2020 twende na Membe ama January Makamba?

2020 twende na Membe ama January Makamba?

Alokwambia CDM wanamtaka Membe ni nani??? Wanaomtaka BM ni wa hukohuko kwenu...... Yaan mchama wenu umeshaparanganyika paranganyika.....

CDM tupo kimya....... Tunasubiri mtifuane sisi tuje tuokote nchi kilaini.
Hahahaa......... Chadema mtamuumiza Lowassa kwa pressure!
 
Hivi mkuu tokea awamu hii ianze ushawahi sikia huyu mama akiropoka ama kutoa maneno ya shombo,mama wa watu mstaarabu sana,hana ng'wang'walu kabisa.
Ameshindwa kumsaidia magu kwa hiyo pamoja na ustaarabu wake asepe naye tu!
 
Our future president and prime minister.
Mshazoea kuiba mpaka mil 10 mnaita ela ya mboga sasa mmebinywa korodani mnaanza kulia. Akitoka JPM tunaweka makinda au musiba. Mnatafuta mtu calibre ya JK ili muendelee kuiba
 
Ni kweli watu walitaka mtu kama mh JPM, kwa Mimi ninachoona kwa sasa tunahitaji muhimili na mifumo yenye nguvu then watu wente nguvu baadae, alichokosea huyu bwana ni kuvunja sheria na haki za watu, akiongozwa na hisia badala ya hali halisi
Huyu mkali alafu mshamba
 
Nafahamu alijiunga baada ya kumnyima kijiti kugombea urais kwa tiketi ya ccm na kumuweka katika kundi la wasio na nidhamu.

Membe amejiunga lini???
Mkuu ruhusu ubongo wako uwe huru acha Kuwa mtumwa wa fikra
Wewe unajua Sumaye alijiunga lini Chadema?!
 
Mod Anthony Mod One Moderator Maxence Melo mnatukosea kuchanganya uzi wetu na nyuzi zingine, mna zi merge hizi uzi za BERNARD MEMBE na JANUARY MAKAMBA mturudishie zilipokuwepo tafadhali vinginevyo tutaacha ku post uzi humu msizichanganye tafadhali tunaomba acheni ziwe wazi zisomeke na title zake zinajieleza kivingine tafadhali kama mnatujali rudisheni msizichangaye ila kama mnaona mtuvuruge zisisomeke zenyewe kama zilivyo sawa tutaacha ku post. cc: Sky Eclat
 
Watanzania watu wa ajabu sana, kutoka kutaka rais dikteta mpaka rais mjanja kisa? Hamueleweki, kikwete alikuwa dhaifu, magufuli mshamba sasa mnataka mjanja, duh!
 
Kanungila Karim,

  • Nitalalaje wakati nchi iko njia panda?. Furaha gani niliyokuwa nayo mimi mpaka nilale usingizi mnono!
  • Mfukoni chapaa hakuna, kuna watu wamepotea mpaka sasa hawajulikani wlipo, mishahara wafanyakazi hawaongezwi kwa mujibu wa sheria, trilioni 1.5 zimeyeyuka, tuna hela za kurudia chaguzi za kuunga mkono juhudi lakini hatuna hela za katiba ya wananchi.
  • Nitalalaje wakati tunaambiwa imeundwa mahakama ya mafisadi lakini waliotajwa kwenye ripoti ya makinikia bado wapo mtaani wanadunda.
  • Nitalalaje wakati wote waliotajwa kwenye listi ya madawa ya kulevya hakuna hata mmoja aliyeko jela?
  • Hebu niambie utalalaje wakati kuna wananchi wanavunjiwa nyumba halafu wengine wanaambiwa wasivunjiwe kwa sababu walimpa mtu kura.
  • Niambie wewe mwenyewe, ulale, usingizi utoke wapi wakati kiongozi anayepaswa kuheshimu sheria anaagiza mzigo kutoka nje ya nchi , mzigo unafika bandarini halafu anataka kukwepa kodi na bado anaachwa ofisini aendelee na kazi ya kuhimiza watu walipe kodi!
  • hebu ndugu yangu tusemezane, utalala usingizi utatoka wapi wakati kuna watu wamefukuzwa kazi kwa vyeti feki lakini mwingine anaambiwa achape kazi tu maadamu anajua kusoma na kuandika
  • Nitalalaje kwa mfano ili iweje wakati ndoto ya nchi yangu kupata Trilion 425 sawasawa na Noah Moja kwa kila mtu imepotea
  • Sijui wewe mwenzangu, Lakini mimi nimeshindwa kulala kwa sababu serikali hii imekataa kutekeleza ilani ya chama, imekataa kutoa milion 50 kila kijiji, imekataa watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo, imekataa kukamilisha mchakato wa katiba kinyume cha ilani. Katika mazingira kama hayo nitalalaje mimi?
  • Nitalalaje wakati Trafiki wanaambiwa buku tano ni hela zakung'arisha viatu, naumiza kichwa nitazipata wapi buku tano za kumpa afande ang'arishe viatu
  • Nitalalaje wakati Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano yupo nje anatibiwa kwa pesa za hisani ya serikali nyingine wakati serikali yake yenyewe imekataa kumpa hata senti tano. nitalalaje mimi kwa mfano!
  • Nitalalaje kwa mfano, kwa raha gani wakati siasa za kistaarabu hazipo, yaani ni ubabe ubabe, undava undava, viongozi wakuu takriban zaidi ya asilimia 90 ya viongozi wa vyama vya siasa vilivyopo kwa mujibu wa sheria wana kesi mahakamani
  • Nitalalaje ndugu yangu, Nanyimwa kuwaona Laivu wawakilishi wangu bungeni, lakini naonyeshwa kila mara, kila wakati mtu mmoja
Katika Mazingira kama haya, ndiyo maana nimeamka na kusema twende na Membe tu 2020 haya mambo hayatakuwepo!
Umeongea mambo mazito ila swali langu ni je CCM wameshawahi kumsimamisha mgombea mwingine kabla ya rais aliyetoka kwenye chama chao hajamaliza mihula miwili?
 
Watanzania watu wa ajabu sana, kutoka kutaka rais dikteta mpaka rais mjanja kisa? Hamueleweki, kikwete alikuwa dhaifu, magufuli mshamba sasa mnataka mjanja, duh!
Wa Tanzania hatutaki rais anaewaonea wafanyakazi, mwizi wa mafao ya wastaafu, kaua uchumi ,biashara, wananchi maisha magumu, mwenye kuonea wapinzani,kununua wabunge, hataki kukosolewa na maupuuzi mengine kibao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom