2026 FIFA World Cup - Special Thread

Hii mechi imeshangaza wengi aisee ..Spain wamewasoma vizuri sana Ufaransa..

Hawa wajukuu wa Charles wakitinga fainali baada ya miaka 60 watakamia mno ...
Angalau hata Argentina anaweza isumbua Spain wenda hata kuifunga ila kwa timu za ulaya ni Ureno tu ndio huwa naona Spain huwa anapata tabu sana kutoka na matokeo mazuri hua hata anafungwa au anashinda ushindi mwembamba sana ila hawa wakina Ufaransa ,Spain sasa hivi hii ni match ya tatu mfululizo anajipigia tu Ufaransa.

Hiyo England itakuwa match ya pili mfululizo yeye kufungwa na Spain labda Argentina anishangaze kumfunga Uingereza kitu ambacho ni kigumu japo kinawezekana.
 
Mimi bado nawashangaa hivi kwanini mlikuwa mna mchukulia poa Spain..? Spain ile pale ina mtu mmoja tu ambae hayupo serious (Lamine) wengine wote ni watu wa kazi na mpira wanaujua.
Shikeni maneno yangu, mtaiona Fainali nzuri tamu ya kitaalam na mpira utatembea sana, na hii fainali ni LAZIMA iwe Argentina vs Spain.
Hao waingereza ni kama Taifa Stars, nyie endeleeni kuwaamini watawatia aibu kama ureno na kizee chao walivyo watia aibu...
Argentina anabeba 🏆 back to back
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…