2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite", Tusiishie Kubweka Tu, Tung'ate!

Kwa vile leo ni mwisho wa mwaka, nafanya tuu marejeo, niliwa kushauri nini, nini kilifanyika, na matokeo ni nini.
Kwaheri 2020, karibu 2021.
Mimi na familia yangu tawatakia Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali
 
Wanabodi Salaam.

Wakati tukifunga mwaka, sisi wana JF individually au collectively inatubidi tujitathimini kama hizi kelele tunazopiga humu kupigia kelele mambo mengi yanayoendeshwa ndivyo sivyo, zinasaidia?.

Tujiulize tumepigia kelele mangapi na jee kelele hizo zimesaidia kitu?, au zimeleta mabadiliko? .

Kwa upande wangu nakiri hizi kelele kwa kiasi fulani zimesaidia, ila ili kelele zetu zizae matunda ni kupunguza kelele za maneno matupu na tuongeze matendo.

Japo wapigiwa kelele wanajifanya kuweka pamba masikioni kujifariji kuwa hawasikii kelele zetu na kuvaa miwani ya zege kuwa hawaoni, ila ukweli ni kuwa, sio tuu wanasikia sana kelele zetu, pia wanaona sana, bali pia wanabadilika kidogo kidogo, changing for the better. Kama kelele zetu zitaandamana na matendo, hawawezi kujifanya hawasikii maana matendo yatawasikilizisha, wakijifanya hawaoni, matendo yatawaonyesha kwa jinsi ile ile kura zikipigwa zisipotosha zinatosheshwa, zisipo jaa zinajazilizwa.

Hivyo natoa wito kwa wana JF ambao ni bold enough, kwa mwaka 2017, tusiendelee tuu kupiga kelele kwa kuwa just a Barking dogs who seldom bite, besides barking only, let's start to bite little by little by taking simple actions towards bringing about radical changes we need for the better kwa mambo tunayoyapigia kelele.

Tukiona kuna jambo ambalo linakwenda ndivyo sivyo, tusiishie kulipigia tuu kelele bali pia tupendekeze hatua za vitendo za kuchukua kuibadili hiyo hali na naamini serikali yetu sikivu itatekeleza na isipotekeleza, tutafanya actions kuifanya itekeleze, yaani isipotekeleza, itekelezeshwe kwa jinsi ile ile ilivyochaguliwa kwa kura zisipotosha, zinatosheshwa na kama ni ujazo ukijaza usipojaa unajazilizia, hivyo kwa mwaka 2017, tupunguze maneno maneno kwa kusema sema sana, maneno mengi, kelele nyingi lakini vitendo sifuri. Tuongeze vitendo.

Tuwe watu wa maneno mafupi na vitendo virefu. Tupunguze maneno, tuongeze vitendo kuisaidia Tanzania yetu ibadilike kwa ku change for the better! .

Wahenga walisema "maneno matupu hayavunji mfupa", na "matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno" hivyo watu mnakuja humu na kauli tupu zenye maneno makali kama hizi kauli za "hatukubali kuona katiba ikivunjwa" as if katiba ikivunjwa kuna kitu mna uwezo wa kufanya!, wakati kiukweli katiba kila siku inavunjwa bila kufanywa lolote kwa sababu hamna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubweka tuu!, wakati kiuhalisia kuna kitu tunaweza kufanya..
Paskali

Japo hili ni wazo la siku nyingi lakini bado liko valid, leo serikali ime recognises uwepo wa jf, kwa Waziri wa habari kutembelea jf, hivyo hili wazo nalifufua,

the action ya kufanya ni JF ianzishe its own online TV.

The TV will fully be owned na JF, operated by jf, run by jf, na sisi members tunakuwa ni contributors.
mnalionaje hili?.
Bado haijafahamika alichoteta na Mkurugenzi wetu Maxence Melo , bali muda wote wa mazungumzo yao wote walionekana kuwa na nyuso zenye bashasha , jambo lililoashiria amani kutawala .

Mungu ibariki JF

====

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa @innocentbash leo Agosti 26, 2021 ametembelea Ofisi za Jamii Forums JamiiForums jijini Dar

Waziri ameweza kujionea jinsi Taasisi ya Jamii Forums inavyofanya kazi pamoja na kukutana na baadhi ya watendaji wa taasisi yetu

Pamoja na mambo mengine, Waziri amepongeza jitihada za Jamii Forums katika kuelimisha umma juu ya masuala anuai ikiwemo afya ya jamii na hasa Ugonjwa wa UVIKO-19
View attachment 1910052View attachment 1910053View attachment 1910054
Hongera sana Mkuu Maxence Melo , this is the beginning of government official recognition.
Ile the JF spirit ya "be the first to know" worked very well hata juzi kwenye hili tukio la Ubalozi wa Ufaransa ni JF ndio wa kwanza kutoa breaking news tangu jamaa akiwa Salender bridge.

