UPDATE: Senegal 4 - 0 Iraq (Kipindi cha Pili Dakika 77)
Senegal wanaendelea kuisulubu Iraq katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi I kwenye Kombe la Dunia 2026 unaopigwa sasa hivi huko Toronto, Canada.
Matukio makubwa ya mechi hadi sasa:
Dakika ya 4: Habib Diarra anaipatia Senegal goli la kwanza akimalizia pasi ya Abdoulaye Seck.
Dakika ya 13: Beki wa Iraq, Rebin Sulaka, anapewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya VAR kubaini amemzuia mchezaji wa Senegal aliyekuwa anenda kufunga. Iraq wako 10 uwanjani.
Dakika ya 56: Ismaïla Sarr anapachika goli la pili kwa Senegal baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Lamine Camara.
Dakika ya 59: Pape Gueye anapiga msumari wa tatu kwa Senegal sekunde chache tu baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi kuchukua nafasi ya Diarra.
Dakika ya 71 Mchezaji wa akiba Pape Gueye alifunga goli la nne baada ya kuuwahi mpira uliookolewa vibaya na mabeki wa Iraq na kupiga shuti kali na la nguvu la mbali lililokwenda moja kwa moja wavuni, kipa wa Iraq akiwa hana la kufanya.
Kipa wa kwanza wa Iraq, Ahmed Basil, aliumia na kufanyiwa mabadiliko wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Jalal Hassan. Senegal sasa wanajisogeza vizuri kwenye nafasi ya kuwa miongoni mwa washindi watatu bora ili kufuzu hatua ya mtoano (Round of 32).