Wazee wetu punguzeni nongwa, ubinafsi na roho mbaya

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,694
11,019
Wazee wetu punguzeni nongwa, ubinafsi na roho mbaya. Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wamekuwa ni miongoni mwa sababu mojawapo ya vijana wengi kunyimwa ajira kwa kigezo cha uzoefu. Wazee wanawasagia kunguni vijana.

Sasa kumezuka wimbi kubwa la wazee kulazimisha kupewa msaada wa hali na mali, kijana anapambana huko na wengine mpaka wanafanya dili za haramu roho mkononi ili tu kuzitengeneza future zao cha ajabu mzee akikuta kijana amejipanga na kujijenga anaanza kulazimisha kupewa msaada wa hiki na kile tena kwa kulazimisha kama vile haelewi hali ilivyo, wazee wetu ujana wenu mlikula na nani?

Punguzeni nongwa, ubinafsi na roho mbaya wazee. Kama ulishindwa kupambana na kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha yako kipindi cha ujana wako sasa hivi ndio unakumbuka kujifunika shuka wakati ndio kunakucha?
 
Waulize ambao baba zao waliwakataa walimiss nini kutoka kwao? Halafu next time hata ukiwa na povu unakufa nalo moyoni. Hao ndo Wazee, huwezi kuwalipa hata alichokifanya mpk leo ukapata ujasiri wakuongea hivyo.
 
Wazee hawa si ndiyo waliokugharimia shule na sasa wanaendelea kuwagharimia wadogo zako watano waliobakia akiwapo yule kitinda mimba aliye darasa la 4? Wakiyafanya hayo huku wakikabiliwa na mzigo mkubwa wa Kodi na tozo zisizokuwa na idadi?

Umewahi kuzisikia tozo za Mwigulu, Kodi za viwanja, Kodi za pango, Kodi za mapato, VAT na tozo kila mahali hadi kwenye kulipa kodi na mlolongo wa kodi usiokuwa na kikomo?

Ina maana kama walamba asali walivyowatelekeza watanzania wanaowakamua kodi, nawe umewakamua wazee wako na sasa mjanja ni wewe na wajinga ni wao?

Haya kula maisha.

"Kijana wa hovyo usiyekuwa na mchango wowote kwa taifa hili."

Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom