2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

Mechi ya kwanza ya mpira kuumia maumivu makali ni Man U Vs Barca 2010 kama 11 kama sikosei enzi hizo nipo shule ya msingi , napenda Man U kuliko kitu chochote Duniani siku hiyo nilipata tabu sana na ukawa mwanzo wa kumchukia Messi.

Yanga na Mamelodi sikuamini eti mtu mzima nishindwe kulala kisa maumivu ya mpira dah! maumivu yalidumu kama wiki mbili mpaka nikasahau , tokea siku hiyo mpaka leo kama nimeacha hata kuangalia mechi za Yanga . Mpaka Leo haijalishi Yanga anacheza mechi gani hauwezi kunikuta natoa hela yangu kwenda Banda umiza kucheki na kuifuatilia kama zamani .

Sasa maumivu ya mpira sina kabisa baada ya depression nilipunguza kama sio kuacha kabisa ushabiki , sasa nacheki mechi moja Moja tu au michuano muhimu kama burudani tu na sio kama shabiki kindakindaki wa kuumia kama zamani
Ndio mpira ulivyo mkuu, Leo unakumiza kesha unakupa furaha. Sema mie ninacho mshukuru MUNGU ni kutojiingiza kwenye masuala ya kubeti.
 
Lao moja hao

FB_IMG_1783449360861.jpg
 
Mkuu pole.
Out of Point 2010 ulikuwa bado shule ya msingi?
Inamaana unapishana kidogo umri na first born wangu 😃😃
Ndio mkuu nipo darasa la 3 kipindi hiko . Kombe la Dunia 2010 nilikuwa Brazil shabiki mkubwa namba 9 wao Luis Fabiano mechi ya ufunguzi na Ivory coast alipiga kamba mbili tukaja kutolewa na Netherlands huo ndio ukawa mwanzo wa kuichukia Netherlands mpaka Leo na nilifurahi sana Spain walipotwaa ndoo
 
Back
Top Bottom