2025 na mbeleni

Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Uteuzi wa Dr Bashiru unafuatia kifo cha Balozi Kijazi. Binafsi sioni maandalizi ya kubadili katiba. Laiti Balozi Kijazi (RIP) angefutwa kazi kisha nafasi ikajazwa na Dr Bashiru kidogo ningeungana na kwaya inayoimba mapambio ya maandalizi ya kufuta ukomo wa miaka 10.
 
Naona njaa imekupanda kichwani hasa mara baada ya biashara ya kubeba mabox kuota mbawa.

Hata kama wewe ni ngosha hupati uteuzi ng'ooo
 
Naona njaa imekupanda kichwani hasa mara baada ya biashara ya kubeba mabox kuota mbawa.

Hata kama wewe ni ngosha hupati uteuzi ng'ooo
We jamaa dizaini una njaa sana hadi unaishia kui project kwa wengine.

Nani kakuambia mimi nataka uteuzi?

Na sijui uteuzi wa nini/ wapi?

Nyumbu bana...
 
Reaction ya Watanzania baada ya uchaguzi ilitosha tu kukujuza kuwa CCM ni chama cha namna gani. Watanzania hawakuwa na si wajinga kama unavyoamini wewe.

Ndo maana haya maneno ya kuibiwa kura, sijui katiba mbovu, mara sijui tuma.....yatabaki kuwa yenu hapa jf. Mwananchi wa pale Mziha anaihitaji umeme, akiupata kupitia CCM si mpaka nirudi shule kujifunza uimara wa CCM.
Mkulima wa pale NgareNairobi Sanya Juu akiiona ile lami inayokwenda kuiunganisha Siha na Longido.....Siha na Hai.....anaiona CCM,so hapo hata kama nchi ingekuwa haina katiba kwake sawa tu.

Mtu wa pale Moshi mjini akiiangalia hospitali ya Mawenzi pale mambo yanavyopamba moto hatajuwa kuwa upinzani uliibiwa kura.....anajuwa CCM ipo kazini. So siku mkiitambua CCM kama chama kikubwa,na wananchi watawaheshimu kama wapinzani wa CCM.
 
Maneno ya paragraph ya mwisho kabla ya ni hayo tu, ni rushwa - unajaribu kumpa rushwa Mh. Rais!
Pia unashangaa nani ataweza kuinua mdomo kusema! Je! Si mnaye mtetezi wenu Amsterdam?
 
Hata kama anafikiria kuongoza muda anajidanganya wachawi tupo tutaunganisha nguvu atakufa [emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hukuelewa kauli hiyo! Alimaanisha, baada ya kuwa katibu mkuu, hata taka uteuzi mwingine wa kuongezewa hapo (kwa kingereza - concurrently). Ukikumbuka, baada ya hapo watu wengi walinyang'anywa vyeo vingine wakabaki na kimoja!
 
Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Ni wapuuzi tu ndiyo wanaozusha. Mwenyewe ukimuona JPM amechoka na angependa 2025 ifike kesho akabidhi kijiti ila michadema, mungu anaiona
 
Kapewa nafasi ile ile ya ukatibu...
 
Term limits zimeanza wakati wa Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Kwa kumbukumbu zangu hata Mzee Mwinyi alikuwa anabembelezwa aendelee kukaa madarakani.

Wakati wa Mkapa sikusikia sana hii habari ya kumbembeleza aongeze muda.

Labda ni kwasababu Salmin Amour alijaribu kule Znz lakini akakataliwa na chama chake.

Awamu ya JK nayo kulikuwa na wana-CCM waliomtaka aongeze kukaa madarakani lakini hakufanya hivyo.

Kishawishi cha kuongeza muda ni suala ambalo watangulizi wa Magufuli walikipitia lakini walikishinda.

Katika awamu hii mahali pa kuwa makini napo ni BUNGENI. Je, bunge hili la CCM watupu halitabadili katiba?

Baada ya hapo itabidi tumuangalie Magufuli, lakini hatuwezi kujua nini atafanya kwasababu uchaguzi mwingine ni 2025.

Mwisho, miaka yote kumekuwa na kambi mbili; inayotaka Rais aongeze muda, na inayopinga muda wa Urais usiongezwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…