2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite", Tusiishie Kubweka Tu, Tung'ate!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,556
2,000
Wanabodi Salaam.

Wakati tukifunga mwaka 2016 na kujiandaa kuupokea mwaka 2017, sisi wana JF individually au collectively inatubidi tujitathimini kama hizi kelele tunazopiga humu kupigia kelele mambo mengi yanayoendeshwa ndivyo sivyo, zinasaidia?.

Tujiulize tumepigia kelele mangapi na jee kelele hizo zimesaidia kitu?, au zimeleta mabadiliko? .

Kwa upande wangu nakiri hizi kelele kwa kiasi fulani zimesaidia, ila ili kelele zetu zizae matunda ni kupunguza kelele za maneno matupu na tuongeze matendo.

Japo wapigiwa kelele wanajifanya kuweka pamba masikioni kujifariji kuwa hawasikii kelele zetu na kuvaa miwani ya zege kuwa hawaoni, ila ukweli ni kuwa, sio tuu wanasikia sana kelele zetu, pia wanaona sana, bali pia wanabadilika kidogo kidogo, changing for the better. Kama kelele zetu zitaandamana na matendo, hawawezi kujifanya hawasikii maana matendo yatawasikilizisha, wakijifanya hawaoni, matendo yatawaonyesha kwa jinsi ile ile kura zikipigwa zisipotosha zinatosheshwa, zisipo jaa zinajazilizwa.

Hivyo natoa wito kwa wana JF ambao ni bold enough, kwa mwaka 2017, tusiendelee tuu kupiga kelele kwa kuwa just a Barking dogs who seldom bite, besides barking only, let's start to bite little by little by taking simple actions towards bringing about radical changes we need for the better kwa mambo tunayoyapigia kelele.

Tukiona kuna jambo ambalo linakwenda ndivyo sivyo, tusiishie kulipigia tuu kelele bali pia tupendekeze hatua za vitendo za kuchukua kuibadili hiyo hali na naamini serikali yetu sikivu itatekeleza na isipotekeleza, tutafanya actions kuifanya itekeleze, yaani isipotekeleza, itekelezeshwe kwa jinsi ile ile ilivyochaguliwa kwa kura zisipotosha, zinatosheshwa na kama ni ujazo ukijaza usipojaa unajazilizia, hivyo kwa mwaka 2017, tupunguze maneno maneno kwa kusema sema sana, maneno mengi, kelele nyingi lakini vitendo sifuri. Tuongeze vitendo.

Tuwe watu wa maneno mafupi na vitendo virefu. Tupunguze maneno, tuongeze vitendo kuisaidia Tanzania yetu ibadilike kwa ku change for the better! .

Nakiri kuwa inspired kupandisha bandiko hili katokana na hoja ya mwana JF huyu
Mapambano dhidi ya udikteta yataendelea ndani ya nchi hii.

Hatutakubali kuona uhuru, vyombo vya habari na kujieleza ukiminywa na watu wachache
Hatutakubali kuona katiba ikivunjwa.

Maana naona kuna mbegu ya udikteta inayomea na watu fulani kujifanya miungu watu.

Watanzania hawatoruhusu hayo
Freegodblesslema
Tunamtakabenakiwahai
Wahenga walisema "maneno matupu hayavunji mfupa", na "matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno" hivyo watu mnakuja humu na kauli tupu zenye maneno makali kama hizi kauli za "hatukubali kuona katiba ikivunjwa" as if katiba ikivunjwa kuna kitu mna uwezo wa kufanya!, wakati kiukweli katiba kila siku inavunjwa bila kufanywa lolote kwa sababu hamna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubweka tuu!, wakati kiuhalisia kuna kitu tunaweza kufanya.

Kwa kunisaidia mimi na wengine, usiishie kusema hatutakubali kuona katiba yetu ikivunjwa, bali twende a step further kwa kusema, utafanya nini au unaweza kufanya nini endapo katiba yetu itavunjwa tena, ili kupunguza mabandiko ya maneno matupu, vinginevyo na bandiko hili ni muendelezo wa mabandiko mengi ambayo mimi nayaita mabandiko ya
" a barking dog seldom bite!".

Kwa mwaka 2017, wana jf tupunguze kubweka tuu, ikibidi kung'ata pia tung'ate.
Bye Bye Mwaka 2016, Karibu 2017.
Paskali
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,004
2,000
Tunapenda kujadili matukio tu.

"Wapinzani, siasa zetu za mtandaoni ni za kirahakati tu zisizo na mipango wala mikakati ya kutuwezesha kushika dola."

Nasema hivi kwasababu,interest yetu kubwa kujadili habari na matutukio tu.Watawala wanapofanya maamuzi au mambo mabaya sisu hujikita zaidi kuyajadili na kuyakosoa lakini hakuna mikakati tunayoiweka kutumia mapungufu hayo kama mtaji wa kisiasa ili tuweze kuidhofisha na kuiondia CCM madarakani.

Mfano,swala la kujenga Airport huko Chato tumeishia kujadili na kuponda tu lakini hatuweki mikakati yoyote ya kulitumia swala hili kuonyesha ni jinsi gani swala hili linaweza kuwa limeathiri maisha ya watu wengine na pia hatuna mikakati ya kusambaza habari hii ili iwafikie wananchi wengi zaidi maana wengi hawajui nini kinaendelea huko Chato.

Mfano Waziri Kivuli wa ujenzi angehoji au kulifanya uchambuzi swala la kujenga Airport huko Chato hata waandishi wangeandika na taarfa zingewafikia wananchi wengi zaidi ila tuko kimya tume-relax tu alafu tunataka kushika dola!

Hata viongozi wa upinzani nao wameshindwa kabisa hata kutumia mitandao ya kijamii kusambaza habari kama hizi au kuhoji baadhi ya mambo kama alivyofanya Zitto kuhoji taarifa ya uchumi ilyotolewa na BOT pamoja na swala la malori zaidi ya 15,000 kukosa kazi kutokana na kodi kubwa.
 
Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
23,292
2,000
ukisema uende further kwa hatua zaidi kama unavyopendekeza ndipo hapo MANENO UCHOCHEZI NA KUHATARISHA AMANI YETU yanapokuja..
- binafsi nimekata tamaa na siwezi kufanya lolote zaidi ya kulalamika tu, labda ningekuwa public figure kama mbunge, mwandishi wa habari, politician au awaye yote mwenye ushawishi wa wazi katika jamii na mwenyewe kufahamika vizuri. Nayasema haya kwakuwa watu wa p"public figures" hao hata wakikamatwa uchochezi(ukweli waliousema) jamii itapaza sauti wakiwa lupango tufauti na sie Watanzania wa kawaida.
- Hivyo basi nashauri wenye kuweza kuyasemea haya myasemeee, na sie wa kawaida nawashauri tuwe making maana tunaweza potea kama punje ya haradari..
BT the way neno langu sio sheria..

remote
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,345
2,000
Sawa tutabadilika

Lakini tutawezaje kuleta mabadiliko chanya? Kwa mfano swala la president kulalamikiwa kukanyaga katiba? Je hapa wajumbe wa JF tunatatua vipi hii issue?

Binafsi naamini lazima njia za kuchukua/kufuata zijulikane lasivyo wengi hapa hatutoelewa nini chakufanya.

Je JF itasaidia kupeleka mashauri kama haya mahakamani? Kwasababu kama ulivyosema kupiga kelele haitoshi sasa hapa hebu tujuze mkuu Paskali njia ni ipi yakufuata?
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,893
2,000
Paschal umekuja na andishi moja la nguvu katika kufunga mwaka huu. Lakini nikuambie kitu jamaa yangu kwa nchi yetu ilivyo hili la kumwaga hasira zetu hapa jukwaani ndio pekee tunaloweza kufanya. Kinyume na hapo labda tuingie msituni, kwenye nchi hii wenye uwezo huo wangalau ni watu wa Arusha na Pemba. Tofauti na hapo hata hili andiko lako litakuwa tamu tu kama mengine bila matokeo chanya.
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,946
2,000
Wanabodi Salaam.

