Tangu Muslim brotherhood ianzishwe na akina Sheikh Hassan Banna mwaka 1928... na hata baadaye walipokuja kushika akina Sheikh Khutub baada ya kifo cha Banna ambaye inasemekana aliuawa na serikali ya Misri wakati huo, kimekuwa na mifarano mikali na serikali.
Lengo la kuanzishwa kwa kikundi hiki lilikuwa ni ku-renew imani ya kiislam ambayo ilikuwa inaonekana kudhoofu na western culture kuchanua katika ulimwengu wa nchi za kiislam. Kwa muktadha huu utawala ambao ulionekana sana kuwa 'bila din' yaani serikali isiyo na dini, wao waliupinga wakitaka wanachokiita 'din wa dawla' yaani kwao dini na dola ni vitu visivyotenganishwa. Kwahiyo wanachosisitiza ni dola inayoongozwa kwa misingi ya Quran na Sharia.
Kikundi hiki ndiyo mama wa vikundi vingine kama Hizbollah cha Lebanon na Hamas cha Palestina. Kwa misimamo hii mikali ya kundi hili katika historia yake limekuwa mwiba kwa karibuni tawala zote za Misri, likichangia mauaji ya viongozi, kama akina Nasri na wengine wengi; nao pia wakiuwawa kwa wingi.
Hivyo yanayotokea Misri ni kujirudiarudia kwa historia tangu kuanzishwa kwa kikundi hiki cha Muslim Brotherhood, Udugu wa Kiislam.