanza kukuacha?...naomba mm nije tuitanue mama ntilie yetu iwe na kiwango km cha Shishi food,,,,mm nikipika chai ww unapika vitumbua,,mm nikisonga ugali ww unakaanga dagaa km yule chawa,sema tu mm sio fundi gereji
 
ikiwa umeandika kwa roho safi, hongera sana.
bt kama nikwakutafta comment, basi umetushika mkuu.
 
Hapo ndio utajua penye miti hapana wajenzi. Binti kama huyu unamuacha kwenye mataa hivi we mwanaume umerogwa au namna gani? Samahani nimepaniki mimi wakati mwenyewe ana amani
Unamfahamu au kufungua mgahawa blah blah tayari ni binti alieshushwa kutoka peponi?!
 
Back
Top Bottom