Wakati tukifunga mwaka 2016 na kujiandaa kuupokea mwaka 2017, sisi wana JF individually au collectively inatubidi tujitathimini kama hizi kelele tunazopiga humu kupigia kelele mambo mengi yanayoendeshwa ndivyo sivyo, zinasaidia?.

Tujiulize tumepigia kelele mangapi na jee kumesaidia kuleta mabadiliko? .

Kwa upande wangu nakiri hizi kelele zimesaidia sana. Japo wapigiwa kelele wanajifanya kuweka pamba masikioni kujifariji kuwa hawasikii na kuvaa miwani ya zege kuwa hawaoni, ukweli ni kuwa, sio tuu wanasikia sana, na wanaona sana, bali pia wanabadilika, changing for the better.

Hivyo natoa wito kwa wana JF ambao ni bold enough, kwa mwaka 2017, tusiendelee tuu kuwa just a Barking dogs who seldom bite, besides barking only, let's start to bite little by little by taking simple actions towards bringing about radical changes for the better kwa mambo tunayoyapigia kelele.

Tukiona kuna jambo ambalo linakwenda ndivyo sivyo, tusiishie kulipigia tuu kelele bali pia tupendekeze hatua za kuchukua kuibadili hiyo hali na naamini serikali yetu sikivu itatekeleza na isipotekeleza, tutafanya actions kuifanya itekeleze, yaani isipotekeleza, itekelezeshwe kwa jinsi ile ile ilivyochaguliwa kwa kura zisipotosha, zinatosheshwa na kama ni ujazo ukijaza usipojaa unajazilizia, hivyo kwa mwaka 2017, tupunguze maneno maneno kwa kusema sema sana, maneno mengi, kelele nyingi lakini vitendo sifuri.

Tuwe watu wa maneno mafupi na vitendo virefu. Tupunguze maneno, tuongeze vitendo kuisaidia Tanzania yetu ibadilike kwa ku change for the better! .

Nakiri kuwa inspired kupandisha bandiko hili katokana na hoja ya mwana JF huyu

Maneno matupu hayavunji mfupa, watu mnakuja na kauli zenye maneno makali kama hizi kauli za "hatukubali kuona katiba ikivunjwa" as if katiba ikivunjwa kuna kitu mna uwezo wa kufanya!, wakati kiukweli katiba kila siku inavunjwa bila kufanywa lolote kwa sababu hamna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubweka tuu!.

Kwa kunisaidia mimi na wengine, usiishie kusema hatutakubali kuona katiba yetu ikivunjwa, bali twende a step further kwa kusema, utafanya nini au unaweza kufanya nini endapo katiba yetu itavunjwa tena, ili kupunguza mabandiko ya maneno matupu, vinginevyo na bandiko hili ni muendelezo wa mabandiko mengi ambayo mimi nayaita mabandiko ya
" a barking dog seldom bite!".

Kwa mwaka 2017, wana jf tupunguze kubweka tuu, ikibidi kung'ata pia tung'ate.
Bye Bye Mwaka 2016, Karibu 2017.
Paskali
Mkuu Paskali, ni bahati nzuri andiko lako umeliambatanisha na andiko ambalo content yake ni mambo ambayo bila shaka wewe mwenyewe yamekukoroga sana, na bila shaka kwenye ule mkutano baina yenu (wanahabari) na mwenye nchi uliuliza swali kuhusu mambo hayo, na tukaona majibu yake yakaishia kuwa ni kutolewa kwa tafsiri ya jina lako. Sasa, japokuwa mwaka 2017 ambao unataka/unapendekeza wana JF mmoja mmoja au wote tuuanze kwa kubadilika, kwanini usingeonyesha kupitia andiko hili hili ulilolileta kama rejea, namna ya kubadilika na kuchukua action?
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Kwanza nikutakie heri ya mwaka mpya brother Pascal, 2017 uwe na ujasiri wa kuuliza follow up questions ukiambiwa jina lako linamaanisha ulizaliwa wakati wa njaa.

