A living reincarnation, rebirth..!

[emoji120][emoji120][emoji115][emoji115][emoji106][emoji106][emoji106][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 
Kuna ushuhuda wa dada mmoja hivi ni waajabu sana, huko youtu.

Anasema yeye alizaliwa mwaka 1991, ila hakuishi sana akafa akiwa mtoto, anasema kimwili alikufa ila kiroho alikuwa hajafa kwani alikuwa huko kuzimu. Mwaka 2001 alizaliwa tena duniani ila katika familia nyingine ambayo ndio yuko mpaka sasa.
Sijui hii imekaaje.
 
Living from future... Zipo kesi chache mno lakini zisizo na ithibati za kisayansi zaidi ya shuhuda binafsi kwakuwa ni mambo ya kiroho zaidi
 
Sasa mkuu hayo uliyo ongelea hapo kuna moja huwa linanitokea sana, la kufananishwa na watu kila nitakapokwenda nakua sielewi kama kuna kitu kimejificha ama vp.Je kutokana na kuwa katika hali hiyo vp kuna effect yoyte inaweza kutokea na kuniathiri kimwili au kiroho na katika maisha kiujumla
 
Kiroho hapana ila kimwili ni kama ikatokea hali ukafananishwa na mhalifu fulani ama mtu aliyefanya tukio mahali.... Marekani kuna kesi moja jamaa alifungwa kifungo kirefu kumbe alifananishwa na ikatokea alikuwa sehemu ya tukio
 
Tukimaliza kwenye kumbukumbu,bado tutahoji tena kuwa roho haina sehemu ya kuhifadhi kumbukumbu,iweje basi iwe na macho ya kuona inapoenda....ndipo nitafikia uamuzi wa kusema roho ni roho yenye kila kitu ndani yake[emoji41]
 
Tukimaliza kwenye kumbukumbu,bado tutahoji tena kuwa roho haina sehemu ya kuhifadhi kumbukumbu,iweje basi iwe na macho ya kuona inapoenda....ndipo nitafikia uamuzi wa kusema roho ni roho yenye kila kitu ndani yake[emoji41]
Baada ya roho kutengana na mwili huondoka na memory stick ya ubongo

Jr[emoji769]
 

Dhana ya 'Utwaaji Upya Mwili' yaani 'Reincarnation' kwa lugha ya kiingereza -- na tena kulingana na imani, maarifa ya kimapokeo na dini -- kama vile Uhindu, Ujaini, Ubuddha n.k; huenda si 'ukweli kamili' juu ya 'kuishi' na 'maisha ya mtu'.

Kwa namna yake, Utwaaji upya mwili, huenda ilikuwa ni tafsiri nyepesi juu ya ukweli wa jambo fulani lililo pana na tata kuhususiana na 'uzima' na 'miili'. Hii ilikuja na 'maona', 'manabii' na 'watu wakuu kiroho'. Kwa maana hawa wote-- iwe kutokea mashariki ama magharibu -- wametuletea nasibu ya habari na visomo kuhusiana na 'mtu','mataifa/kabila/staarabu', 'matukio', 'wakati' na 'hatma' zake.

Yesu, kutokea nchi ya zamani kule Mashariki ya Kati -- kwa mfano, amenukulishwa katika vitabu vya dini, imani na mapokeo kupata kusema "siku za mwisho, maarifa yataongezeka duniani...". Kwamba, yale anayoyafanya, watu wengi wataweza kuyafanya pia hata na zaidi... Sasa, siku za mwisho kwa mfano, ni zipi? Ikiwa mengi aliyopata kuyasema tunayakubali -- na kwa kiasi fulani kushangazwa, ni kwa namna gani aliweza kujua "Mambo ya mbele ya wakati"(?)... Maarifa kuongezeka, Vita na Mabadiliko ya Nchi...

Ni KWELI YESU ALIKUWA NI MWENYE KUWEZA KUONA MATUKIO hata nje ya mzingo wa fahamu zake za mwili wa nyama. Watu wengi tu wamepata kuwa hivyo hivyo; kuwa na 'Jicho la Tatu' -- yeye Yesu, kunukuliwa hili linawezekana pale 'mbili inapofanywa kuwa moja'... Lakini, Je, kuona nje ya mzingo wa wakati ndiyo 'kuwa na maarifa' kama yote? SI LAZIMA... Na hapa tunaweza kutumia kesi hiyo hiyo ya Yesu, kuanza kukadirisha yumkini ya ukweli wa jambo...

