MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Najua tupo 2010 na hata uchaguzi wa mwaka huu hauja isha. Najua bado watu wapo katika hali ya furaha na matumaini mapya kusikia Mh. Slaa ana gombea uraisi. Najua wengi wetu tuna tamani muda uwe huu na wakati uwe huu. Ukweli ni kwamba Tanzania haija jipanga kwa mabadiliko yoyote 2010. Vumbi likisha tulia tuta kuta hali ni ile ile.
Watanzania tuna kasumba ya kusubiria uchaguzi ndiyo kuwa na mwamko wa kisiasa. Hili lime thibitishwa na hali halisi ya miaka 2005-2010. Tunge kuwa ni nchi nyingine basi kwa sasa tunge kuwa tuna subiria kuhalalisha uongozi wa chama kipya na utawala mpya. Sasa pamoja na yote yaliyo tokea miaka hii mitano bado hakuna uhakika wa upinzani kushinda. Hapo lazima wenyewe tujiulize ni kwa nini.
Binafsi sina mapenzi na chama chochote cha upinzani. Na sifichi ukweli kwamba nime kuwa mpenzi wa CCM tokea udogo haswa kutokana na kumu idolize Nyerere. Ila pia naweka mapenzi ya nchi mbele ya mapenzi ya chama. Najua Tanzania ita nufaika sana na upinzani wenye nguvi na vyama vinavyo pokezana mara kwa mara. Najua fika kwamba mwaka huu uraisi unge takiwa uende kwa Slaa. Lakini sidhani kama hayo yata tokea mwaka huu.
Wakuu safari bado ni ndefu. Ushindi hautokani tu na hisia na hamu za ushindi bali hutokana na mikakati na utekelezaji. Tanzania bado hatuja jiwekea mazingira ya kupokezana madaraka au kuweka utaifa mbele ya itikadi za kichama na mapenzi yetu na watu binafsi.
Tuchukulie kwa muda mfano wa timu. Kwenye timu yoyote kuna yule mchezaji mmoja au wawili ambao ndiyo mastaa wa kikosi. Lakini timu hii hata iwe na mastaa wangapi au staa mkubwa kiasi gani haiwezi kufanikiwa bila wachezaji wa akiba wazuri, kocha mzuri na uongozi mzuri. Staa yoyote hawezi kubadilisha timu mbovu bila kete zingine kuji panga vizuri.
Wagombeaji "mastaa: tunao wengi tu kuanzia ngazi za udiwani mpaka uraisi. Lakini swala ni je hawa "wachezaji nyota" wana weza kufanikiwa bila mazingira ya kufanikiwa kuwepo? Tume jiwezesha vipi kuhakikisha kwamba wachezaji wetu nyota wana weza kutusaidia kufanikisha malengo yetu? Tukubali ukweli kwamba Tanzania tuna nyota wengi tu wa kisiasa au watu ambao wana utashi wa kuweza kuwa nyota wa kisiasa. Lakini sisi kama wapiga kura bado hatuja wawekea mazingira ya kushinda.
Kwa hiyo wakuu sisemi na wala sishauri tukate tamaa. 2010 bado haija isha. Ninavyo sema mimi ni kwamba hatuja jipanga vya kutosha na matokeo yoyote mwaka huu hayata tosha kuleta mabadiliko ya kudumu katika mfumo wetu wa kisiasa. Ila tusi kate tamaa na tusichoke. Tuji pange kwanzia sasa kwa ajili ya ushindi wa baadae. Tukumbuke kwamba ngo'mbe hanenepi siku ya mnada bali hushiba tu na kuvimbiwa. Mwaka huu ngo'mbe wetu haja nenepa bali tumefanya haraka haraka kumshibisha na kumvimbisha. Hali hii italeta mafanikio madogo kuliko tunayo taka na hayata kuwa ya kudumu. Tuji pange kwanzia sasa. 2015 si mbali!