4R (reconciliation, resilience, reforms & rebuilding) za Rais Samia sio maneno bali anaishi nazo katika matendo yake

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Katika hatua madhubuti ya kurejesha nchi katika hali ya maelewano,usalama,na maendeleo endelevu kufuatia siasa za uhasama zilizorithiwa kutokana historia ya vyama vingi na mapungufu mbalimbali ndani ya vyama vya upinzani pamoja na serikali. Raisi Samia Suluhu Hassan ameamua kujenga nchi yenye watanzania wanaoishi kwa kusameheana, kuvumiliana, kuleta mabadiliko na kujenga nchi kwa pamoja.Mpango mkakati huu unaojulikana kama R4 amekua akiusema na kuishi nao kwenye matendo yake licha ya vikwazo vingi kutoka kwa baadhi ya watu ambao hawana nia njema na nchi yetu.

Historia inaonesha ni wazi kuwa watanzania wengi hawakuwa tayari kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.Hii inatokana na ripoti ya tume ya Jaji Nyalali ambapo ni asilimia 20% ya Watanzania walikubali kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Serikali kwa kuona mbali ili lazimisha Tanzania kuanza mfumo wa vyama vingi kutokana na athari ambazo zingeweza kutokea pamoja na kuanguka kwa mfumo wa ujamaa. Mfumo huu licha ya kuwa na changamoto mbalimbali kutokana na mapungufu yake na mapungufu ya vyama umejenga mahusiano mabaya katika jamii hasa katika vipindi vya uchaguzi. Kutokana na hili na mengine Tanzania imepitia katika majanga mengi ambayo yamepoteza maisha ya watu na mali zao katika nyakati mbalimbali.Raisi kwa kuliona hili ameanza na upatanishi.

RECONCILIATION-UPATANISHI
Hakuna shaka kuwa kila mmoja wetu anajua umuhimu wa kutafuta suluhu na kusameheana kama msingi mkubwa wa kuzuia kutokea kwa mpasuko au kuziba nyufa ndani ya jamii.Jambo hili linafanywa kwa vitendo na Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuongea,kujadiliana na kujenga mahusinao mema miongoni mwa vyama,makundi na kijamii na wananchi kwa ujumla.

Uongozi imara wa Raisi Samia Suluhu Hassan umeanza kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani, makundi mbalimbali, asasi za kiraia na matunda ya upatanishi yanaonekana katika jamii ya watanznaia. Viongozi wakuu wote wa vyama vya upinzani wameoneshwa kufurahia na kuunga mono juhudi za Raisi Samia kwenye sera zake pamoja na nia yake ya kuikwamua Tanzania ilipokuwa imekwama.

Mfano,Raisi ametoa maagizo kwa ofisi ya DPP na Jeshi la Polisi kutizama kesi mbalimbali zikiwemo za wanasiasa ambazo hazina ushahidi na kuwaachia huru wananchi ili warudi kujenga uchumi wa nchi yao.Mwenyekiti wa Chadema ni mmoja wa waliofaidika na hatua hizi za Raisi Samia Suluhu Hassan.Hapa anasema.

“Ningekuwa mjinga kukataa fursa ya kuona Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kutoka gerezani kwa sababu niliitafuta fursa hii kwa muda mrefu ili kuweka msingi wa maridhiano ya kitaifa kuhusu maendeleo ya Tanzania”. Mh Freeman Mboe March 2022.

Kwa kutambua changamoto ambazo demokrasia inaipitisha Tanzania,Rais Mama Samia Suluhu Hasan amewashawishi wanachama wa CCM na viongozi wa Serikali na vyama vya Upinzani kufungua ukurasa mpya wa siasa za demokrasia Tanzania. Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Mh Zitto Kabwe nae anasema

"My presence in this meeting is a clear indication that political reconciliation is your priority; you are looking at Tanzanians as one, neither as individuals nor their political affiliations," Mr Zitto said at a public meeting at Lake Tanganyika Stadium in Kigoma Region October 2022.

"You can do everything in this country for development, but generations will remember you for your ideas and what you're doing... what you've explained in the 4R, is a way to show how you commit to a united country," Mr Zitto said

TUCHANGIE SEHEMU HII YA KWANZA KWA KUELEZA MIFANO AMBAYO INAONESHA UPATANISHI
 
Upatanishi ungeonekana wakweli endapo vyama vingepewa Uhuru wa kufanya shughuli zake kwa usawa na kwa ulinzi wa Dola Kama kifanyavyo chama Dola ,vinginevyo ni mbinu za kuviangamiza vyama vingi.
 
Kuhusu Reconciliation / Maridhiano Raisi anatakiwa aunde TUME ya Ukweli, Haki, na Maridhiano.

Kinyume cha hapo itakuwa ni maneno matupu au danganya-toto.
 
Bro kwani huko kwako Kuna maji na umeme vinapatikana ? au maharage na Mchele shillingi ngapi ? Azia hapo Kwanza ndio uanze kusifia ? Namkumbuka Sana Magufuli.
 
Ambao tupo nje ya system hatuelewi it's becoming worse than ever before
Tuambie wewe ni miongoni mwao?
 
Upatanishi ungeonekana wakweli endapo vyama vingepewa Uhuru wa kufanya shughuli zake kwa usawa na kwa ulinzi wa Dola Kama kifanyavyo chama Dola ,vinginevyo ni mbinu za kuviangamiza vyama vingi.
Kwani kuna chama kimeomba kuongea na wanachama wake kikakatazwa?,Mikutano ya kuwakutanisha watu na kusimamisha shughuli za uchumi ndio inatafutiwa utaratibu mzuri
 
Kuhusu Reconciliation / Maridhiano Raisi anatakiwa aunde TUME ya Ukweli, Haki, na Maridhiano.

Kinyume cha hapo itakuwa ni maneno matupu au danganya-toto.
Vikao anavyofanya na viongozi wa vyama vya upinzani havina hesabu,ukiona viongozi wa upinzani hawalalamiki,jua mambo yanaenda vizuri.Achana na maneno ya watu wa club house
 
Vikao anavyofanya na viongozi wa vyama vya upinzani havina hesabu,ukiona viongozi wa upinzani hawalalamiki,jua mambo yanaenda vizuri.Achana na maneno ya watu wa club house

..za kuambiwa changanya na zako.

..reconciliation huenda pamoja na ukweli na haki.
 
Kuhusu Reconciliation / Maridhiano Raisi anatakiwa aunde TUME ya Ukweli, Haki, na Maridhiano.

Kinyume cha hapo itakuwa ni maneno matupu au danganya-toto.
Naamini falsafa ya "Reconcialition" haihitaji tume yoyote.

Nimeandika machache kuhusu hilo, pitia labda utaielewa:

 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Back
Top Bottom