First Born
JF-Expert Member
- Jul 11, 2011
- 5,310
- 1,473
Nilimuaga mke wangu Ijumaa asubuhi kuwa naenda Dar.
Safari hii alikuwa anaifahamu siku tatu kabla kuwa naufuata mzigo wa biashara! Usiku kabla hatujalala aliniandalia nguo za kuvaa na kubadilisha kwa sababu ningerudi baada ya siku nne.
Kiukweli sikuwa naenda popote, nilikuwa nahamisha makazi kwa mchepuko wangu uliopo maeneo ya sakina-jijini arusha.
Jumapili Muda mchache kabla ya kuingia ukumbi wa Tripple A nilimpigia wife akanipa habari njema kuwa yupo nyumbani na anajiandaa kulala, kelele nilizokuwa nasikia ilikuwa mziki wa nyumbani tu, nikamtakia usiku mwema. Nikamshika mkono mchepuko wangu tukaingia ndani.
Wakati nikiwa nimelewa kiasi huku nikiwa ktk mazingira ya mahaba nikamwona mdada mrembo kwa pembeni akiwa kaegemea kifuani kwa mwanaume, baada ya mda nikawaona wanaondoka, kumwangalia kwa makini zaidi nikabaini ni mke wangu, nataka kwenda kuleta vagi mchepuko ukazingua, akili zikanijia kuwa niliaga niko Dar na leo ni siku ya 3 tangu niondoke hapahapa jijini arusha!
Nikabaki naduwaa nikisindikiza kwa macho!