A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

kwa mwenye ushahidi wa uhakika aupeleke polisi au aongee na vyombo vya habari. tuache unafiki.

MOD: FUNGA HII THREAD!!!!!!!!!!!!!! HATUWEZI KUJADILI SWALA BASING ON RUMOURS / TETESI

Apeleke ushahidi wapi?? POLISISIEM!? unanengua wewe, tulishashtuka longtime kitambo,imebaki na sisi raia tuunde chombo chetu cha usalama kwani vingine vyote vimebaki ni usalama wa nyinyiem na baba mwanaasha. shame on you VAMPIRES!!!!,your days are numbered!
 
Nimefanikiwa kuona hiyo clip akielezea kilichomkuta nimejikuta mwili ukizizima kwa hasira!!

Kwa mwendo huu nchi hii lazima tupeleke watu ICC.....

Kaburini patawafaa zaidi
 

ulikuwa wapi wewe siku zote ..unajitokeza leo kwa mgongo wa dr.ulimboka ..chama chako cuf kimekushinda kinakufa..acha kutuharibia amani yetu watanzania wewe..nenda kajenge chama chako huko usijenge kwa kushawishi watu wavunje amani..uandamane mwenyewe. Alafu una ushahidi gani kama ni usalama wa taifa wamefanya hivyo.. Nafikiri elimu yako haikusadia mtatiro.
 
Watawala waliua manabii ili kuzuia ujumbe wa manabii lakini, walikuja manabii wengine na ujumbe ukawafikia watu.Ya Ulimboka yanapita tu lakini tutafika.Nchi imeuzwa.
 
Mnakumbuka yale mauaji ya Gen Kombe 1996? Ilikuwa aibu tupu! Mkewe Rose aliyekuwa eye witness wakati Kombe anamiminiwa risasi kwenye shamba la mahindi hakuitwa kama shahidi pale awali kwenye kesi ya wale askari waliomuuwa wakifikiri eti ni jizi la magari liitwalo Mr White.

Baadaye sana, baada ya Waziri wa ndani, Ali Ameir Mohamed kumtembelea Rose na kumuahidi mapesa ndiyo akaitwa kama shahidi lakini alifundishwa ya kusema.
 
Mtatiro anawajua vizuri watu wa TISS sijui kapata wapi ujasiri huo tena?

anawafaham mana wakat mi nipo chuo first year ye alikua fourth year udsm, alikua mwanaharakat wa ukweli, so i blv he z sayin the truth.
 
-Miaka saba imepita,
tangu ulipoibuka,
jemedari kujikita,
harakati kuongoza.
-Hatamu ukazishika,
kuongoza tafakari,
imetosha kupigika,
kwa maslahi kiduchu.
-Daktari sio punda,
wa kubebeshwa mizigo,
na mgongo kumpinda,
daima akitumika.
-Wito isiwe ni fimbo,
ya kutodai mafao,
msitupiwe makombo,
wengine wakila kuku!
-Pamoja mkashikana,
kudai haki zaidi,
na sime mkatiana,
mkasimama imara.
-Sumaye akawajia,
kwa makeke na mikwara,
mwishowe akachukia,
kuambiwa iwe noma.
-Uli hukutetereka,
na mwenzio Kigwangwala,
wala hamkutishika,
kucheleweshwa hitimu.
-Hukuwa mbinafsi,
japo walikuandama,
ukazikosa nafasi,
ajira serikalini.
-Wengi walifaidika, kwa majitoleo yako,
ijara kuongezeka,
japo hukuifaidi
-AMO, CO na nesi, wote walichekelea,
nao wakajinafasi,
kupitia jasho lako.
-Maisha yakasogea,
na siku zaendelea, wapo walokusahau,
na wala siwalaumu.
-Mwaka huu ukaanza,
na mambo yake ni mapya,
Njelekela kajiponza,
Interns kuwachokoza.
-Kaka zao wakaguna,
mbona mnawaonea,
wakaamua kwa kina, na utangazwe mgomo.
-Ulimboka hukulemba,
unahodha ukashika,
vuguvugu likatamba,
nchi ikatikisika.
-Pinda katoa vitisho,
watu wakamtazama,
likamtoka na jasho,
hadi kwenye meno yake.
-Mwisho kadai suluhu,
ahadi akazimwaga,
na mrejee kazini,
yote yatatekelezwa
-Kumbe ni danganya toto,
hakuna lililojiri,
mazingira na kipato,
vyote vikatelekezwa!
-Madokta wakagoma,
Rais akawasihi,
na wao wakamsoma,
wakarejea kazini.
-Siku tisini zapita,
madai yajadiliwa,
mwisho tamko lapita,
hakuna pesa hazina.
-Madokta wajadili,
hili haliwezekani,
huu ni udhalili,
fani yetu kutendewa.
-Wakaitisha mgomo,
juni ishirina tatu,
usokuwa na kikomo,
huu ni aina yake!
-Kortini wakaenda,
serikari wasikivu,
kuuzuia mgomo,
wajifiche udhaifu.
-MAT wakaishitaki,
na kujitoa akili,
ya kwamba ni jumuia,
iloitisha mgomo.
-Walipokuja ng'amua,
ya kuwa wamepotoka,
Ulimboka wamsaka, na kumtia nguvuni.
-Walimpiga vigongo,
na taya wakamvunja,
wakamponda ubongo,
ili akome fikiri.
-Na mbavu wakamvunja,
msituni wambwaga,
maskini kajikunja,
wakadhani amekufa
-Ujumbe kwao majuha ,
waliyoyatenda haya,
damu ya Dokta Uli,
haitamwagika bure.
-Amani tunda la haki, hailetwi kwa mtutu,
kwa vile wastahiki,
madokta watashinda.
-Na daima mkumbuke,
mabavu yana mipaka,
mamlaka yenu yote,
yatoka kwa wananchi.
-Daktari Ulimboka, ninakuombea heri,
Mungu akupe fanaka,
na afya njema daima.

MWENYE HAKI DAIMA ATASTAWI KAMA MTENDE, NAAM, KAMA MWEREZI WA LEBANONI!
 
Mhxx, watakufa wamesimama hawa wauaji. Ukiua kwa upanga,utakufa kwa upanga.Mwisho wao ni mbaya sana,
 
Busara itumike zaidi. tutawale hisia zaidi. Mungu alitupa macho mawili, masikio mawili na mdomo mmoja, ili tuone mengi, tusikie mengi na tuseme machache.
"Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibari, rip Tanzania"

Alitupa na mikono miwili na vidole kumi,ili tushike keyboard tuandike saaaana!
 
Big up Sunday Charles aka Julius Mtatiro kwa points zako wachane hao wachane!
 
polisi imemkamata gaidi wa al shabaab haitashindwa hawa wahuni wachoma makanisa na kuteka watu. Mia
 

natamani kina Dk.Slaa watangaze tahir square yetu mara moja shughuli ya kumuondoa Kikwete ianze.
 
Umetisha sana mkuu, Mungu atamsaidia na atapona kwa uwezo wake Inshaallah.
 

i like that
 

MWISHO WA UBAYA NI AIBU,Serikali ya ccm aibu kwenu kwa kuwaua wanaodai haki zao za kimsingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…