Big up Maxence Melo,
Big up wana Jf.
Let's keep up the jf spirit
Long Live JF
P
 
Wanabodi Salaam.

Wakati tukifunga mwaka 2016 na kujiandaa kuupokea mwaka 2017, sisi wana JF individually au collectively inatubidi tujitathimini kama hizi kelele tunazopiga humu kupigia kelele mambo mengi yanayoendeshwa ndivyo sivyo, zinasaidia?.

Tujiulize tumepigia kelele mangapi na jee kelele hizo zimesaidia kitu?, au zimeleta mabadiliko? .

Kwa upande wangu nakiri hizi kelele kwa kiasi fulani zimesaidia, ila ili kelele zetu zizae matunda ni kupunguza kelele za maneno matupu na tuongeze matendo.

Japo wapigiwa kelele wanajifanya kuweka pamba masikioni kujifariji kuwa hawasikii kelele zetu na kuvaa miwani ya zege kuwa hawaoni, ila ukweli ni kuwa, sio tuu wanasikia sana kelele zetu, pia wanaona sana, bali pia wanabadilika kidogo kidogo, changing for the better. Kama kelele zetu zitaandamana na matendo, hawawezi kujifanya hawasikii maana matendo yatawasikilizisha, wakijifanya hawaoni, matendo yatawaonyesha kwa jinsi ile ile kura zikipigwa zisipotosha zinatosheshwa, zisipo jaa zinajazilizwa.

Hivyo natoa wito kwa wana JF ambao ni bold enough, kwa mwaka 2017, tusiendelee tuu kupiga kelele kwa kuwa just a Barking dogs who seldom bite, besides barking only, let's start to bite little by little by taking simple actions towards bringing about radical changes we need for the better kwa mambo tunayoyapigia kelele.

Tukiona kuna jambo ambalo linakwenda ndivyo sivyo, tusiishie kulipigia tuu kelele bali pia tupendekeze hatua za vitendo za kuchukua kuibadili hiyo hali na naamini serikali yetu sikivu itatekeleza na isipotekeleza, tutafanya actions kuifanya itekeleze, yaani isipotekeleza, itekelezeshwe kwa jinsi ile ile ilivyochaguliwa kwa kura zisipotosha, zinatosheshwa na kama ni ujazo ukijaza usipojaa unajazilizia, hivyo kwa mwaka 2017, tupunguze maneno maneno kwa kusema sema sana, maneno mengi, kelele nyingi lakini vitendo sifuri. Tuongeze vitendo.

Tuwe watu wa maneno mafupi na vitendo virefu. Tupunguze maneno, tuongeze vitendo kuisaidia Tanzania yetu ibadilike kwa ku change for the better! .

Nakiri kuwa inspired kupandisha bandiko hili katokana na hoja ya mwana JF huyu

Wahenga walisema "maneno matupu hayavunji mfupa", na "matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno" hivyo watu mnakuja humu na kauli tupu zenye maneno makali kama hizi kauli za "hatukubali kuona katiba ikivunjwa" as if katiba ikivunjwa kuna kitu mna uwezo wa kufanya!, wakati kiukweli katiba kila siku inavunjwa bila kufanywa lolote kwa sababu hamna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kubweka tuu!, wakati kiuhalisia kuna kitu tunaweza kufanya.

Kwa kunisaidia mimi na wengine, usiishie kusema hatutakubali kuona katiba yetu ikivunjwa, bali twende a step further kwa kusema, utafanya nini au unaweza kufanya nini endapo katiba yetu itavunjwa tena, ili kupunguza mabandiko ya maneno matupu, vinginevyo na bandiko hili ni muendelezo wa mabandiko mengi ambayo mimi nayaita mabandiko ya
" a barking dog seldom bite!".

Kwa mwaka 2017, wana jf tupunguze kubweka tuu, ikibidi kung'ata pia tung'ate.
Bye Bye Mwaka 2016, Karibu 2017.
Paskali

Wajameni, baada ya mimi mwana JF mwenzenu kuwa admitted as an advocate, I will do something about this!.
P
 
Back
Top Bottom