24K together for Kagera

24K together for Kagera

Fursa watu wamekamata fasta!!!
Hii yote ni kutokana na ukimya wa bigdady.
 
napenda kujua mchango wa clouds media kwenye haya maafa maana naona wamegoma kabisa kusitisha fiesta yao
Tunashukuru kwa ushauri na ushirikiano wanaotupa! Shukrani za kipekee kwa Ruge.
Lakini pia clouds wamekuwa na mtoa taarifa wao mubashara toka bkb.na nimeona 360wakilizungumzia...mengineyo sijui sbbu mimi sio msemaji wao..
Kuhusu fiesta nadhani isingekuwa rahisi kuahirisha.
 
Niliona mahali...MAJANGA NAYO SIKU HIZI YAMEKUWA FURSA.....mmh wacha watu wajipigie pesa
 
Fursa watu wamekamata fasta!!!
Hii yote ni kutokana na ukimya wa bigdady.
Jifinze kuangalia upande wa pili wa fikra zako (private msg) maana yake upewe maelezo ya kina usiporidhika unaacha. Usiwaze kuibiwa tu kila mara kumbuka aliwazalo mjinga ndilo limtokealo.
 
Kama hii issue yako unafanya na huyo tapeli Ruge basi hapa kuna harufu ya kuibiwa.
 
Niliona mahali...MAJANGA NAYO SIKU HIZI YAMEKUWA FURSA.....mmh wacha watu wajipigie pesa
Duhh,nchi hii wote tukiwa na mawazo kama yako na fikra kama zako itakuwaje fikir inaanza na wewe! Kama wewe unawaza hayo...
 
Toeni mchanganuo je wahanga watanufaika VP
 
Ila kwa majigambo huwezi amini kuwa pale ni wanapotoka kina Milioni Kumi ya Mboga
 
Jifinze kuangalia upande wa pili wa fikra zako (private msg) maana yake upewe maelezo ya kina usiporidhika unaacha. Usiwaze kuibiwa tu kila mara kumbuka aliwazalo mjinga ndilo limtokealo.
Usiwe mkali, hii ni fursa na ukimya wa bigdady umechangia kondoo kujichunga wenyewe.

Naumizwa na ukimya huu hata kutufikisha mahala tunabuni mbinu za kujiokoa wenyewe.

Tungeweza kuchanga fedha tasilimu badala ya kununua T-shirt ambazo indirect unakuwa umegharimia uchapishaji wake ambao kimsingi utamnufaisha mchapaji (kiwanda) na msambazaji ndipo salio liende kwa mlengwa.

Usiushambulie uwezo wangu wa kufikiri kwa maana unajivua nguo mwenyewe.
 
Fursa watu wamekamata fasta!!!
Hii yote ni kutokana na ukimya wa bigdady.
Serikali zinazojitambua duniani hili tatizo wangekuwa washali-handle saahizi wanapanga kuwajengea makazi yao hao waathirika na usingekuta ujinga huu kwamba watokee watu waprint t-shirts ziuzwe ndo wahanga wasaidiwe.
 
Ahsante.
 
Duhh,nchi hii wote tukiwa na mawazo kama yako na fikra kama zako itakuwaje fikir inaanza na wewe! Kama wewe unawaza hayo...
Sio inaanza na wewe ikianza na wewe ni kwamba unatoa kwa huruma tu isizoeleke kwamba tatizo likitokea basi waziri fulani au sijui mkuu wa mkoa aanze kuhimiza watu wachange kusaidia,serikali ndiyo ya kwanza kuwahudumia watu walioichagua na nchi hii watu tunalipa kodi,twakatwa pesa kibao maendeleo sio kujenga barabara tu hata kuwajibika ktk majanga nako ni maendeleo,kama pesa hakuna wapunguze allowances waazolipana bungeni na vikao vya kawaida ili kuwe na fungu maalum la maafa raia wenyewe tuna hali mbaya.
 
Duhh,nchi hii wote tukiwa na mawazo kama yako na fikra kama zako itakuwaje fikir inaanza na wewe! Kama wewe unawaza hayo...
Kama unataka kujitangaza kuwa umewasaidia wana bukoba NUNUA T-shirt, otherwise serikali haihitaji michango yenu nyinyi masikini, yenyewe inauswahiba na matajiri, ujue na hawa matajiri ndio waliambiwa hawakuchangia chochote kwenye kampeni za uchaguzi na inaonekana ni kweli maana ingekuwa uongo walipoalikwa kuchangia waathirika wa tetemeko la kagera wasingeenda!!!!
 
Ok,! Basi sawa.
 
Jifinze kuangalia upande wa pili wa fikra zako (private msg) maana yake upewe maelezo ya kina usiporidhika unaacha. Usiwaze kuibiwa tu kila mara kumbuka aliwazalo mjinga ndilo limtokealo.
Usilaumu watu hapa. Wewe umeweka meseji/tangazo ambalo halieleweki. Hakuna bei ya hizo tisheti. Hakuna mchakato wa mapato yatakayowafikia wahanga na habari nyingine muhimu. Yaani ni kama vile limeandikwa na mtoto. Yaani kupata taarifa muhimu watu inabidi waje PM? Watanzania wa sasa ni lazima wahoji mambo haya ili wawe na uhakika. Sasa wewe badala yake umeanza kutoa povu. Yaani unataka tu wafakamie hizo tisheti hata bila kujua mchakato wenyewe ukoje? Kuna ugumu gani wa kuweka tangazo linalojitosheleza hapa hapa laivu badala ya private message? Something is wrong somewhere!
 
....nonsense!..pesa za kugharamia hayo maronyaronya si mngezipeleka moja kwa moja kwa wahanga?
..msitukere mjue.,watu tuna machungu yetu blalfuu!
 
Back
Top Bottom