2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

Hawezi kumfunga muingereza labda ajitahidi kwa croatia 🇭🇷 game ya kwanza alipowahi kukutana na england ghana iliweza kuondoka na point moja pekee na kumbuka ile ndo ilikua ghana sasa sio ya sasa
Unajua watu hatujaiona sana Ghana ndio maana tunapoteza nao imani.
Au kwasababu kina Kudus hawakutia juhudi kwenye qualification za AFCON?
 
2026 World Cup Groups​

Utabiri Wangu.

Group A: Mexico, South Korea, South Africa, Czechia

Hapa Nafasi natoa Kwa Mexico na Korea Kusini...
Japo South Africa wanaweza kufanya muujiza.

Group B: Canada, Switzerland, Qatar, Bosnia and Herzegovina
Hapa Canada ana faida ya uenyeji, watasonga mbele na Uswisi.

Group C: Brazil, Morocco, Haiti, Scotland.
Hapa nafasi iko wazi kwa Brazil na Morocco, labda Scotland waingie kama best looser.

Group D: United States, Paraguay, Australia, Türkiye
Kundi gumu kidogo, Faida iko kwa Marekani na Uturuki Watasonga mbele.

Group E: Germany, Ecuador, Ivory Coast, Curacao.
Hapa nawapa nafasi Wajerumani na Ivory Coast, Kina Caicedo wanaweza kuingia kupitia nafasi ya mpotezaji bora(best looser)

Group F: Netherlands, Japan, Sweden, Tunisia
Nawapa nafasi Uholanzi na Wajapan kusonga mbele.

Group G: Belgium, Iran, Egypt, New Zealand
Belgium na Misri, njia nyeupe kabisa.

Group H: Spain, Uruguay, Saudi Arabia, Cape Verde.
Nafasi iko wazi kwa Uhispania na Uruguay.

Group I: France, Senegal, Norway, Iraq
Kwangu hili ndilo kundi gumu zaidi kwenye haya mashindano.
Big chance natoa kwa Ufaransa na Senegal kusonga mbele...

Group J: Argentina, Algeria, Austria, Jordan
Argentina na Algeria njia nyeupe...
Japo Austria wananafasi finyu kidogo.

Group K: Portugal, Colombia, Uzbekistan, DR Congo
Mungu ibariki DR Congo, nawapa nafasi wao na Ureno kusonga mbele.

Group L: England, Croatia, Ghana, Panama.
Hapa England na Croatia, njia nyeupe huyu Ghana apitie kwa wapotezajibora...

Nitarudi hapa kutetea nilichoandika baada ya michuano ya Makundi kukamilika.
cc; uran Palac Mtaachana raraa reree Smart911 kiwatengu Waufukweni kalendi Imeloa na wanamichezo wengine wote.

Baada ya hapo nitaleta utabiri wangu kwenye 16 bora
 
Unamtazama na Jordan sema na ndugu yetu Congo ana hali ngumu labda ajitahidi kwa uzbekistan lakini bado shuguli ni pevu
DR Congo ana maingizo mapya mazuri...
Anakikosi bora kuliko Colombia na hao Uzbekistan.
Wissa Alikuwa na msimu mzuri sana pale New Castle, Bakambu pia akiwa kwenye form atafanya kitu.

Mwanetu Wan-Bissaka atasimamia Ulinzi....
Wanaye pia Noah Sadiki alipata sana nafasi na Sunderland ni Middle ya ball.
Wakimpa Mayele nafasi lazima atupie walau kimoja.
 
Narudia tena ili ni kombe la dunia kuna watu wanataka mbali na kuchukua kombe basi ata mfungaji bora ila uhalisia Congo akijikita kufunguka mbele ya Colombia anakula nyingi kwa meno ndo asijaribu kabisa mpe nafasi ya best looser
 
Sasa weka hii kwenye kumbukumbu zako, game yake ya kwanza na Ureno tarehe 17 Juni hatafungwa.
 
Back
Top Bottom