Tukija kwenye hoja yako naomba nikukumbushe kuwa sisi humu wana JF ni watanzania wa kawaida kabisa, wewe una ujasiri wa kuja na verified account sisi wengine hatulali kuogopa siku server za JF zikikamatwa nani atasomesha hawa watoto wa kaka na mjomba wanaonitegemea na ukizingatia kuwa huenda maiti ikatupwa mto wami na mtu asijue niliko. Kwa nini nisiwe muoga wakati uoga ni jadi yetu watanzania? Nani sio muoga? Lema? Kama Lema sio muoga afukuze mawakili hela ya uwakili itumike kulipia ada watoto wa masikini Arusha. Freeman Aikael Mbowe aliitisha maandamano ya ukuta nchi nzima watu wakajipanga na polisi wakajipanga kwa kushirikiana na JWTZ kwa mazoezi ya "KAWAIDA" siku chache kabla ya maandamano huyu jasiri uchwara aliyeitisha maandamano akaibuka na kusema busara imetumika amewasiliana na viongozi wa dini kuahirisha maandamano. Sisi ni nani hadi twende beyond keyboards/ keypads? Mgombea urais wa UKAWA aliaminiwa watanzania watu wazima zaidi ya milioni sita kwa kupigiwa kura uchaguzi mkuu uliopita, hadi leo hajapita kuwashukuru hao watu milioni sita kwa vile haki ya kikatiba ya kukusanyika kisiasa imenyimwa na jeshi na yeye na watu wake wamenywea,,, huku upande wa pili Mawingu media imeitisha mikutano ya hadhara kwa jina la FIESTA ambayo inafanyika hadi usiku wa manane na waatu wanaenda wakiwa wamekusanyika kwa wingi wanakunywa viroba, kuvuta sigara, bangi, kondomu mfukoni, gizani lakini hakuna uvunjifu wa amani unaotokea wala tishio la kuzuiwa kukusanyika. Pascal, sisi nini nani kwenda beyond? Acha tulee watoto wetu bwana nani anataka kutupwa mto wami kama wale wengine
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,345
2,000
Paschal umekuja na andishi moja la nguvu katika kufunga mwaka huu. Lakini nikuambie kitu jamaa yangu kwa nchi yetu ilivyo hili la kumwaga hasira zetu hapa jukwaani ndio pekee tunaloweza kufanya. Kinyume na hapo labda tuingie msituni, kwenye nchi hii wenye uwezo huo wangalau ni watu wa Arusha na Pemba. Tofauti na hapo hata hili andiko lako litakuwa tamu tu kama mengine bila matokeo chanya.
Hivi suala ya kusaini "petition" kwenye mtandao linanguvu kiasi gani?

Je hapa JF tunaweza kutumia kuleta shinikizo kwa government?

Nimeona watu kama Avaaz.com wanafanya hili? Je hii haina nguvu kuibana government? Sisi tunawezaje kutumia kama JF?

Kama tukiwa serious kwa hii mambo tunawaza fanikiwa kupata njia.

Mwisho serikali isione kufanya hivi ni uasi, hapana tutajaribu tu kuonyesha serikali wapi inakosea kwasababu sisi tupo huku mtaani tunaona uhalisia
 
Mkuu Petition itasaidia nini kwa watu waoga namna hii. Nasema wangalau Arusha na Pemba kuna majasiri ambao wamevunjika moyo kwa woga wa wengine. Sasa hivi inabidi tukae kimya tuongozwe na watu wenye uwezo mdogo wa kututoa hapa tulipo labda wajukuu wetu wanaweza. Huyo Pascal mwenyewe anapendekeza tuchukue hatua za ziada kuliko kupiga kelele lakini ukimwambia tuingie mtaani kwa amani kuonyesha kutokukubaliana na jambo fulani anaenda hospital kuchukua kikaratasi kuonyesha ni mgonjwa ili asiende front line. Kuna mtu jasiri wangalau namuona anasimamia kile anachoamini bila woga naye ni Lema. Lakini hawa akina Mayalla warembo tu.
 
Kwani kuingia mtaani na kuandamana ndoyo njia bora zaidi? Nimeuliza hivi kwasababu umeonyesha kuiamini zaidi. Inamaana serikali ndiyo imekataa katakata kusikiliza sauti za wananchi wao hata kama zinaumuhimu?

