Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 11,719
- 8,625
Pascal Mayalla mwalimu mzuri huamini hoja nzuri ni ile yenye mifano kuntu.Wanabodi Salaam.
Wakati tukifunga mwaka 2016 na kujiandaa kuupokea mwaka 2017, sisi wana JF individually au collectively inatubidi tujitathimini kama hizi kelele tunazopiga humu kupigia kelele mambo mengi yanayoendeshwa ndivyo sivyo, zinasaidia?.
Tujiulize tumepigia kelele mangapi na jee kumesaidia kuleta mabadiliko? .
Kwa upande wangu nakiri hizi kelele zimesaidia sana. Japo wapigiwa kelele wanajifanya kuweka pamba masikioni kujifariji kuwa hawasikii na kuvaa miwani ya zege kuwa hawaoni, ukweli ni kuwa, sio tuu wanasikia sana, na wanaona sana, bali pia wanabadilika, changing for the better.
Hivyo natoa wito kwa wana JF ambao ni bold enough, kwa mwaka 2017, tusiendelee tuu kuwa just a Barking dogs who seldom bite, besides barking only, let's start to bite little by little by taking simple actions towards bringing about radical changes for the better kwa mambo tunayoyapigia kelele.
Tukiona kuna jambo ambalo linakwenda ndivyo sivyo, tusiishie kulipigia tuu kelele bali pia tupendekeze hatua za kuchukua kuibadili hiyo hali na naamini serikali yetu sikivu itatekeleza na isipotekeleza, tutafanya actions kuifanya itekeleze, yaani isipotekeleza, itekelezeshwe kwa jinsi ile ile ilivyochaguliwa kwa kura zisipotosha, zinatosheshwa na kama ni ujazo ukijaza usipojaa unajazilizia, hivyo kwa mwaka 2017, tupunguze maneno maneno kwa kusema sema sana, maneno mengi, kelele nyingi lakini vitendo sifuri.
Tuwe watu wa maneno mafupi na vitendo virefu. Tupunguze maneno, tuongeze vitendo kuisaidia Tanzania yetu ibadilike kwa ku change for the better! .
Nakiri kuwa inspired kupandisha bandiko hili katokana na hoja ya mwana JF huyu
Maneno matupu hayavunji mfupa, watu mnakuja na kauli zenye maneno makali kama hizi kauli za "hatukubali kuona katiba ikivunjwa" as if katiba ikivunjwa kuna kitu mna uwezo wa kufanya!, wakati kiukweli katiba kila siku inavunjwa bila kufanywa lolote kwa sababu hamna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubweka tuu!.
Kwa kunisaidia mimi na wengine, usiishie kusema hatutakubali kuona katiba yetu ikivunjwa, bali twende a step further kwa kusema, utafanya nini au unaweza kufanya nini endapo katiba yetu itavunjwa tena, ili kupunguza mabandiko ya maneno matupu, vinginevyo na bandiko hili ni muendelezo wa mabandiko mengi ambayo mimi nayaita mabandiko ya
" a barking dog seldom bite!".
Kwa mwaka 2017, wana jf tupunguze kubweka tuu, ikibidi kung'ata pia tung'ate.
Bye Bye Mwaka 2016, Karibu 2017.
Paskali
Ebu tupe mfano, unaposema watu wasilalamike tu. Wachukue hatua, tupe mfano.