529 wahukumiwa kifo Misri!

529 wahukumiwa kifo Misri!

Neiwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
728
Reaction score
634
Mahakama nchini Misri imewahukumu kifo watu 529 ambao wanasemekana kuwa wafuasi wa Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed Morsi. Watu hao walikabiliwa ma mashitaka mbali mbali yakiwemo mauaji ya polisi na kuwavamia polisi.

Wafuasi hao wa chama kilichopigwa marufuku, cha Muslim Brotherhood, ni sehemu ya kundi lengine kubwa la watu zaidi ya 1,200 wanaoaminika kuwa wafuasi wa Morsi. Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa wakiendesha msako mkubwa dhidi ya wafuasi wa vuguvugu hilo, tangu Morsi kuondolewa mamlakani mwezi Julai mwaka jana.

Maelfu wamekamatwa huku mamia wakiuawa. Mahakama hiyo ilitoa hukumu baada ya vikao viwili pekee ambapo mawakili wa watuhumiwa walilalamika kuwa hawakupewa muda wa kuwasilisha kesi yao vyema.

Mauaji wanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa yalitokea Kusini mwa Misri, mwezi Agosti, baada ya vikosi vya usalama kuvunja kambi mbili za wafuasi wa Morsi waliokuwa wanataka arejeshwe mamlakani.

CHANZO:
Watu 529 wahukumiwa kifo Misri! | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
An Egyptian court has sentenced 529 members of the outlawed Muslim Brotherhood to death on charges including murder, a defence lawyer said, in a sharp escalation of a crackdown on the movement.

Those convicted are part of a group of 545 defendants on trial for the killing of a police officer, attempted killing of two others, attacking a police station and other acts of violence.

"The court has decided to sentence to death 529 defendants and 16 were acquitted," lawyer Ahmed al-Sharif told Reuters news agency on Monday.

The ruling can be appealed.

The trial is part of a government crackdown on the Muslim Brotherhood that started after the removal of President Mohamed Morsi in July.

Most of the defendants were arrested during clashes which erupted in the southern province of Minya after the forced dispersal of two Muslim Brotherhood protest camps in Cairo on August 14.

Only 123 of the defendants were present. The rest were either released, out on bail or on the run.

A second group of about 700 defendants will be in the dock on Tuesday. They are accused of attacking both people and public property in southern Egypt in August.

The government has declared the Brotherhood a "terrorist" group.

It comes as Al Jazeera journalists will be returning to court as part of their ongoing trial for spreading false news and being part of a terrorist organisation.

Al Jazeera denies all charges levelled against its staff.

Source: http://www.aljazeera.com/news/middl...mbers-sentenced-death-201432481112672803.html
 
Mahakama ya Misri imewahukumu kifo wanachama 529 wa Muslims brotherhood.

Src: cnn

Huu ni uonevu mkubwa wa haki za binadamu!!! Ili mtu ahukumiwe kifo ni lazima ahusike moja kwa moja katika kuua!!! Au wao wanatumia sharia law!!?? Ndiyo maana tunaomba Tanzania ikae mbali na mahakama ya kadhi!!! cc FaizaFoxy
 
Mahakama ya kadhi ya Tanzania haitoshughulikia makosa ya jinai na uhaini.
 
Haya makabila ya jangwani yashazoea kuchinjana kwao hao sio watu ni kama kunyonga kuku tu!
 
Huyu myahudi si atawamaliza sasa hawa wamisri.
 
Huu ni uonevu mkubwa wa haki za binadamu!!! Ili mtu ahukumiwe kifo ni lazima ahusike moja kwa moja katika kuua!!! Au wao wanatumia sharia law!!?? Ndiyo maana tunaomba Tanzania ikae mbali na mahakama ya kadhi!!! cc FaizaFoxy

Hili jambo halikubaliki, inabidi Makamanda USA waingilie kati, hao watu ni wengi mno kuuawa
 
Mahakama ya kadhi ya Tanzania haitoshughulikia makosa ya jinai na uhaini.

Asante mkuu, je una chapisho lake tusome!!! Lichapisheni katikamagazeti kama ilivyokuwa kwa rasimu ya katiba ili watanzania tuisome tuelewe!!! Kila kitu ni lazima tuwe na evidence si kuambiwa tu mkuu!! Inatisha!!! Na wakristu nawasihi waombe nao kibali cha kuanzisha ya kwao!!! Kumbe mpasuko si wa Muungano tu, wa Bara na wa Visiwani!!! ni kila mahali sasa!!
 
Hili jambo halikubaliki, inabidi Makamanda USA waingilie kati, hao watu ni wengi mno kuuawa

Kweli mkuu, nimeshangazwa sana. Huyo jaji aliyehukumu hivyo akapimwe akili kwanza!!! Ila hii ni tactic ya siasa kuwatishia brotherhood!!! Waliwafungulia kesi za kubambikiza tu na rais wao ndiko huko huko wanataka kumlengesha!!! Aibu sana hii.
 
Huyu myahudi si atawamaliza sasa hawa wamisri.
Who is General Abdel Fattal el-sis?.
Born to a morrocon jewish mother,his maternal uncle was a member of David Ben Gurion's political party(mapai).
How did this sephardi sleeper stay within the loop without being exposed for so long and rising to the top of
 
Wanaharibu amani hivyo wao ni mfano. Vijana tufanye kazi tuachane na maandamano na fujo
 
Daah! Ni wengi mno. Nina imani wengine watapata msamaha waachiliwe huru. Wakinyonga wote hao basi nchi hiyo itabaki ya visasi. Mungu awajaze busara Wamisri kwani wanapita katika mapito yenye majaribu makubwa kama taifa.
 
Ili mtu ahukumiwe kifo ni lazima ahusike moja kwa moja katika kuua!!! Au wao wanatumia sharia law!!??

Ndugu capital crimes si lazima iwe kwa makosa yanayosababisha kifo i.e murder pekee.

Hii inategemeana na sheria za nchi husika tena mbali kabisa na sharia law.

Mbali na murder offenses hukumu ya kifo kwa baadhi ya nchi yaweza husisha uhaini, ugaidi, illegal drugs, rushwa, ubakaji, biashara ya silaha, usaliti dhidi ya nchi(espionage) etc

Ingawa pia sijapenda hii hukumu lakini nahisi hapa yaweza kuwa kesi ya ghasia ilihusisha pia mashtaka ya ugaidi kwa kuharibu miundombinu ya umma na kusababisha vifo pia.
 
Asante mkuu, je una chapisho lake tusome!!! Lichapisheni katikamagazeti kama ilivyokuwa kwa rasimu ya katiba ili watanzania tuisome tuelewe!!! Kila kitu ni lazima tuwe na evidence si kuambiwa tu mkuu!! Inatisha!!! Na wakristu nawasihi waombe nao kibali cha kuanzisha ya kwao!!! Kumbe mpasuko si wa Muungano tu, wa Bara na wa Visiwani!!! ni kila mahali sasa!!

Ahsante tumekuelewa.
 
Huu ni uonevu mkubwa wa haki za binadamu!!! Ili mtu ahukumiwe kifo ni lazima ahusike moja kwa moja katika kuua!!! Au wao wanatumia sharia law!!?? Ndiyo maana tunaomba Tanzania ikae mbali na mahakama ya kadhi!!! cc FaizaFoxy

Hiyo nzuri sana,kuna watu kama wafuasi wa Lema hawana akili kabisa.
 
Mahakama nchini Misri imewahukumu kifo watu 529 ambao wanasemekana kuwa wafuasi wa Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed Morsi.
Watu hao walikabiliwa ma mashitika mbali mbali yakiwemo mauaji ya polisi na kuwavamia polisi.
Wafuasi hao wa chama kilichopigwa marufuku, cha Muslim Brotherhood, ni sehemu ya kundi lengine kubwa la watu zaidi ya 1,200 wanaoaminika kuwa wafuasi wa Morsi.
Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa wakiendesha msako mkubwa dhidi ya wafuasi wa vuguvugu hilo, tangu Morsi kuondolewa mamlakani mwezi Julai mwaka jana.
Maelfu wamekamatwa huku mamia wakiuawa.
Mahakama hiyo ilitoa hukumu baada ya vikao viwili pekee ambapo mawakili wa watuhumiwa walilalamika kuwa hawakupewa muda wa kuwasilisha kesi yao vyema.
Mauaji wanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa yalitokea Kusini mwa Misri, mwezi Agosti, baada ya vikosi vya usalama kuvunja kambi mbili za wafuasi wa Morsi waliokuwa wanataka arejeshwe mamlakani.

chanzo bbc swahili
 
Back
Top Bottom