Nimekuelewa sana mkuu kila kitu kitakuwa wazi. Sijataka kuweka hapa namna ya kuzinunua sbbu tunahitaji kuweka kila kitu katika misingi iliyo sawia isiyotia shaka. Ila kwa sasa ni vema watu wakajua kuwa hazitagawiwa bure ila zitauzwa.Usilaumu watu hapa. Wewe umeweka meseji/tangazo ambalo halieleweki. Hakuna bei ya hizo tisheti. Hakuna mchakato wa mapato yatakayowafikia wahanga na habari nyingine muhimu. Yaani ni kama vile limeandikwa na mtoto. Yaani kupata taarifa muhimu watu inabidi waje PM? Watanzania wa sasa ni lazima wahoji mambo haya ili wawe na uhakika. Sasa wewe badala yake umeanza kutoa povu. Yaani unataka tu wafakamie hizo tisheti hata bila kujua mchakato wenyewe ukoje? Kuna ugumu gani wa kuweka tangazo linalojitosheleza hapa hapa laivu badala ya private message? Something is wrong somewhere!
Huwa wapo kimaslainapenda kujua mchango wa clouds media kwenye haya maafa maana naona wamegoma kabisa kusitisha fiesta yao
Iyo hafla itafanyika wapi? na kuwepo na physical evidence kwamba kinachopatikana kitaenda kwa wahanga na co kufa kufaana.Nawe pia waweza shiriki sbbu enzi za kusubiri wafadhiri katika maafa zimepita kumbuka inaanza na wewe wengine wanafuatia. Pia unakaribishwa katika kampeni hiyo.
Si ungeweka maelezo yote yanayojitosheleza hapo mtu anasoma anaelewa. Sema wazi hizo hela za tisheti zinakwenda wapi na zitatumikaje. Mbona huwa ni vigumu sana kwa sisi Wabongo kuweka tangazo linalojitosheleza? Ujanja ujanja tu kila kona.
Mimi siwezi kushiriki kwenye hilo tamasha bila kujua kama mchango wangu kweli utawafikia wahanga au utaishia mikononi mwa wajanja akina Getrusa. Kuna njia nyingi nyingine za kufikisha mchango wangu huko na hii yako SIYO!
Yani sijaelewa hii nonsense kabisa. Yametokea maafa ya maana sembuse hao wahaya 15 waliokufaCity boy ziliua watu zaidi ya 28 lakini hapakua na kampeni, ajali ya train dodoma iliua zaidi ya watu 100 hapakua na kampeni, kivuko cha kilosa , mv spice islander, mv bukoba, kote hakuna kampeni......
Tetemeko limeua 16 kampeni kila kona, vikumbo kibao, nyimbo zimetungwa, fund raising kibao mpaka hazina wanafanya fund raising......mnajua kwa nini...?????
Embu fanya yako kwanza mkuu..Hujui kichwani kwangu nawaza nini!!Duhh,nchi hii wote tukiwa na mawazo kama yako na fikra kama zako itakuwaje fikir inaanza na wewe! Kama wewe unawaza hayo...