Ila wee jamaa bhana uko primitive Sana 😁😁😄
Mnalalamika kuwa Messi ana bebwa mean while mchezaji wenu kwenye tournament kaishia kufunga magoli 3
Mnalalamika kuwa Argentina ana bebwa mean while wachambuzi wakubwa wote duniani wamepitia match review na hakuna sehemu iliyo onyesha kuwa Argentina kabebwa Salah alijiangusha before haja jiangusha beki alitangulia kuucheza mpira ,
And goal la misri lilikataliwa it was clear faulo , so hizo lawama mnazitoa wapi !? Kama mnaona wivu kisa mabao ya Messi siumwambie Goat wenu nayeye aibebe team afunge mabao mengi mtu unafunga magoli 3 halafu una depends team ipate mafanikio are you kidding me!? 😁😁😁
Kama mnaionea Argentina wivu Kwa kuchukua WC 2022 Siumwambie GOAT wenu aifikishe team yake ya Portugal walau nusu final tuone
Okay tufanye Messi na Argentina wanabebwa so Fifa ndio waliowatuma Portugal wafungwe na Morocco kwenye lats WC tournament!?
And fifa ndio walio Watumwa mfungwe na Spain in this WC tournament!? Kwanini hamtaki kukubali kuwa uwezo hamna !? 😄😄😁😁
Au Kuna siku Portugal mlifunga magoli ambayo yange wavusha kwenda nusu final halafu fifa / refer wakayakataa !??
Litimu lenu libovi mnashindwa or kuliborsha kazi kukaa nakuanza kulalamika , you guys are insane for sure
Ukweli ni kwamba simkubali Messi na Argentina.
Hii haijawahi kuwa siri nililiweka wazi from the scratch hadi tuliokuwa nao kwenye uzi wa World Cup ya 2022 wanajua hili.
Hoja ni kwamba, je ukweli wa hoja zangu unaupima kwa kuangalia uhalisia na ushahidi nilioweka au unaupima kwa kuangalia mapenzi yangu kwa Messi?
Labda nikupe mfano mmoja.
Baada ya Messi kukosa penalty kwenye mechi ya juzi, kuna mashabiki wa Argentina na Messi humu walisema "Messi hamna kitu"
Lakini kitu kama hiki hiki nikikisema mimi kinatafsiriwa tofauti kwasababu nafahamika kuwa simkubali.
Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba mimi naweza kujitetea kwa evidence, wewe utajitetea kwa hisia za ushabiki.
Na kama nilivyosema awali, naongea haya yote sio kwa lengo la kukufanya wewe na wengine mkubaliane na mimi.
Mimi naongea na kuambatanisha evidence kwa kuweka rekodi sawa just in case huu uzi unaweza kuja kutumiwa na wadau kama reference au watu wengine ambao wangetaka kusikia stori kutoka pande zote.
Nyinyi tayari mmeongea kuhusu positive za Argentina na Messi, na mimi nitaongea ule upande ambo nyinyi hamjaongea.
Audience itachagua iende na habari gani ndio maana najitahidi kuweka ushahidi.
Umesema Salah alijiangusha. Wacha nikubaliane na wewe kwenye hili, lakini kwanza unaelewa kihezo kilichotumika kukataa goli la pili la Egypt?
VAR baada ya kufanya review goli lilikataliwa kwasababu kwenye build up mchezaji wa Egypt Marwan Attia, alimkanyaga Lisandro Martinez. VAR ilionesha mgusano kati ya mguu wa Marwan Attia na Martinez
Lakini tukio la Mo Salah pia ni incident hii hii ambapo Julian Alvarez alimkanyaga Mo Salah ndani ya box dakika ya 92 na kuanguka na hata video ukiangalia inaonesha Mo Salah akikanyagwa.
Video hii hapa chini
Mpaka hapo sidhani kama kuna utata kuwa Alvarez hakumkanyaga Mo Salah, wote tunaona. Hoja inabaki kuwa kwanini tukio hili halikupewa attention ya kuangaliwa kwenye VAR ilihali tunaona mtu akikanyagwa?
Umedai wachambuzi wengi wakubwa wamekubaliana kuwa Egypt haikuonewa. Umesema wengi ila hujataja kwa majina na kusema ni wangapi.
So namimi nikikuonesha evidence ya kuonesha wachambuzi na ma legend wa mpira wakikubali kuwa Egypt amedhulumiwa, utasemaje? Utawaita hater?
Hawa wote walisema Egypt imenyongwa na mwamuzi.
Rob Green, Gary Neville, Garry Kasparov, Rob Green, Alan Shearer, Ian Wright, Jamie Carragher na Jose Mourinho.
Na hawa hapa chini ndio waliosema yalikuwa ni maamuzi fair
Pierluigi Collina: (Huyu ni mkuu wa waamuzi wa FIFA), Dr. Joe Machnik na Nikhil Naz
Zlatan na Henry hawakuzungumzia kabisa kuhusu controversial ya matukio na maamuzi yaliyoamuliwa.