5G vs Starlink

Dah! hii comparison haiendani hata kidogo, unalinganishaje mnara na router ya starlink...?
Mnara unabebeka? umeme unaotumia mnara na gharama za uendeshaji utalinganisha na ki router cha starlink?

Haya ukitaka kusafiri kabebe mnara uwe unatembea nao...

Kama satellite ilikuwa gharama na spaceX wametengeneza satellite zaidi ya 7578 zinazunguka angani watashindwa tengeneza ground stations za kutosha EA hapa?
 
umeambiwa starlink ni ghali na sio 5G acha kuhamisha mafaili.
 
My point is satelite zao zimeshindwa kuhuduMia watu 19,000 tu kiasi ambacho minara miwili tu inahudumia bila shida, itawezaje kukomboa watu milioni 60 wakati 19,000 imeshindwa?

Na Elon hawezi kukuletea satelite 7000 ni matrilioni ya hela, kwake yeye ni faida zaidi kununua mitandao yote ya Tanzania kuliko kuleta hizo satelite.
 
sio kweli acha kukakaza fuvu. kustream content sio lazima eti ulipie app. mimi huu mwaka wa 4 siwajui azamtv lakini Nbc ligi nacheki bila usumbufu na mbs kidogo. kuhusu starlink kutumika hata ngorongoro ni kweli ila itahitaji uwe eneo husika yaani usiondoke happ. na miaka hii ngumu kukaa sehemu moja,
 
nani kasema fiber? khee. mimi nazungumzia mobile internet 5g na sio mambo ya faiba. huu sio ulimwengu wa maantena ndugu. yaani unanibebesha begi ukiulizwa eti antenna
 
line of sight niliizungumzia kwa sababu wewe umetuambia eti unaweka antenna kwenye begi(😂) sasa ukishaweka kwenye begi, line of sight itawezekana?
 
Hapo hujaelewa kitu mzee..
Satellite moja ya starlink inaweza hudumia watu hadi 5000 na zaidi kwa wakati mmoja...

Nimekuelezea hapo kwamba bado starlink hawajaweka ground stations za kutosha, Africa nzima kuna ground stations mbili tu , moja ipo Nigeria nyingine Nairobi.. hizo ndizo zinahudumia Africa yote...
Tatizo sio satellite, tatizo hapo ni ground stations....

Kama huku mnavyopambana na kujenga minara toka 1990s, starlink ya juzi hapa inaendelea kujenga ground stations , Nigeria sasa wanaendelea na ujenzi katika miji mitatu Lagos, Ogun, na Port Harcourt.

Mwezi march hapo Msumbiji wametengeneza kituo hapo Msumbiji kwa ajili ya ku feed connection Kusini mwa Jangwa la Sahara, hasa kwa nchi jirani kama Zambia na Zimbabwe..

Kama starlink wana satellite zaidi ya 7578... hawashindwi kutengeneza ground stations(PoP) za kutosha hapa East Africa..

Hadi sasa kuna Point of Presence mbili tu Africa kote, moja ni Nigeria na nyingine ni Kenya...

Gharama moja ya kutengeneza satellite ya starlink v2 mini ya kisasa ni dola $200,000–$300,000 kwa satelaiti moja.. ikiwa ni pamoja na ujenzi, majaribio, na urushaji...
Starlink inarushwa kwa kutumia roketi za Falcon 9 kutoka SpaceX, kwa gharama ya karibu $67 milioni kwa roketi moja, inayobeba satelaiti kati ya 22–60.

Tuje kwenye gharama ya ground stations...
Kituo cha PoP cha Starlink, ground station yenye dishes kubwa, fiber connection na data center ndogo hugharimu Takribani $50,000 hadi $250,000 kutegemeana na eneo...
Hapo Gharama ni ya kujenga, kuweka vifaa, na kuunganisha na fiber kwenye internet backbone...

Hivyo elewa Satelaiti ya Starlink ni ghali zaidi kutengeneza na kurusha kuliko PoP ya ardhini lakini bado angani wana satellite 7578, watashindwa kusambaza hizo PoPs bara la Africa?
 
nani kasema fiber? khee. mimi nazungumzia mobile internet 5g na sio mambo ya faiba. huu sio ulimwengu wa maantena ndugu. yaani unanibebesha begi ukiulizwa eti antenna
Nani anataka 5G ya 1GB unanunua Tshs 2000, ukisafiri kwenda nje ya mji connection hakuna...
 
Hujui chochote acha kujitia ujuaji ndugu, starlink wanaweka hadi kwenye gari na ndege na boti, gari inakwenda na internet unapata... punguza ujuaji mkuu..
 
line of sight niliizungumzia kwa sababu wewe umetuambia eti unaweka antenna kwenye begi(😂) sasa ukishaweka kwenye begi, line of sight itawezekana?
Nilisema n portable...
Na mimi nikauliza ukienda nje ya mji utabeba nyaya za faiba... au utabeba mnara wa 5G hadi nje ya miji au vijijini?
 
Kwanza unakandia fiber halafu kila comment unasifia Ground station, unajua kama ground station ni fiber?

Lete ushahidi hapa Satelite ya starlink inahudumia watu 5000 kwa pamoja.

Satelite moja ina Bandwidth 20Gbps kwa speed ya 200mbps ni watu 100, na kwa hio 47mbps ni watu 450, ingekua inahudumia watu wengi hivyo why ishindwe kuhudumia watu 19,000?
 
Huelewi nini hapo?
KInachopelekea Kenya starlink imesimamisha watumiaji wapya sio satellite ni ground stations chache...
Satellite za sasa zina tech ya ISL hazitegemei sana ground stations, lakini starlink huko angani wana satellite pia zile za kwanza ambazo zinategemea ground stations... hivyo zinatumiaka bado..

Nimeeleza pia hata kama starlink wataleta hizo starlink za kisasa v2 ambazo zina tech ya ISL ambayo inasaidia kutotegemea zaidi ground stations bado kusheria nchi nyingi wanahitaji ground stations ili wadhibiti data za watumiaji wao.. umeelewa hapo?

Narudia tena hao watumiaji 19,000 wa Kenya wanaweza kuhudumiwa na satellite nne tu za starlink... umeelewa hapo,? tatizo ni ground stations ambazo bado zinasambaa baran Africa..
 
Si Kweli Kenya wameanza kutoa huduma bila ground station na Ground station ndio mpya ya karibuni.

Tofauti na Kuwa na ground station ama kutoka na ground station ni ping, ukiwa na ground station inasaidia kupunguza latency ila satelite ndio inaamua capacity.
 
20Gbps ni generation ya kwanza, wanazorusha sasa hivi 2nd Gen zinafika 98Gbps, 3rd Gen ni 1Tbps so it gets better overtime.

Also hio 20Gpbs ni kwa beam moja tu inayopiga eneo flani so kutegemea na configuration kama satelite ina multiple beams mpaka 16 means 1st Gen tu inaweza kuhudumia clients mpk 1600 at 200Mpbs. 2nd Gen inaweza kufika 10,000 clients etc.
 
Hizo V2 Starlink mini inatoa beams hadi 60 na hio inayokuja itatoa beams hadi 100..
 
V3 ni future so far ipo kwenye makaratasi zaidi, ina gharama zaidi, nzito zaidi etc haiwezi kuwa solution kwa huyu anaelipa Laki East Africa.

For the sake of discussion tu assume East Africa wanatumia latest satelite kushinda hata Usa unagota hapo ~90Gbps ambayo still haihudumii hao watu 5000 anaosema jamaa.

Hakuna data ambazo zinaonesha exactly satelite ngapi zipo deployed Africa ila uki judge kwa hio Ramani ya starlink zinaweza fika hata 100.ama zaidi. No way satelite 4 zihudumie hao watu
 
The way constellation ya Starlink inafanya kazi ni engineering marvel. The system works like a live organism, kama ambavyo white blood cells zinakuwa dispatched kwenda eneo husika kufanya kazi, Starlink automatically ina-allocate more satelites kadri demand ya eneo husika inavyoongezeka. Since demand sio static so number of satelites sio static kwenye eneo flani ina-vary. Uwezekano wa sat moja kuhudumia 5000+ clients ni uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…