manyanyaso2012
Member
- Jun 18, 2012
- 5
- 0
Mkurugenzi wa NHIF kuongezewa muda wa kuliongoza shirika ikiwa ameshatimiza muda wa kustaafu. Hivi serikali yetu inatupeleka wapi.
Mkurugenzi wa nhif kuongezewa muda wa kuliongoza shirika ikiwa ameshatimiza muda wa kustaafu. Hivi serikali yetu inatupeleka wapi.
Mwenzenu ana Masters ya Facebook, someni na nyie.
Lawama ni za pande mbili zote - serikali pamoja na huyo mkurugenzi. Kwanini hawakufikiria succession planning in advance? Hawakujua kuna siku itafika nafasi itatakiwa ikaliwe na mtu mwingine? Kwa nini hawaandai watu mapema katika kuwajengea uwezo?
Mkurugenzi wa NHIF kuongezewa muda wa kuliongoza shirika ikiwa ameshatimiza muda wa kustaafu. Hivi serikali yetu inatupeleka wapi.
Mbona hata World Bank wanafikiria kuongeza muda wa kustaafu to 65 yrs?
Watanzania tuwe na moyo wa shukrani. Huyu CEO amefanya kazi kubwa sana kwa Shirika hili. Amelitoa mahali ambako lilikuwa halionekani, na leo hii ni chombo cha kujivunia. Dosari ndogo ndogo zipo, lakini hasisababishwi na yeye bali mfumo mbovu wa Watanzania kuchakachua kila kilicho mbele yao. Kuna watu wanadanganya kwenye matibabu, wenye hospitali wanadanganya ili wapate malipo kwa kazi hewa, sisi wenyewe mitaani tunapeana vitambulisho ili tutibiwe bure, kuna viburi vya watoa huduma hospitalini, n.k
Huyu ana manufaa zaidi kuongezewa muda kuliko wale ndugu zetu wanaoshinda ndani ya Bunge kazi yao ikiwa kukusanya posho kila kona!
Wanaofanya kazi nzuri tuwapongeze. Tusiwakatishe tamaa. Ikibidi waongezwe muda tu wachape kazi. Kuna vijana wengi wasio na weledi wala uzalendo. Tumewaona. Tumewajaribu. Wamefeli.