Mkuu mimi nipo Arusha, ndiyo hapa Arusha watu wanapenda kuhoji mambo lakini hata mikoa mingine naamini wapo watu wengi tu hawafurahishwi na mambo mengi ya hovyo yanayotokea. Kuhusu ujasiri kuchukua hatua labda hii inasababishwa na mbinu zinazopendekezwa. Kwa mfano wewe unapendekeza kuingia mtaani lakini wapo wanaoona hii swala si gumu hivyo zipo njia nyingine bora kufuata. Na kwa muktadha huu tunaendelea kutafuta hizo njia bora kutatua matatito yetu kama nchi na si kama watu wa Arusha au Pemba.
 
Hebu taja hizo zako ili tuone anayezitii.
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,345
2,000
Hebu taja hizo zako ili tuone anayezitii.
Moja ni hii ya kupata saini za wananchi kuonyeshwa wanakubaliana au hawakubaliani na issue fulani inayoendelea nchini.

Hii ni rahisi kutekeleza lakini sifahamu inanguvu kiasi gani ndiyo maana nikauliza. Pia hii njia inaweza kutumika hata kwawasio tumia Internet. Watu wanafutwa kwenye community zao wanapewa karatasi waweke saini zao.

Haya mambo yanatakiwa yafanywe na wananchi na si wanasiasa. Kama wanasiasa watashiriki basi washiriki kama watu wakawaida tu. Unajua serikali ingependa kusikiliza zaidi raia wake lakini si makundi yanayoongozwa na wanasiasa.

Serikali ikiona wananchi wanasisitiza jambo la haki kabisa kabisa haiwezi kupuuza. Labda hiyo serikali haijielewi kwelikweli.
 
MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
2,000
Mkuu umenena vyema. Lkn ombi langu moja kwako Tunapoanza January tuwekee thread zenye mifano ya unachokishauri ili tupate framework au template ya ushauri wako maana kwenye thread umetoa mfano Wa unachokikataa hyjatupa mfano Wa unachokipendekeza.
Maana hata UN huishia kulaani is bila kuchukua hatua.wapinzani wetu nao utasikia tunalaani ukiukwaji Wa democrasia kisha wanaondoka bila kuchukua hatua. Yawezekana tatizo likawa kubwa zaidi na linaridhishwa kutoka kwa wanasiasa wetu.

Natanguliza shukrani kwako kwa ushauri murua.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,418
2,000
Wanabodi Salaam.

Wakati tukifunga mwaka 2016 na kujiandaa kuupokea mwaka 2017, sisi wana JF individually au collectively inatubidi tujitathimini kama hizi kelele tunazopiga humu kupigia kelele mambo mengi yanayoendeshwa ndivyo sivyo, zinasaidia?.

Tujiulize tumepigia kelele mangapi na jee kumesaidia kuleta mabadiliko? .

Kwa upande wangu nakiri hizi kelele zimesaidia sana. Japo wapigiwa kelele wanajifanya kuweka pamba masikioni kujifariji kuwa hawasikii na kuvaa miwani ya zege kuwa hawaoni, ukweli ni kuwa, sio tuu wanasikia sana, na wanaona sana, bali pia wanabadilika, changing for the better.

Hivyo natoa wito kwa wana JF ambao ni bold enough, kwa mwaka 2017, tusiendelee tuu kuwa just a Barking dogs who seldom bite, besides barking only, let's start to bite little by little by taking simple actions towards bringing about radical changes for the better kwa mambo tunayoyapigia kelele.

Tukiona kuna jambo ambalo linakwenda ndivyo sivyo, tusiishie kulipigia tuu kelele bali pia tupendekeze hatua za kuchukua kuibadili hiyo hali na naamini serikali yetu sikivu itatekeleza na isipotekeleza, tutafanya actions kuifanya itekeleze, yaani isipotekeleza, itekelezeshwe kwa jinsi ile ile ilivyochaguliwa kwa kura zisipotosha, zinatosheshwa na kama ni ujazo ukijaza usipojaa unajazilizia, hivyo kwa mwaka 2017, tupunguze maneno maneno kwa kusema sema sana, maneno mengi, kelele nyingi lakini vitendo sifuri.

