Ni nani alifuatilia mauaji ya Giulio Regeni? Mwanafunzi wa Italia aliyetekwa nyara Misri kisha kuuawa kwa tuhuma za ujasusi

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
EGYPTY - ITALY ON THE VERGE OF DIPLOMATIC STANDOFF: Mvutano mkubwa wa kidiplomasia baina ya Italia na Misri juu ya kifo cha mwanafunzi Giulio Regeni.

14489.jpeg

Mnamo Septemba 5, Misri na Italia zilianza tena uhusiano wao wa kidiplomasia baada ya mwaka mmoja na nusu, wakimrudisha Balozi wa Italia Giampaolo Gantini ofisini kwake Cairo mara baada ya tarehe 14 Septemba.

Mahusiano ya pande hizi mbili kati ya Roma na Cairo yalizorota wakati mwili ulioteswa wa Msomi wa Kiitaliano kutoka chuo cha Cambridge Giulio Regeni ulipopatikana nchini Misri, mauaji ambayo yanaaminika kufanywa na vikosi vya usalama vya serikali.

images (4).jpg

Katika kujibu, Italia ilimuita Balozi Maurizio Massari wa wakati huo na kumteua Gantini kama "non-resident" mnamo Mei 2016. Regeni alikuwa akifanya tafiti juu ya vyama vya wafanyikazi huko Misri wakati alipotekwa nyara, kuteswa na mwishowe kuuawa.

Ilikuja kufahamika kwamba polisi wa Misri walikuwa wamemshikilia Regeni na kisha kumhamishia kwenye eneo lenye ulinzi mkali linalomilikiwa na idara ya usalama wa ndani wa Misri siku aliyotekwa nyara, jambo ambalo hapo awali lilipingwa na mamlaka za usalama za Misri.

images (2).jpg

Ni nani alifuatilia mkasa huu kwa kina? Ninaomba ufafanuzi tafadhali.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

MAONI YA WADAU;
==========
Shukrani, Mkuu kwa kunistua juu ya hili tukio.

Ni kweli nilisikia mtikisiko wa uhusiano kati ya Misri na Italy juu ya mauaji ya mwanafunzi huyu. Ingawa wakati huo sikulipa umuhimu sana. Leo baada ya kunistua ndiyo nimefuatilia. Nimefuatilia kwa haraka habari za tukio hili mtandaoni. Inaoneka huyu msomi wa kiitali naweza kuwa kweli alikuwa 'mamluki' (msisitizo yawezekana maana sina uhakika).

Uwezekano huo unatokana na kumbukumbu inayoonesha kuwa 'marehemu' aliwahi kufanya kazi na Cambridge Analytica. Hawa CA rekodi zao si nzuri kwani wanatuhumiwa kuiba taarifa za raia ili kufanikisha utafiti wao ama kurubuni raia juu ya mwenendo ambao utawanufaisha wateja wao kwa faida ya wachache na hasara kwa wengi.

Pia kitendo cha UK kushindwa kutoa ushirikiano katika uchunguzi uliokuwa unafanywa na Italy una ongeza mashaka ya kuwa uwenda marehemu alikuwa mamluki! Na mwisho, ni kitendo cha US kudai kina 'ushahidi wa kishindo' juu ya wale waliohusika na mauaji ya msomi wa kiitaliano. Hata hivyo, US hakutoa ushihidi huo. Ikumbukwe US ana ushirikiano mzuri katika mambo ya kupeana taarifa za kiitelijensia na Misri. General Sisi yasemwa ni mtu wao hawa Wamarekani!

Kwa uchache haya ndigo yamenijia kichwani baada ya kuchakurachakura mtandaoni juu ya mkasa huu.

Kwa mara nyingi, shukrani mleta mada.
==========
Nimejaribu kutafuta story ya huyu jamaa. Inawezekana sana alikuwa ajenti wa Israel. Alishakaa sana Misri, kwa kuja na kuondoka kabla hajaja mara ya mwisho alipodakwa.

Aliwahi kufika Israel na inasemwa alikuwa na totoz ya kule.

Alikuwa anafuatiliwa kwa muda mrefu na mashushushu wa Misri kabla hajatiwa nguvuni, kuteswa na kuuawa

Alikuwa yuko karibu sana na vijikundi vya mitaani, alijichanganya navyo sana

Inavyoonekana kujishughulisha na utafiti kama mwanafunzi wa PhD ilikuwa kama kijificho fulani ili aweze kufanya mishemishe yake bila kung'amuliwa
 
Shukrani, Mkuu kwa kunistua juu ya hili tukio.

Ni kweli nilisikia mtikisiko wa uhusiano kati ya Misri na Italy juu ya mauaji ya mwanafunzi huyu. Ingawa wakati huo sikulipa umuhimu sana. Leo baada ya kunistua ndiyo nimefuatilia. Nimefuatilia kwa haraka habari za tukio hili mtandaoni. Inaoneka huyu msomi wa kiitali naweza kuwa kweli alikuwa 'mamluki' (msisitizo yawezekana maana sina uhakika).

Uwezekano huo unatokana na kumbukumbu inayoonesha kuwa 'marehemu' aliwahi kufanya kazi na Cambridge Analytica. Hawa CA rekodi zao si nzuri kwani wanatuhumiwa kuiba taarifa za raia ili kufanikisha utafiti wao ama kurubuni raia juu ya mwenendo ambao utawanufaisha wateja wao kwa faida ya wachache na hasara kwa wengi.

Pia kitendo cha UK kushindwa kutoa ushirikiano katika uchunguzi uliokuwa unafanywa na Italy una ongeza mashaka ya kuwa uwenda marehemu alikuwa mamluki! Na mwisho, ni kitendo cha US kudai kina 'ushahidi wa kishindo' juu ya wale waliohusika na mauaji ya msomi wa kiitaliano. Hata hivyo, US hakutoa ushihidi huo. Ikumbukwe US ana ushirikiano mzuri katika mambo ya kupeana taarifa za kiitelijensia na Misri. General Sisi yasemwa ni mtu wao hawa Wamarekani!

Kwa uchache haya ndigo yamenijia kichwani baada ya kuchakurachakura mtandaoni juu ya mkasa huu.

Kwa mara nyingi, shukrani mleta mada.
 
When the body of the Italian doctoral student Giulio Regeni was found by the side of a Cairo highway in 2016, his mother later said she only recognised her son's corpse by “the tip of his nose”, as he had suffered such extensive torture.
Waarabu wanafanyaga torture mbaya sana. Ulizia utawala wa Saddam Hussein
 
Back
Top Bottom