Basi la Kampuni ya Abood Bus Service lagongana na gari dogo maeneo ya Mikese

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi la Kampuni ya Abood Bus Service linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda Morogoro, limepata ajali ya kugongana na gari dogo aina ya Toyota Raum Jana maeneo ya Mikese mkoani Morogoro.

Taarifa zinasema hakuna vifo na abiria walioko kwenye basi wametoka salama pamoja na dereva wa gari dogo kupata majeraha madogo.

Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Abood Bus Service, kuovertake gari iliyokuwa mbele yake bila kuangalia usalama, hivyo kusababisha kugongana uso kwa uso na gari dogo.

IMG_20191115_083104_999.jpeg
 
Abood inabidi ajifunze kwa kampuni ya zamani Scandinavia.
Kuajiri madereva wenye weredi wa kazi yao.
 
Wiki mbili zilizopita kuna dereva wa Abood bus Service aliliagusha maeneo ya Temboni, na jana dereva wa Abood kafanya uzembe kuovertake bila tahadhari

Tunawasihi madereva wa mabasi kuwa makini wawapo barabarani..Poleni abiria kwa hiyo taharuki.
 
Hawa wanategemea ukiwa na gari ndogo uwapishe lakini mara nyingine unakuwa huna sehemu ya kupisha matokeo yake ndio haya.
Reflex. Ni kitendo cha kibinaadamu kukwepa ambacho hutokea kwa haraka bila mtu mwenyewe kupanga. Mwenye Raum alishamkwepa kwa kutoka nje ya barabara na mwenye basi naye akataka kukwepa kwa kutoka nje ya barabara!
 
Nawaza SGR ikikamilika, Moro - Dar itakuwa ni train tu, mabasi yatapigwa marufuku kama walivyofanya kwa BRT.
Ni upuuzi kupiga mabasi marufuku.... Kama treni litakuwa linatembea muda mfupi kuliko mabasi. Basi watu wengi watahamia kwenye treni simple tu kama hivo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom