Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,103
34,062
Habarini Wadau,

Ninaomba kuuliza lakini pia kupatiwa msaada katika jambo hili.

Mwaka Jana mwezi wa 5, watumishi wengi wenye sifa walipandishwa madaraja. Lakini cha kushangaza katika mabadiliko ya mishahara ni kama kuna ubaguzi kwa watumishi.

Kwa Mkoa wa Kilimanjaro kuna ambao wamebadilishiwa mishahara na wengine wenye barua kabisa za kupanda daraja mishahara yao haijabadilika.

Mimi nina miaka 7 tangu kuajiriwa, huu ni wa 8. Nilipoajiriwa baada ya miaka miwili nikapata ruhusa rasmi ya kwenda masomoni, nikarudi kazini tangu 2017 na kufanya kazi kwa miaka miwili na huu wa 2020 ni wa tatu.

Nimepata barua ya kupandishwa daraja mwaka jana lakini leo Afisa Utumishi wilaya ananiambia kuwa sina sifa ya kubadilishiwa mshahara hata kama barua imekuja.

SABABU: Afisa Utumishi anasema kuwa kuna Mwongozo umekuja ambao hautambui ule muda wa mtumishi kuwa masomoni kuwa upo ndani ya Utumishi hata kama alienda kwa barua rasmi bila kutoroka.

SWALI: NI KWELI HUO MWONGOZO UPO? JE, NI RASMI ?

Au upo kwa Mkoa wa Kilimanjaro tu?

Naombeni Msaada wenu.

=======
Soma pia:

1) Je, watumishi wa umma watarajie nyongeza ya mishahara 2019/2020? - JamiiForums

2) Serikali: Mishahara minono yaja kwa watumishi wa umma - JamiiForums

3) Mwaka wa 4 watumishi wa umma bila nyongeza ya mshahara - JamiiForums

4) Kama Serikali itashindwa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma 2020 vyama vya wafanyakazi vifutwe - JamiiForums

5) Maadhimisho ya Siku ya Sheria: Rais Magufuli adai hata yeye mshahara haumtoshi, awaasa wapelelezi kuharakisha upelelezi - JamiiForums

6) Mei Mosi 2019: MEI MOSI 2019: Rais Magufuli asisitiza kuwa ataongeza mishahara akikaribia kuondoka madarakani. Awataka wafanyakazi kuwa na subira - JamiiForums
 
Waliopanda mwaka huu walikasimiwa kwenye budget kama sikosei ya mwaka 2018, wewe ulikuwa na mwaka mmoja tangu kutoka kazini. Utahtajika kufanya kwa miaka 3. Hivyo mwakani waweza panda daraja

Hata annual increment ukiwa masomoni hutakiwi kupata
Ahsante kwa Msaada, Sasa kufidia ni kwa miaka mingapi baada ya kutoka masomoni? Tangu 2017 mpaka leo bado sijatimiza vigezo?

Na huo Mwongozo unapatikana wapi Mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Dumelang
 
Waliopanda mwaka huu walikasimiwa kwenye budget kama sikosei ya mwaka 2018, wewe ulikuwa na mwaka mmoja tangu kutoka kazini. Utahtajika kufanya kwa miaka 3. Hivyo mwakani waweza panda daraja

Hata annual increment ukiwa masomoni hutakiwi kupata

Dumelang
Mwaka huu unamaanisha???
 
Ahsante kwa Msaada, Sasa kufidia ni kwa miaka mingapi baada ya kutoka masomoni? Tangu 2017 mpaka leo bado sijatimiza vigezo?

Na huo Mwongozo unapatikana wapi Mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali lako lilikaa kiuchochezi na ubaguzi wa ki jiografia sana.
Umejibiwa kwa hekima.
Kama hujui kitu uliza direct sio unatengeneza chuki ktk swali.
Umesoma lkn nadhani umefaulu mitihani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali lako lilikaa kiuchochezi na ubaguzi wa ki jiografia sana.
Umejibiwa kwa hekima.
Kama hujui kitu uliza direct sio unatengeneza chuki ktk swali.
Umesoma lkn nadhani umefaulu mitihani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nimeandika hivyo kwasababu hujajua majibu ninayopatiwa na huyu Mtumishi na ni kwa muda mrefu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom