Mkuu wa emergency dept anazuia gari kwenda kumchukua Daktari mwenzake aliyeokotwa akiwa hajitambui?
Aisee ndiyo maana migomo yenu haifanikiwi wakuu...
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
Kwanza kabisa siungi mkono kwa jinsi iwayo yote matumizi ya nguvu kwa mwananchi wa kawaida kama Dr. Ulimboka. Yeyote aliyefanya ama kuruhusu haya kufanywa ni mtovu wa maadili na hapaswi kuwa uraiani - sehemu stahiki anayotakiwa kupelekwa ni segerea ama eneo jingine linalofanana na hilo. Ila bado nina utata kuhusu mazingira aliyokamatiwa Dr. Ulimboka. Walikuwa wanafanya nini kwenye hivi vikao vya usiku alivyokuwa akifanya na wenzake? Je vilikuwa vinahusu nini? Inakuwaje masuala ya mgomo wa madaktari yajadiliwe usiku wa manane kwani kwani yamekuwa uchawi?
Acha upumbavu wewe ndugu zako c ndo huwa wanaenda kutibiwa india! Unapenda huduma za dhaifu za hospital zetu?Ndugu zetu wangapi wamepoteza maisha katika mgomo wa kwanza mbona hukusema kitu, leo Uli unajifanya kuongea sana, acha unafiki wa mawazo.
If they wanted him DEAD, he'd be dead by now, na mngekuwa mnaongea mambo mengine kabisa.......probably, they still need him for something..........the big question is wat is it??
and kimtazamo wangu, 1st, wat has bin done to him isnt fair, Unless, he(ulimboka) framed it....najua kwa hili, wengi mtanilaumu, but mkisoma stories nyingi kama hizi, mtaona, ulimboka hatokuwa wa kwanza, kufake something like this, but FOR GOOD REASONS..............cause, seriously, kama wangetaka afe, angekufa longtym........
2dnly, killing one person for the benefit of two or more people, i find it reasonable................
Hawa ndio watanzania ndugu yangu likishatokea jambo kila mmoja anatengeneza story yake. Hakuna tofauti na hekaya ya Abunuasi
Serikali na Usalama wameumbuka walizani wameuwa,
Damu ya Ulimboka itakuwa chachu ya ukombozi wa Tanzania (Tunisia)
ya pili hiyo imewadia
"Ndugu zangu,
Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".
Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.
Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...
Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.
Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.
Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy aliyehusika kumsaka kama nilivyoyanukuu Mabadiliko Group.
Huyo Dr Ulimboka siyo COMANDO,atakuwa ni mla rushwa (CORRUPT) sana na inavyoonekana anaweza kuwauza wenzake.Nasema hivyo kwa sababu ukiiangalia hii incidence unaona kuwa huyu Dr Ulimboka ana tamaa ya pesa na anaendesha mgomo kwa kushawishi wenzake ili anufaike binafsi.Nasema hivyo kwa sababu hebu fikiria kwa akili ya kawaida tu,wewe una ishu kubwa kama hiyo ya mgomo,halagu unaitwa na mtu usiyemjua ili mkafanye reconcilliation na wewe unaenda tena peke yako!!!!.Bila shaka ni reconcilliation kuhusu mgomo.Hapo naona kuwa anaweza kuitwa na watu asiowajua na yeye akaenda tena peke yake!!!!.Baada ya hapo anaweza kuwageuka wenzake.HAFAI KABISA ANASUMBULIWA NA TAMAA NA NJAA TU.
Kama umesoma vyema maelezo hayo kabla ya yote alikuwa na Daktari mwenzake, kisha wakamteka pekee, lakini mpaka maelezo hayo yanapatikana, Dk Ulimboka amefanikiwa kuzungumza kwa taabu sana, na hata baadhi ya vyombo vya habari vimeweza kuzungumza naye kama Clouds Tv japo anazungumza kwa taabu sana, lakini maelezo yamesikika.Mimi hapo penye red ndo panaponifanya nishangae sana juu ya hii skendo. Hata kwenye ile thread nyingine nilijikuta nashindwa kuamini kama serikali imehusika.
Swali langu ni kuwa "Ulimboka alitekwa peke yake, na baada ya kuokotwa alikuwa hana fahamu na hawezi kuongea. Je, haya yaliyomtokea kayasema nani?
kauli tata ya "liwalo na liwe" imeanza kufanya kazi kabla
cacico, kwa matamshi haya? Umifanya siku yangu kuwa siku muhimu. Thanks for the comments, have no problem I understand you!!!wewe kama ni mwanaume ni hasara kwa nchi hii, huna faida! Na kama ni mwanamke, beba ujasiri tuliojaliwa wa kuleta binadamu duniani tuwapo labour, tetea nchi yako! Acha uoga!