Moshi: Mlinzi aliyehukumiwa kifo kwa Mauaji ya Mwanafunzi wa Sekondari ya Scolastica aachiwa huru

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Mahakama imemuachia huru aliyekuwa mlinzi wa Shule ya Sekondari Scolastica, iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Hamis Chacha (34) aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kumuua kwa makusudi mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi.

Chacha ameachiwa huru baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania kusikiliza rufaa, kushusha shitaka lake kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa ya bila kukusudia, baada ya kubaini hakuwa na nia ovu ya kuua.

Maelezo ya kosa hilo yanaeleza kuwa Septemba 6, 2017 saa 2 usiku, katika mji wa Himo, mlinzi huyo alimuua mwanafunzi Humphrey aliyekuwa kidato cha pili kwa kumpiga na ubapa wa panga.

Baada ya kesi kusikilizwa, Juni 3, 2019 Jaji Firmin Matogolo alimtia hatiani.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, siku hiyo (Septemba 6, 2017) mlinzi akiwa doria nje ya uzio wa shule, alisikia kishindo cha mtu kuruka ukuta kutoka ndani ya shule.

Alipofuatilia aliona mtu akikimbia, alimkimbiza na alipomkaribia alimpiga kwa ubapa wa panga lakini hakusimama.

Mlinzi aliendelea kumkimbiza, umbali mfupi baadaye, mtu huyo alianguka. Alimsogelea na kumpiga tena kwa ubapa wa panga, mtu huyo ambaye wakati huo hakuwa amemtambua hakuamka tena.

Mlinzi huyo alimpigia simu mmiliki wa shule, Edward Shayo na mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa; walibaini mtu yule ni mwanafunzi Humphrey Makundi (16) na alikuwa amekufa, ndipo walijadiliana na kuamua kuutupa mwili katika Mto Ghona ulio jirani na shule. Mwili uligundulika Septemba 12, 2017 katika mto huo ukiwa umeanza kuharibika na ilibainika ni wa mwanafunzi huyo.

Shayo, Nabiswa na Chacha walikamatwa na kuhusishwa na mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi huyo.

Baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, iliwaondoa Shayo na Nabiswa katika kosa la mauaji ya kukusudia na kuwatia hatiani kwa kosa dogo la kuficha taarifa za tukio hilo na kuwahukumu kifungo cha miaka minne jela.

Wawili hao walishamaliza kutumikia vifungo vyao gerezani na kurejea uraiani; mlinzi huyo akimtumia Wakili David Shillatu alikata rufaa kupinga kutiwa hatiani na adhabu ya kifo aliyopewa akiegemea katika sababu kuu mbili za rufaa.

Moja walipinga uchukuaji wa maelezo ya ungamo kwa mlinzi wa amani kuwa hayakufuata mwongozo wa Jaji Mkuu na hayakuungwa mkono na ushahidi mwingine, hapakuwa na nia ovu; na pili shitaka halikuthibitishwa bila kuacha shaka.

Chanzo: Mwananchi
 
Mahakama imemuachia huru aliyekuwa mlinzi wa Shule ya Sekondari Scolastica, iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Hamis Chacha (34) aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kumuua kwa makusudi mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi.

Chacha ameachiwa huru baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania kusikiliza rufaa, kushusha shitaka lake kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa ya bila kukusudia, baada ya kubaini hakuwa na nia ovu ya kuua.

Maelezo ya kosa hilo yanaeleza kuwa Septemba 6, 2017 saa 2 usiku, katika mji wa Himo, mlinzi huyo alimuua mwanafunzi Humphrey aliyekuwa kidato cha pili kwa kumpiga na ubapa wa panga.

Baada ya kesi kusikilizwa, Juni 3, 2019 Jaji Firmin Matogolo alimtia hatiani.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, siku hiyo (Septemba 6, 2017) mlinzi akiwa doria nje ya uzio wa shule, alisikia kishindo cha mtu kuruka ukuta kutoka ndani ya shule.

Alipofuatilia aliona mtu akikimbia, alimkimbiza naa lipomkaribia alimpiga kwa ubapa wa panga lakinia hakusimama.

Mlinzi aliendelea kumkimbiza, umbali mfupi baadaye, mtu huyo alianguka. Alimsogelea na kumpiga tena kwa ubapa wa panga, mtu huyo ambaye wakati huo hakuwa amemtambua hakuamka tena.

Mlinzi huyo alimpigia simu mmiliki wa shule, Edward Shayon na mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa; walibaini mtu yule ni mwanafunzi Humphrey Makundi (16) na alikuwa amekufa, ndipo walijadiliana na kuamua kuutupa mwili katika Mto Ghona ulio jirani na shule. Mwili uligundulika Septemba 12, 2017 katika mto huo ukiwa umeanza kuharibika na ilibainika ni wa mwanafunzi huyo.

Shayo, Nabiswa na Chacha walikamatwa na kuhusishwa na mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi huyo.

Baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, iliwaondoa Shayo na Nabiswa katika kosa la mauaji ya kukusudia na kuwatia hatiani kwa kosa dogo la kuficha taarifa za tukio hilo na kuwahukumu kifungo cha miaka minne jela. Wawili hao walishamaliza kutumikia vifungo vyao gerezani na kurejea uraiani.

Mlinzi huyo akimtumia Wakili David Shillatu alikata rufaa kupinga kutiwa hatiani na adhabu ya kifo aliyopewa akiegemea katika sababu kuu mbili za rufaa. Moja walipinga uchukuaji wa maelezo ya ungamo kwa mlinzi wa amani kuwa hayakufuata mwongozo wa Jaji Mkuu na hayakuungwa mkono na ushahidi mwingine, hapakuwa na nia ovu; na pili shitaka halikuthibitishwa bila kuacha shaka.

Hukumu ya Majaji

Katika hukumu iliyotolewa Ijumaa iliyopita na kuwekwa katika mtandao wa Mahakama, jopo la majaji watatu, Jacob Mwambelege, Patricia Fikirini na Benhaji Masoud walikataa hoja kuwa uchukuaji maelezo ya ungamo yaliyochukuliwa na mlinzi wa amani ulikiuka sheria.

Badala yake, majaji walikubaliana na hoja za Wakili wa Serikali Mkuu, Cecilia Mkonongo aliyesaidiana na mawakili Peter Utafu na Philbert Mashurano kuwa yalichukuliwa kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania.

Majaji hao walisema maelezo yalipokewa kwa usahihi mahakamani kama kielelezo cha kukiri kutenda kosa hilo, wakashikilia msimamo kuwa ulikuwa ushahidi bora dhidi ya mrufani na ushahidi bora kwenye jinai ni ushahidi wa aina hiyo.

"Tumeridhika kuwa ushahidi ulioletwa na upande wa mashitaka ulitosheleza kumtia hatiani mrufani kwa kusababisha kifo cha marehemu. Kukiri kwake kuliungwa mkono na ushahidi wa mazingira ambako hakukuhitaji ushahidi zaidi," inaeleza sehemu ya hukumu.

Kuhusu hoja ya kutokuwapo kwa nia ovu, wakili Utafu alishikilia msimamo kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kilisababishwa na mrufani kwa kuendelea kumpiga mfululizo hata baada ya kuanguka, kuwa hiyo inathibitisha nia ovu ya kuua kwa kukusudia.

Hata hivyo, majaji katika hukumu yao, walisema baada ya kupitia maelezo ya ungamo ya mrufani ambayo ndiyo ushahidi muhimu katika kesi ya jinai, hawaoni kurudia rudia kwa mrufani kumpiga kama wakili Utafu alivyoeleza.

Katika maelezo hayo, kwa mujibu wa majaji yanaelezea namna alivyokimbizwa na kwenye kona alipigwa bapa na baada ya muda mfupi baadaye alianguka na kwa mara nyingine, mlinzi alimpiga bapa lingine.

Majaji walisema inaonyesha alipigwa mara mbili; ya kwanza kwenye kona na ya pili baada ya kuanguka chini na mrufani kama alikuwa na nia ovu ya kutaka kumuua, angempiga kwa kutumia upande wenye makali lakini alitumia ubapa.

"Hapo hatufikiri kilichotokea kabla na baada ya kitendo hicho kinatengeneza nia ovu ya kutenda kosa la mauaji. Mrufani kwa mazingira haya alipaswa kutiwa hatiani kwa kosa dogo la kuua bila kukusudia.

"Kuhusu adhabu, tumezingatia muda ambao mrufani ameutumia akiwa gerezani tangu alipotiwa hatiani Juni 3, 2019. Tunaona ametumikia muda wa kutosha kulingana na adhabu ambayo angepewa baada ya kutiwa hatiani kwa kuua bila kukusudia," inaeleza hukumu.

Majaji katika hukumu hiyo wanasema, "Kwa hiyo tunakubali sehemu ya rufaa kwa kubatilisha na kufuta adhabu ya kifo aliyopewa mrufani na kuibadili na kutiwa hatiani kwa kuua bila kukusudia na adhabu kama angetiwa hatiani, hivyo aachiwe huru labda kama anashikiliwa kwa kosa lingine."

Akizungumza na gazeti hili jana, baada ya hukumu hiyo, wakili Shillatu aliyemtetea mrufani huyo, alisema ametimiza wajibu wake na Mahakama imetimiza wake wa kikatiba wa kutoa haki.

Source: Mwananchi.
 
Mahakama imemuachia huru aliyekuwa mlinzi wa Shule ya Sekondari Scolastica, iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Hamis Chacha (34) aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kumuua kwa makusudi mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi...
Kwahiyo kuua bila kukusudia kesi yake inaanza lini na akiwa uraiani au anabaki kwanza rumande?
 
Back
Top Bottom