4. JKT Kama Taasisi ya Taifa, Sio Kambi ya Kuosha Vijana Wakae Kimya

4. JKT Kama Taasisi ya Taifa, Sio Kambi ya Kuosha Vijana Wakae Kimya

CHAGOSI GERALD

Senior Member
Joined
Jan 25, 2020
Posts
162
Reaction score
284
Duniani kote, taasisi ni mahali pa kujenga watu, kuunda fikra, kutengeneza ndoto, na kuibua vizazi vinavyokuja kubeba uchumi.
Lakini kambi ni mahali pa kuamrishwa, kukaa kimya, kutii bila kuuliza, kutumika bila kuulizwa.

"JKT ilizaliwa kama Taasisi. Mfumo uliigeuza Kambi."
Hili ndilo kosa la kihistoria ambalo Watanzania wengi hawajawahi kuliona, wala kulifanyia uchambuzi.
Lakini leo tunavaa mawani ya ukweli - tunakata mzizi wa tatizo.

a) Nyerere Hakutaka “JKT ya Amri”, Alitaka “JKT ya Ujenzi wa Taifa”

Nyerere alijua kitu kimoja:
"Kijana akiwekewa nafasi ya kutengeneza uchumi, atafanya zaidi ya mtu mzima aliyejaa woga, mazoea, na hofu ya kupoteza mali."

Alitaka JKT iwe:
~Shule ya Uongozi wa Kiuchumi
~Kiwanda cha Uzalishaji
~Chuo cha Ubunifu wa Teknolojia
~Sehemu ya kushikilia umiliki wa taifa (Mines, banks, viwanda, mashamba)
~Kisima cha mawazo mapya ya taifa

Alitaka kijana akiingia JKT, atoke akiwa:
-mjasiriamali
-mbunifu
-mzalishaji
-mjenga miundombinu
-mtaalamu
-kiongozi

Yaani JKT iwe kichwa cha roho ya uchumi wa taifa.
Lakini kilichotokea badala yake ni kinyume.

b) Mfumo Uliogopa Vijana — Ukaigeuza JKT Kambi

Mfumo ukasema:
“Ukampa kijana madaraka, atabadilisha nchi kuliko sisi.
Ukampa uchumi, atageuza meza.
Ukampa nguvu, tutafunikwa.”

Kwa hiyo wakageuza JKT kuwa:
~mahali pa kufundishwa kutii badala ya kutengeneza
~mahali pa kuweka vijana busy ili wasiulize maswali makubwa
~mahali pa kuzuia vijana wasigundue uwezo wao wa kubadilisha taifa
~mahali pa kupeleka vijana kwa miezi 3 ili “waheshimu serikali”
~mahali pa “kuchuja ajira” badala ya kuchochea uchumi

Hapo ndipo taasisi ikafa.
Ilipogeuzwa kambi, ndoto ya Nyerere ilikufa kimya kimya.

c) JKT Ilitakiwa Iwe INJINI, Imegeuzwa Magazeti ya Ajira

JKT ya Nyerere ilitakiwa iwe:
-Jeshi la Migodi
-Jeshi la Viwanda
-Jeshi la Kilimo cha Taifa
-Jeshi la Uchumi
-Jeshi la Usafiri
-Jeshi la Ujenzi
-Jeshi la Technologies
-Jeshi la Mawasiliano
-Jeshi la Nguvu Kazi ya Taifa

Lakini leo imebaki kama sehemu ya:
~kuandikiwa majina kwenye “ajira za jeshi”
~kutoa certificate za kuomba nafasi serikalini
~kufundisha parade badala ya mechanics
~kufundisha kuimba wimbo wa taifa badala ya kuunda satellite
~kufundisha kupiga magoti mbele ya bendera badala ya kusimama mbele ya uchumi

Hiki ndicho kilichotuumiza kama taifa.

d) Mfumo Uliweka JKT Pembeni Ili Wafanyabiashara Wachache Wapate Riziki ya Taifa Zima.

Wakati Nyerere akisema:

“Rasilimali ni za vijana, vijana ni JKT.”

Mfumo ukasema:
“Rasilimali ni za marafiki wa chama na wafadhili wa siasa.”

Matokeo yake:
~Migodi ikachukuliwa na makampuni ya nje
~Benki zikabinafsishwa
~Viwanda vikauzwa bei ya kahawa
~Ardhi ikawa soko la ukiukaji
~Mabillioni yakawa mikononi mwa watu 50
~Taifa lote likawa maskini kwa hiari

Na JKT ikabaki pembeni, ikitumia bajeti ya kubembeleza badala ya bajeti ya kujenga uchumi.

e) Tatizo Kubwa: Mfumo Unataka Kijana Aishi Bila Kujiuliza.
-Mfumo ulihakikisha:
-kijana asiulize maswali
-kijana asifikirie tofauti
-kijana asiamini ana uwezo
-kijana asihoji mfumo wa kiuchumi
-kijana asiulize ‘kwa nini hatumiliki migodi?’
-kijana asiulize ‘ivi kwa nini nchi tunaijenga sisi lakini tunaiendesha kwa mikopo?’

Ili kufanya hivyo, JKT iligeuzwa kuwa mahali pa ku-discpline vijana, sio kuwaweka huru kiuchumi.

“Taasisi Iliyouawa, Vijana Walioachwa Yatima”**

Nitarudi tena.
 

Attachments

  • Picsart_25-12-02_19-02-11-488.jpg
    Picsart_25-12-02_19-02-11-488.jpg
    306.3 KB · Views: 12
Back
Top Bottom