Japo kuna 'kanuni ya msababishano' wa vitu na matukio; ndani ya 'mapana ya yote', wakati waweza 'kuchezeshwa' na basi hata kuwa kana 'mwisho wa dunia' usiwe ni 'mwisho' wa dunia... Tunaweza kunasibu kesho iliyo ni tofauti na 'jaala' zetu. Kwenye dini, huzungumzwa 'unafsishi' wa 'Mungu Muweza yote'... Kwamba 'utu' ama 'umma' wenye 'nyoyo safi' na 'Kuishi katika Yeye' huo waweza 'kuepushwa' na lolote 'ovu'... HII NI KWELI; lakini 'Mungu' ni fumbo la Imani...

Katika siku za leo, tunayonafasi ya kujua mambo ilivyo bora kuliko siku za nyuma zilizotuletea dini na mapokeo yanayotawala wengi duniani.

Kati ya vitu ambavyo tutavijua ama kuviandea vyema ili kujua ni 'fumbo la Mungu'; lakini sasa--tunaelekea kujua ukweli kwamba hakuna 'Mungu' hasa, ila kuna 'Uungu'... Vitu vyote, ni 'sifa', 'ishara' na 'utukufu' wa 'kweli' moja iliyo ni 'Mungu'. Lakini ni pale tu tunapoimaizi ama kujinasibu na 'kweli' katika muktadha wa 'Uungu' ndipo tunaweza kujilingania uwezo wa 'kufanyika moja na mawezekano yaliyo makuu'... Ikiwemo kutawala 'Mambo ya Nyakati' na kukadirisha 'Sheria za Madhahirisho' si tu hapa duniani ila ulimwenguni pote. Labda mapokeo ya kidini yangetaja hili kana kusema: 'kuwa Warithi wa Ufalme wa Mbingu -- Mbingu na Nchi'... Ndivyo Yesu alivyoita hasa; kusema baada ya 'Mtu kuzaliwa mara pili'... Mtume Paulo kusema; kuwa 'Mtu Mpya' mwenye nasibu ya 'Nchi Mpya'...

Mshana, 'kweli' ni si hasa --- ama tuseme, haipatikani katika stori stori ama visa vya ajabu ajabu... Kweli ni 'Taji la Imani na Taa' katika ufahamu na katika mtu. Labda mtu mwenye kuiishi njia ya imani ya namna hii anaweza kuwa ni 'mtu wa maarifa'--lakini ikiwa ni hivi, mtu huyu atanasibika 'hekima' na 'busara'. Lakini pia, maarifa si lazima iwe ni maneno... Hata katika ukimya, mapenzi na utumishi, roho ya 'kweli na uzima' inatenda -- wakati wowote na popote; kupitiliza hata 'matukio katika Nyakati'... Watu wa haya ni 'Waamuzi' katika yote yatendekayo--leo, hata kesho katika leo. Katika Uungu hakuna mwanzo wala mwisho, hakuna 'mipaka' wala 'kiasi'...

Basi, humu JF sasa, kipo kizazi cha chipkizi wenye kiu na hamu ya 'kuijua kweli'... Hawa, ndiyo huanza na udadisi, wengine watahoji kuhusu dini na mapokeo, wengine watavutika na mambo yanaonekana kupitiliza kawaida, wengine watakuwa wakanushaji wa yote yaliyoletwa na dini na kuja kuonekana ni kizingiti kwa utanuzi wa fikra, maarifa na upeo. Yote haya ni kheri, Labda pamoja tutajenga 'Hema jipya la Makutanio' katika 'Hesabu' ya watu wa Leo... 'Walawi wa leo' wanamuhitaji Musa wa vilemba vingi -- mkufunzi wa fikizia za kikwantumu, mtaasisi wa maendeleo--mipango na usimamizi, mvumbuzi, mzazi, ndugu na rafiki katika 'safari ya kuhama'; toka kwenye 'utumwa wa kimafikara' kuielekea lulu ya 'uzima na habari za ulele'.

Hmmm.
 
@mose Mmh..[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545] hebu sema neno na hapa pia
Maslahi ya kiroho kwenye matokeo tasa ya kimwili yaliyoharibika

Jr[emoji769]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…