Tuwe watu wa maneno mafupi na vitendo virefu. Tupunguze maneno, tuongeze vitendo kuisaidia Tanzania yetu ibadilike kwa ku change for the better! .

Nakiri kuwa inspired kupandisha bandiko hili katokana na hoja ya mwana JF huyu

Maneno matupu hayavunji mfupa, watu mnakuja na kauli zenye maneno makali kama hizi kauli za "hatukubali kuona katiba ikivunjwa" as if katiba ikivunjwa kuna kitu mna uwezo wa kufanya!, wakati kiukweli katiba kila siku inavunjwa bila kufanywa lolote kwa sababu hamna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubweka tuu!.

Kwa kunisaidia mimi na wengine, usiishie kusema hatutakubali kuona katiba yetu ikivunjwa, bali twende a step further kwa kusema, utafanya nini au unaweza kufanya nini endapo katiba yetu itavunjwa tena, ili kupunguza mabandiko ya maneno matupu, vinginevyo na bandiko hili ni muendelezo wa mabandiko mengi ambayo mimi nayaita mabandiko ya
" a barking dog seldom bite!".

Kwa mwaka 2017, wana jf tupunguze kubweka tuu, ikibidi kung'ata pia tung'ate.
Bye Bye Mwaka 2016, Karibu 2017.
Paskali
Toa pendekezo tufanyeje kuacha maneno. Tufanyeje? Ukienda barabarani ujue unakufa fafefifofu! Unapata ulemavu wa kudumu milele na milele amina! UN hopeless, AU ndio feces matupu!!! Twende kwa Trump? Hana maslai na Tanzania!!!! Paskali, tufanyeje, toa pendekezo.
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
11,247
2,000
Kwa KUWA mikutano ya kisiasa Umepigwa marufuku. Na ishu ya kusaidia ilikuwa ni Habari Sasa sheria inawabana. Ila huku jf na Fb watumiaji wengi ni vijana na wazi wameonyeshwa kutopendezwa na baadhi ya mambo ya kiutawala.. Sasa kinachobaki ni kuendelea kufanya mijadala Ila tuinge mkono serikali Kwa mambo mazuri inayofanya. Hii nchi yetu. Umoja sio lazima Ila UPENDO tuudimishe ili tusije kumwagana Damu wala fujo. Kuingia mitaani na kufanya action zozote ni HARAKATI za kiwaki Kwa DuniA ya Sasa. Tukae kijanja hivi. Tuwekeze kwenye mitandao..ccm itakufa yenyewe tena hivi endapo vijana wengi wakishiriki uchaguzi..tuendelee kuhabarishana ukweli utafunuka wenyewe..kama magufuli akifanikiwa aliyotuhaidi tutampigia kura tena.

SISI wapinzani tubadili mitizamo. Hii habari ya kutaka kuwaaminisha watanzania kwamba rais magufuli ni dikteta wakati mifano iko michache ya wapi ameonyesha udikteta wake.. Kama ni siasa za kufanya Sasa ni kujadili mambo ya kiuchumi na katiba mpya. Hizi mbinu za kipropaganda za kumbambikizia rais kuwa ni dikteta ni mbinu mbovu. Tusipandikize habari za matukio Kwa watanzania tupandikize mijadala ya Muda mrefu... Sasa MFANO mimi Sioni mantiki ya watu KULALAMIKA rais kuzungumza kwenye clouds TV. Sioni kama ni mambo ya tija ya kuchukulia point. Wapinzani uliopo mtandaoni uhoji mambo ya msingi Sana.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,893
2,000
Moja ni hii ya kupata saini za wananchi kuonyeshwa wanakubaliana au hawakubaliani na issue fulani inayoendelea nchini.

Hii ni rahisi kutekeleza lakini sifahamu inanguvu kiasi gani ndiyo maana nikauliza. Pia hii njia inaweza kutumika hata kwawasio tumia Internet. Watu wanafutwa kwenye community zao wanapewa karatasi waweke saini zao.

Haya mambo yanatakiwa yafanywe na wananchi na si wanasiasa. Kama wanasiasa watashiriki basi washiriki kama watu wakawaida tu. Unajua serikali ingependa kusikiliza zaidi raia wake lakini si makundi yanayoongozwa na wanasiasa.

Serikali ikiona wananchi wanasisitiza jambo la haki kabisa kabisa haiwezi kupuuza. Labda hiyo serikali haijielewi kwelikweli.

Huyo atakayekuwa anapitisha hiyo karatasi ya kusaini atakuwa anatokea platform gani? Ukiwa huna sehemu maalum watasema kuna madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchi, wakati ww unasema ni wanasiasa. Kama utapitia NGOndio ujue itafungwa kwani utaambiwa inatumika kisiasa. Kwa mazingara yalivyo mbinu yako ni ngumu kufanya kazi.
 
linguistics

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
4,527
2,000
Kwanza nikutakie heri ya mwaka mpya brother Pascal, 2017 uwe na ujasiri wa kuuliza follow up questions ukiambiwa jina lako linamaanisha ulizaliwa wakati wa njaa.

Tukija kwenye hoja yako naomba nikukumbushe kuwa sisi humu wana JF ni watanzania wa kawaida kabisa, wewe una ujasiri wa kuja na verified account sisi wengine hatulali kuogopa siku server za JF zikikamatwa nani atasomesha hawa watoto wa kaka na mjomba wanaonitegemea na ukizingatia kuwa huenda maiti ikatupwa mto wami na mtu asijue niliko. Kwa nini nisiwe muoga wakati uoga ni jadi yetu watanzania? Nani sio muoga? Lema? Kama Lema sio muoga afukuze mawakili hela ya uwakili itumike kulipia ada watoto wa masikini Arusha. Freeman Aikael Mbowe aliitisha maandamano ya ukuta nchi nzima watu wakajipanga na polisi wakajipanga kwa kushirikiana na JWTZ kwa mazoezi ya "KAWAIDA" siku chache kabla ya maandamano huyu jasiri uchwara aliyeitisha maandamano akaibuka na kusema busara imetumika amewasiliana na viongozi wa dini kuahirisha maandamano. Sisi ni nani hadi twende beyond keyboards/ keypads? Mgombea urais wa UKAWA aliaminiwa watanzania watu wazima zaidi ya milioni sita kwa kupigiwa kura uchaguzi mkuu uliopita, hadi leo hajapita kuwashukuru hao watu milioni sita kwa vile haki ya kikatiba ya kukusanyika kisiasa imenyimwa na jeshi na yeye na watu wake wamenywea,,, huku upande wa pili Mawingu media imeitisha mikutano ya hadhara kwa jina la FIESTA ambayo inafanyika hadi usiku wa manane na waatu wanaenda wakiwa wamekusanyika kwa wingi wanakunywa viroba, kuvuta sigara, bangi, kondomu mfukoni, gizani lakini hakuna uvunjifu wa amani unaotokea wala tishio la kuzuiwa kukusanyika. Pascal, sisi nini nani kwenda beyond? Acha tulee watoto wetu bwana nani anataka kutupwa mto wami kama wale wengine
Sawa kabisa mkuu...huwa napata shida sana nnapoona watu wanaandika kuwa walimu ni waoga eti kwa kuwa hawadai haki zao. Wanadai siku zote lkn wakigoma wakapigwa mabomu, kukamatwa na kuishia kufukuzwa kazi nani atalea familia zao? Wewe umesema vema. Ili jambo lisikike lazima nguvu kubwa itumike. Watu hawajui kuwa ni miaka tu ya hivi karibuni ndo idadi ya walimu wa msingi wa kiume imeenda inaongezeka wengi walikuwa wa kike...sio rahisi wanawake kuanza maandamano na kukimbizana na polisi na ukizingatia nature ya mafunzo na kazi yao. Pascal umesema vema NAKERWA SANA NA MIJITU MIOGA INAYOPENDA KUJIFANYA IPO NGANGARI NYUMA YA KEYBOARD.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom