A living reincarnation, rebirth..!

Kuna hii movie ya Kihindi inaitwa KaranArjun ukiicheki somo lako la leo la reincarnation litaeleweka saaana.
 
Mku
Mkuu mshana mm nina swali dogo tu kwenye maada hii hasa kipengele cha roho kutoka na kisha kurudi na kumbukumbu kikawaida tunajua ubongo una sehemu maalum ya kuhifadhi kumbu kumbu (hypocampus) au kwa lugha rahisi ni kuwa kumbu kumbu huhifadhiwa kwenye ubongo sasa tunavyoelewa kutokana na mafunzo ya kidini ni kuwa roho huwa haina physical body yaani yenyewe ni sawa na pumzi tu bali wengine husema huwa ina taswira na umbile sawa na physical body yake sasa kama ni hivyo that means huwa haiwezi kushikika wala kuonekana na kama ni hivyo ina maaana haiwezi kuwa na sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu kwa sasa hizo memory inazorudisha kwenye mwili huwa ina bebea wapi? Mkuu?
 
Uko sahihi lakini pia naomba nikuulize hizo kumbukumbu ni physical au ni invisible?
 
Uko sahihi lakini pia naomba nikuulize hizo kumbukumbu ni physical au ni invisible?
Mkuu sipo deep sanaaa katika maswala ya neuroscience ila nitakujibu kadiri ya uwezo wangu ni kuwa katika ubongo kuna system(mfumo) maalum unaohusika katika maswala ya kumbukumbu ambayo kiujumla huitwa LIMBIC SYSTEM ambapo katika lymbic system kumegawanyika sehemu nyingi ila mfano wa hizo ni ( olfactory bulbs, hippocampus, amygdala, anterior thalamic nuclei, fornix n.k) sehemu hizi kama ilivyo kawaida zina mfumo wa neurone kama tunavyojua ubongo una neurons nyingi ambazo zenyewe ndo huwa kama njia ya kusafiririsha tarifa kwa njia ya umeme(electrical impulse) sasa turudi kwenye swali lako ni kuwa katika mfumo huo wa kumbu kumbu huwa kuna kitu wanakiita sensory processor (mchanganuo hisishi) ambao wenyewe huwa unapokea taarifa kwa mfumo wa kemikali(chemicals) au physical vibrations (mawimbi mtikiso) yaani utakapoona tukio ili lihifadhiwe na kwa kumbu kumbu basi mfumo huo utapokea either mabadiliko ya ki kemikali eneo hilo au utapokea mtikisiko maalum ambao utahifadhiwa kipawa chake katika hyppocampus na baada ya hapo kama utakuja kuona tukio hilo hilo basi tukio hilo husababisha utumwaji wa taarifa kama ya awali yenye kipimo (intesity) sawa na kile cha awali basi hapo ubongo wako huweza kupima kiwango cha taarifa kama ni sawa na kile cha awali hii husababisha wewe kupata kumbukumbu:
Mimi ndo hujua hivyo mkuu kwa hiyo kumbu kumbu si invisible bali ni STIMULI ambayo inahifadhiwa kwa mfumo wa chemical change au physical vibrations kwenye ubongo .
 
Asante sana kwa ufafanuzi... Lakini huu bado ni ufafanuzi wa kisayansi zaidi kuliko kiroho... Sayansi ina maelezo mazuri sana lakini inapokuja kama ukiwa wa kiroho utaendelea kuhoji na kuhoji na mwisho wa siku tutarudi kwenye nishati roho (spiritual energy) kama kisababishi cha kila kitu
Sasa iko hivi mfumo mzima wa kitendo ambacho automatically huanzia kwenye fikra, mchakato wake mpaka kufikia kuwa kumbukumbu, ukiachana na kile kitendo halisi mengine yote ni invisible
Kumbukumbu hugeuza visible tu pale unapoziwakilisha kwa maandishi, picha michoro ana kitu... Kwa mfano linatokea tukio la mauaji mtaani.. Halafu kwenye upelelezi polisi wanakuja na picha ya mtuhumiwa... Inatokea ulimuona mtu wa namna hiyo... Hapa sasa unavuta kumbukumbu.. Kitu kilichokuwa visible kilichanyatwa na kuwa invisible na sasa unajaribu kukigeuza visible tena kwa kutoa maelezo na kusaidiwa kuchora picha yake
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…