6 UDSM students died in taqwa bus accident

6 UDSM students died in taqwa bus accident

Mh, kwa jinsi navyoyafahamu mabasi ya Taqwa, wala hili siyo kazi ya Mungu. Nilimsindikiza ndugu yangu mwezi wa saba lakini roho ilibaki juu juu. Wanajaza sana mizigo, sehemu ya kupita abiria ilikuwa imejaa mizigo yani kukaa kwenye siti inabidi upite juu ya mizigo n.k basi halina utaratibu, abiria wanagombea siti kwa sababu wamekatiwa tiketi mara mbili mbili. Poleni wahanga, wenye kampuni wachukuliwe hatua, kuna uzembe mkubwa hapo
 
Kweli kabisa mkuu mimi sina hata wiki nimepanda bus hilo hali ni mbya sna hasa kwnye upangwaji wa mizigo na habiria.kwnye bus walikuemo wafaransa wanalia 2 wanasema ths is not for people ts for animals,maskin ya mungu makonda walikua wanawjbu jeuri na abiria walikua wakshangiria tu inauma but anyz.REST IN PEACE
 
Kwa sababu kazi ya Mungu haifanani kila mahala. Kazi ya Mungu Japan ni kuwapiga na matetemeko ya ardhi. Sisi hapa ni kutuua na ajali. Siku yako ya kufa Mungu ndio anaijua na Mungu ndio anapanga yote. Wameenda kupumzika na Bwana. Tuliwapenda lakini Mungu amewapenda zaidi. Bwana ametoa, Bwana ameua.

Kazi ya Mungu haina makosa.

Naomba mwongozo. Bwana anaua? Kama bwana ametoa then bwana anachukua binadamu ndiyo wanaua.
 
Kifo kimepangwa na mungu,dreva wa ile bus anaitwa Sultan Mohammed ni ni Uncle wangu mimi,na nyuma ya siti yake alikuwa amekaa mama yangu mkubwa ambae yeye ni dada yake,akiwa pamoja na mke wa mjomba wangu ambae dreva anakuwa ni mke wa kaka yake,pamoja na dada yangu ambae yeye drive ni uncle wake mtoto wa dada yake,na wote wamekufa pale pale,
Sasa kama hakuthamini roho za watu hata yake? Hata hawa ndugu zake? Ajali ni mipango ya mungu,kama kuna family ambayo imepata pigo kubwa katika hiyo ajali basi na family yetu,ambae dreva wa bus akiwemo,inauma sana lakini tunamshukuru mungu hatuna hilla kwa hilo,na mungu atawalaza pema mote waliopoteza maisha

Du! Pole sana ndugu yangu, familia imepata pigo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom