2010: Pamoja Tunaweza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2010: Pamoja Tunaweza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Dec 31, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  HERI YA MWAKA MPYA: MWISHO wa mwaka ni wakati wa kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakotaka kwenda katika mwaka mpya. Ni kipindi muhimu kwa taasisi na hata watu binafsi kufanya tathmini na kujiwekea malengo. Kwa binadamu mmoja mmoja yanaweza kuwa ni malengo ya kiuchumi, kijamii na hata ya kisiasa.

  Maamuzi ya masuala ya kiuchumi na kijamii mara nyingi ni masuala binafsi. Hata hivyo, malengo ya kisiasa hususan yale yanayohusu utumishi wa umma ni muhimu kwa maamuzi yake kufanyika kwa kuzingatia mwelekeo wa kiongozi husika lakini pia kwa kurejea utashi wa wananchi iwe ni faraghani au hadharani.

  Hii ni kwa sababu uongozi wa umma wa kuchaguliwa hufanyika katika medani ya demokrasia ambayo inahusisha utawala wa watu kwa ajili ya watu.

  Katika uchaguzi yapo mambo manne ya muhimu katika kuhakikisha ushindi. Mosi, ni mgombea: haiba, wasifu na uwezo wake kwa ujumla. Pili ni ajenda: ujumbe wenye dira unawagusa wapiga kura na kuamsha kuungwa mkono.
  Tatu ni oganaizesheni: huu ni mtandao mzima wa kuratibu vuguvugu la ushindi, unaweza kuwa wa kijamii, kisiasa ama kitaasisi. Nne, rasilimali: hii ni kwa ajili ya kuwezesha kwa hali na mali kampeni husika, iwe ni fedha, zana, mawazo au nguvu kazi.

  Baadhi ya watu hudhani kwamba rasilimali ni jambo la kwanza kuwezesha ushindi, uzoefu wa kimataifa unadhihirisha kuwa katika kufanikisha kampeni za uchaguzi kipaumbele cha kwanza ni mgombea, cha pili ujumbe, cha tatu ni oganaizesheni.

  Rasilimali huongezeka kwa kadiri ya tija na ufanisi wa vipaumbele vitatu vinavyotangulia kwa nadra mtiririko huu unaweza kubadilika kutokana na upekee wa kimazingira ya kisiasa.

  Tumebakiza siku chache kuingia mwaka 2010, kipindi kingine cha kuelekea uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais nchini. Tayari heka heka zimeshaanza na kauli mbalimbali zimeshaanza kutolewa za kheri na za shari.

  Kwa kweli fikra kuhusu uchaguzi ujao zilishaanza toka 14 Desemba mwaka 2005 kwa wale wanaoamini kuwa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine.

  Binafsi nakumbuka mwaka huo wa 2005 wakati mjadala ukiendelea kuhusu utata wa matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Ubungo ambapo mimi nilikuwa mmoja wa wagombea tayari wadadisi wengine wameanza kuulizia masuala ya uchaguzi wa 2010.

  Hali hii ilijitokeza hata katika mkutano wangu na wanahabari Desemba 22, 2005 kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura na kuelezea mafanikio yaliyopatikana, mapungufu yaliyojitokeza na hatua ambazo nilipanga kuzichukua.

  Hata baada ya kutoa msimamo huo, bado mjadala uliendelea katika kipindi cha Januari mpaka Mei 2006; takribani nusu mwaka baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.

  Hivyo, baadhi ya masuala hayo niliwajibika kuyajibu kupitia hotuba yangu ya kuwashukuru wananchi na kuelekeza mwelekeo niliyohutubua jimboni Ubungo Mei 28, 2006.

  Ilinibidi niandike pia waraka kwa wananchi wa ubungo na watanzania Juni 4, 2006 wakati huo nikiwa ziarani nchini Marekani waraka ambao ulisambaa kwa umma kupitia vyombo vya habari na njia zingine za mawasiliano ya umma ikiwemo mikutano ya hadhara niliporejea. Waraka huo uliobeba ujumbe ‘kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi’ uliweza kutuliza kwa muda mjadala.

  Katika waraka huo nilielezea masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa azma ya kufungua kesi namba moja ya mwaka 2006 katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Ubungo.

  Kesi hiyo ambayo nilisimamiwa na Wakili Tundu Lissu ilipigwa danadana za kiufundi kipindi chote na kuishia hewani mwaka 2007 kwa kile kilichoelezwa na wakili wangu kuwa ni kukosekana kwa dhamira ya dhati ya kuisikiliza kesi hiyo.

  Hata hivyo, miaka takriban mitatu iliyopita ya 2006, 2007, 2008 na hata mwaka huu wa nne unaomalizika wa 2009, swali ambalo nimekuwa nikiulizwa ni kugombea ubunge wa jimbo la Ubungo 2010.

  Nimekuwa nikiulizwa swali hili katika mikutano ya hadhara ya kisiasa katika ziara ambazo tumekuwa tukizifanya katika kata zote za jimbo la Ubungo. Katika kipindi chote hicho swali hilo hilo limekuwa likiulizwa hata kwenye shughuli na matukio ya kijamii yawe ni ya kirafiki, kidini, misiba, harusi, michezo, miradi ya jumuiya, ufuatiliaji wa kero za wananchi nk.

  Wakati wote majibu yangu yamekuwa kati ya haya matatu nitajibu wakati muafaka ama umma utajibu ama Mungu akipenda! Najua katika kipindi chote majibu haya yamekuwa yakiwaweka katika mkanyiko waulizaji kwa sababu mbalimbali.

  Wapo wenye mtazamo kwamba majibu kama hayo ni ishara ya kutokuwa na uhakika ama kupima upepo. Wapo wenye imani kwamba kwenye uongozi wa kuchaguliwa sifa mojawapo ya uongozi ni kuutaka uongozi.

  Wapo ambao katika kipindi hicho hicho wamekwenda mbele zaidi kuweka msimamo wao bayana kwamba ni lazima nigombee tamko la wazi la hivi karibuni likiwa ni la mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Makoka na wananchi wa eneo hilo la Novemba 29, 2009. Msimamo huo waliutoa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi ambao walinialika kama mgeni rasmi.

  Kilichonisukuma kuandika makala hii ni majadiliano yanayoendelea hivi sasa kwenye mtandao kupitia www.facebook.com/john.mnyika kuhusu ‘Ubunge Ubungo 2010: Nigombee Nisigombee?’

  Wachangiaji wote waliotoa maoni yao mpaka sasa wamenitaka nigombee huku wakitoa sababu mbalimbali. Wapo waliotoa hoja ya kutambua uwezo, haja ya kubeba harakati za kizazi kipya kushiriki kwenye uongozi wa taifa letu, kufanya vizuri mwaka 2005 na kuhoji kuhusu mikakati ya kuhakikisha ushindi mwaka 2010.

  Mchangiaji mmoja alirejea mfano wa Barack Obama ambaye alikuwa na mashaka kuhusu kugombea kwake lakini mmoja wa washauri wake wa karibu akamweleza kwamba ‘usipogombea umechagua kushindwa; lakini ukigombea una chaguo la kushinda ama kushindwa’. Walatini wana msemo ‘Sauti ya watu ni sauti ya Mungu’. Si lengo la makala haya kujadili hoja mbalimbali ambazo zimetolewa katika mjadala huo.

  Naandika makala kuwezesha tafakari ya wengine ambao ni sehemu ya wapiga kura ama wananchi kwa ujumla hawana fursa ya kushiriki majadiliano kwenye tovuti.

  Tafakari pana zaidi tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; nini kinawasukuma wagombea kujitokeza kugombea: dhamira binafsi ama msukumo wa umma au vyote?

  Mwaka 2005 wakati huo nikiwa na miaka 24 nilipojitokeza kugombea kwa mara ya kwanza nilieleza kwamba ilikuwa ni dhamira yangu binafsi baada ya kuona nina kipawa/kipaji cha uongozi.

  Kusukumwa na dhamira ya ndani inaweza kuwa jambo la kawaida kwa mgombea ambaye utumishi wake bado haujaonekana kikamilifu mbele ya umma.

  Lakini vipi kwa mgombea ambaye anafahamika tayari: nguvu alizonazo, udhaifu alionao, fursa alizonazo na vikwazo vinavyomkabili, naye asukumwe na dhamira binafsi pekee?

  Kwa mgombea ambaye tayari anafahamika ni muhimu pamoja na dhamira yake binafsi pawe pia na msukumo wa umma hii ni kwa sababu nafasi za kuchaguliwa kama ubunge ni za kuwakilisha wananchi.

  Ni muhimu sehemu ya wananchi iwe ni wanachama wa chama, wapiga kura ama baadhi ya watu katika jumuia waone haja hiyo.
  Kuungwa mkono kwa namna hiyo katika dhamira ya kugombea na kuhusisha umma katika kufikia maamuzi nyeti kama hayo yanaweka msingi muhimu wa kuwa mwakilishi wa wananchi husika na hata kuwashirikisha wananchi katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.

  Kwa upande mwingine, kupanua wigo katika kufikia azma ya kugombea ni njia ya kuunganisha nguvu ya umma hata katika kampeni za uchaguzi. Katika siasa za ushindani ni muhimu harakati za uchaguzi zikaendeshwa katika mfumo wa vuguvugu hususan kwa wagombea wanaopitia vyama mbadala ambavyo havitegemei nguvu ya dola.

  Hivyo, ni muhimu kwa yoyote anayetaka fulani agombee katika eneo fulani, mosi, amtake kugombea kama sehemu ya msukumo wa umma. Pili, ajiunge na harakati za kufanikisha ushindi wake kwa hali na mali.

  Ushindani wa namna hiyo ulijidhihirisha nchini Marekani mwaka 2008 mpaka 2009 kwa wagombea kuungwa mkono na umma; kuanzia wakati wa kura za maoni za ndani ya vyama mpaka kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.
  Tunaweza kushiriki kuleta mabadiliko kwa kugombea na kuchaguliwa ama kwa kuchagua viongozi kwa kupiga kura. Ndio maana nachukua fursa hii kuwahimiza Watanzania ambao watakuwa na umri wa miaka 18 na kuendelea mwaka 2010 kutimiza wajibu huu wa kiraia.

  Hivyo, kwa wapiga kura wapya na wote ambao kwa sababu moja au nyingine hawana kadi za mpiga kura wajitokeze kujiandikisha kupitia uboreshaji wa daftari la kudumu unaoendelea ambao kwa upande wa Dar es salaam utafanyika mapema mwaka 2010.

  Izingatiwe kuwa hii ni awamu ya mwisho kabisa ya mchakato huo; kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba hivyo kukosa kujiandikisha ni kujikosesha haki ya kikatiba ya kuchagua kiongozi unayemtaka.

  Hata hivyo, izingatiwe kuwa kushiriki kuleta mabadiliko ni zaidi ya matukio ya kugombea ama kupiga kura ni pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa kuleta mabadiliko kwa njia mbalimbali. Mwito wa Mahatma Gandhi kuwa wakala wa mabadiliko unayotoka kuyaona’ unabeba dhana hii.
  Swali la kujiuliza, je wewe uko tayari kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona? Kama Ndio; je umeshawasiliana na chama ambacho unaamini ni chombo cha kuwezesha mabadiliko hayo na kuwaunga mkono viongozi hata ikiwa ni kwa kuwapa ushauri? Ama umeshashirikiana kwa hali na mali au walau kuwasiliana na mgombea mtarajiwa ambaye unaamini anaweza kupeperusha bendera ya kuongoza mabadiliko?

  Kugombea nafasi za kuchaguliwa zinazohusisha kuwakilisha umma hakupaswi kuwa suala la mtu binafsi. Matokeo ya kuwaachia wagombea binafsi ama vyama vyao pekee ni kuwa na viongozi ambao baada ya kuchaguliwa kwao kwa sababu waliingia kwa dhamira zao na wakafanya kampeni ‘kivyaovyao’; hawawajibiki kwa umma.

  Hivyo tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ni muhimu kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba suala la uongozi wa kuchaguliwa kuwakilisha umma ni wajibu wa pamoja.

  Ni wajibu wa yoyote anayetambua kwamba Mwenyezi Mungu ameijalia nchi yetu na watu wake rasilimali; iwe ni vipaji vyetu, kodi zetu ama maliasili: Hivyo tunawajibika kujenga taifa lenye kutoa fursa ya ustawi wa wananchi. Pamoja Tunaweza!

  Ni wajibu wa pamoja wa watumishi wa umma iwe ni walimu, polisi, wahudumu wa sekta ya afya n.k, ama wafanyakazi binafsi ambao wanataka mabadiliko kutoka katika mishahara midogo na mazingira magumu ya kazi, maslahi duni na kujenga taifa lenye kuthamini utaalamu. Pamoja Tunaweza!

  Ni wajibu wa wazazi, wanafunzi, wazee, wanawake na masikini kwa ujumla wenye kuathirika na kuongezeka kwa gharama za maisha na kuporomoka kwa huduma za kijamii nchini iwe ni elimu, afya, maji, mafao ya wastaafu na waotaka pawepo mifumo thabiti ya usalama na haki katika jamii ili kuepusha migogoro. Pamoja Tunaweza.

  Ni wajibu wa Watanzania wote wenye kukerwa na ufisadi unaolitafuna taifa huku hatua zinazostahili kushindwa kuchukuliwa kutokana na ufisadi kutapakaa katika mfumo mzima wa utawala na kuteteresha hata utawala wa sheria. Tufanye mabadiliko turejeshe uwajibikaji na maadili ya taifa. Pamoja Tunaweza!

  Ni wajibu wa matajiri na wenye fursa wanaoona hatari inayolinyemelea taifa kutokana na kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho, ukosefu wa ajira hususani kwa vijana nk ambayo ni mabomu ya wakati yenye athari vizazi hata vizazi yanayoweza kuepukwa kwa kuweka pembeni ubinafsi na kujali maendeleo ya sekta zinazogusa mustakabali wa waliopembezoni. Pamoja Tunaweza!

  Ni wajibu wa wapenda demokrasia wote wanaotambua kwamba hujuma za kwenye uchaguzi zinaweza kudhibitiwa kwa kuunganisha nguvu ya umma ikiwemo kwa kujenga vuguvugu thabiti la ulinzi wa kura. Pamoja Tunaweza!
  Tukumbuke; mabadiliko ya kweli katika taifa letu hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale. Kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema; Tanzania yenye neema haiwezekani. Tuunganishe nguvu kubadili mfumo wa utawala; mabadiliko yanawezekana.

  Tunahitaji uongozi wenye dira na uadilifu wa kulikomboa taifa; hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha viongozi tunaowahitaji wanashinda. Kwa maneno ya Mwalimu Nyerere jukumu la namna hii linaweza kutekelezwa kama kila mmoja akitimiza wajibu wake; umoja ni nguvu. Kidole kimoja hakivunji chawa; kuelekea uchaguzi mkuu 2010: pamoja tunaweza!

  Nimeitoa: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=11672
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli; ukisoma vema utaona kabisa mtu alifikiria ndio akaandika; thanks 2009; now 2010 more movements should be seen. Maelezo yanajisomesha wakubwa ni vema kuunga mkono hoja sasa
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I admire you Mnyika! Tungekuwa na vijana kumi (wengine wamo humu JF) wenye mtazamo kama wako, na kila mmoja akatafuta wengine kumi, na jumla ya wote wakapatikana wengine kumi kwa kila mmoja tungelijijengea hazina kubwa ya mabadiliko yanayohitajika nchini mwetu.

  Nakuombea ufike mbali katika uongozi wa taifa letu.
   
 4. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hongera bwana Mnyika kwa chapisho lako. Nami nichukue fursa hii kuwa miongoni mwa wale wanaopendekeza wewe ugombee tena ubunge katika jimbo la ubungo. Kwa kuwa wewe na bwana Mbowe mmekuwa role model wangu kisiasa, nami natangaza kuungana nanyi katika harakati za uchaguzi mwakani kwa kugombea ubunge katika jimbo mojawapo Iringa vijijini. Pamoja tunaweza.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Tatizo sicho hicho unachosema,
  tatizo ni tabia zako za kuwachimba wenzio kwa wivu.
   
 6. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #6
  Jan 1, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  The Boss

  Heri ya mwaka mpya!. Fafanua: Nani mwenye tabia hizo za kuwachimba wenzake kwa wivu? Anawachimba kivipi na kwa lipi? Mjadala uendelee


  JJ
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  The Boss!
  Ndo mwaka mpya unavyoanza hivi?
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Swali:

  Hivi huko CHADEMA kila mwanachama au kiongozi anapata airtime ya kutosha na kirahisi kujitangaza kama mdogo wangu John Mnyika anavyotumia website ya chama kwa masilahi binafsi?

  Kwa mtazamo wangu, hii ni aina nyingine ya ufisadi!
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jan 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..Mnyika akigombea Ubungo nampa kura yangu.

  ..this kid is talented, we need him in our Parliament.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180

  Lakini aache kuvaa magwanda.
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kids usually go to school not to parliament !!!
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Jan 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Kasheshe,

  ..but this kid is just too talented we should send him to the Parliament.

  ..nimetumia neno "kid" kwasababu nimemzidi kiumri kijana wetu John Mnyika.

  ..naamini anafanya kazi nzuri na ana uwezo wa kutusaidia na kukabiliana na changamoto za kuwa Mbunge.
   
 13. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu ni utani kazini. Kwani hizo nguo za kijani ambazo tumekuwa tukizichagua wakati wote zimeleta nini cha maana zaidi ya kuyazoea madaraka na kutuona watanzania wote ma zumbukuku?

  Mnyika keep on I always like this sayings:" Kwenye msafara wa mamba na kenge wamo" na kwa kuwa umepiga vizuri katika kuanza mwaka mpya sio rahisi mpinzani akakufurahia.

  Binafsi naazimia kwamba, mwaka 2010 siasa za kupenda sura ya mtu au chama kwangu zimepitwa na wakati na kwamba nitashiriki kampeni kwa kwenda mimi mwenyewe na kusikiliza nini kimekusudiwa na nitafuatilia kwa kiwango changu kura nilizompa mtu kwa mujibu wa ahadi alizonipa, kwamba mbona huendi sawa kwa mujibu wa ahadi katika kampeni zilizopelekea mimi kukupa kura yangu.

  As corrupt system started with single idea, even clean society can start by you, let us together escape the type of politics which will always make our country laged behind all the time. The promised country is on your own hands.
   
 14. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Kaka hata wakati Mussa wakati anawatoa wana wa
  Israel kule utumwani kuwapeleka kwenye nchi yao ya ahadi yalikuwepo majitu mengine yaligoma - yakawa mabishi sana hasa walipofika jangwani sehemu hakuna maji wala chakula yakataka kuruki kule kule utumwani.

  Usijali Mkuu tutafika tu, mi namkubali dogo ametulia kisana - nampa tano.
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tutafika kwa gari ipi? ya CHADEMA?
   
 16. b

  bigilankana Senior Member

  #16
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwaka 2005 uligombea ukiwa umehitimu kidato cha sita. Mwaka 2010 bado elimu yako ni hiyo hiyo ya kidato cha sita. Ubungo watakuuliza umeshindwa kumaliza shule yako mwenyewe utawezaje kuleta maendeleo?Mwenzio Nape alikwenda kusoma India baada tu ya uchaguzi. wewe na chadema tu
   
 17. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakutakia kila la kheri Mnyika katika azma yako ya kugombea ubunge kwa mara nyingine tena.

  Naamini sasa unafahamu kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kupigiwa makofi, kushangiliwa na kushinda uchaguzi. Hii nimeiona katika maelezo yako hapo juu. Unachohitaji kikubwa ni watu wenye kuweza kufanikisha ushindi wako, wenye nia thabiti ya kukuhakikishia support na wanaojua jinsi ya kutafuta kura. Chambua mchele kwa kutoa pumba. Utafanikiwa.

  Usijali sana yanayosemwa na watu wenye nia ya kukurudisha nyuma. Ni haki yako kama ilivyo ya mwingine yeyote kuomba wananchi wamchague. Ushindi haulazimishwi.

  Nakuombea nguvu, hekima, uvumilivu na ujasiri wa kufanya yote yanayohitajika katika kutimiza azma yako.

  Heri ya Mwaka Mpya.
   
 18. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  angalieni pia nyoka mnaowafuga nyumbani,mbebeba waliomo na wasiokuwamo...............
   
 19. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #19
  Jan 11, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Na Salim Said

  SIKU mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaonya mabalozi wasijihusishe na chama chochote cha siasa katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba, baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema, kauli hiyo ni nzito na kwamba kama hataki wajihusihe na siasa nchini aache kupokea misaada yao.

  Akizungumza katika hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya na mabalozi kutoka nchi mbalimbali jijini Dar es Salaam juzi, Rais Kikwete alisema kitendo chochote cha mabalozi hao kushabikia chama kitashughulikiwa vema na serikali yake.

  Lakini kwa nyakati tofauti jana viongozi wa vyama vya upinzani, walisema serikali haina haki ya kukataza mabalozi kujihusisha na siasa endapo watabaini misaada wanayoitoa inatumika 'kubaka' demokrasia nchini.

  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Hamad Rashid Mohammed alisema hakuna balozi yeyote anayeingilia mambo ya ndani ya nchi bila ya kushirikishwa na serikali.

  Alisema serikali inawashirikisha mabalozi mbalimbali na nchi zao katika masuala mbalimbali ya siasa nchini, kupitia misaada yao na kifedha na kiufundi katika miradi mbalimbali ya kuboresha demokrasia na utawala bora.

  "Kauli ya rais Kikwete ni nzito na hii ni kwa sababu anajua kitakachotokea ndio maana anajihami mapema kwa kutoa onyo na vitisho kama silaha dhidi ya mabalozi.

  "Vyama vya upinzani vinapaswa kuitafakari kauli ya Kikwete kwa makini. Kwetu sisi tafsiri ya kauli yake ni kwamba mwaka huu hakuna uchaguzi huru na haki, kwa sababu kama upo uchaguzi huru na wa haki tungeona rais akiwaalika mabalozi kuangalia demokrasia, badala ya kuwatisha," aliongeza Rashid.

  Rashid ambaye ni mbunge wa Wawi Pemba (CUF), alisisitiza kuwa, "kama rais Kikwete hataki mabalozi wajihusishe na siasa nchini, basi asipokee wala kuomba misaada yao, kwa kuwa mabalozi hawataweza kukaa kimya iwapo wataona fedha za walipakodi wao zinatumiwa vibaya."

  Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chadema John Mnyika, alisema anasikitishwa na hotuba ya rais Kikwete kwa mabalozi, ambayo ilikuwa ya vitisho badala ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa mambo aliyowaahidi mwaka 2006 alipokutana nao.

  "Rais aliwaahidi mabalozi mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwanja wa siasa nchini, lakini inasikitisha kwani badala ya kuwapa taarifa ya utekelezaji wa ahadi hizo, anawatisha," alisema Mnyika.

  Mnyika alisema katika mkataba wa Viena kuna vifungu vinavyokataza mabalozi kuingilia mambo ya ndani ya nchi na kuhatarisha usalama wa nchi, lakini vifungu hivyo vimepotoshwa na Rais Kikwete pamoja na waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe.

  Alisema serikali ilikaa meza moja na mabalozi na kuanzisha mradi wa 'kapu la pamoja' kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za kuendeleza demokrasia nchini, sambamba na Mradi wa Kuimarisha Demokrasia (DDP) wa Umoja wa Matifa (UN).

  "Kwa sheria za nchi za mabalozi, wanapotoa fedha za walipakodi wao, hutakiwa kufuatilia matumizi yake kama zinatumika vizuri au zinatumika kubaka demokrasia ya Africa,"alisema Mnyika.

  "Sasa kama rais Kikwete anawaonya mabalozi kujihusisha na siasa nchini, basi aache safari za nje kila siku kwenda kuomba misaada yao, ambayo inatokana na fedha za walipakodi wao," alisema Mnyika.

  Alisema katika dunia ya sasa suala la kuheshimu mikataba ya kimataifa na kuacha serikali ya nchi ikikiuka na kupora haki za binadamu, limepitwa na wakati.

  Alisema hali hiyo ndio imesababisha mabalozi na mashirika ya kimataifa kutoa matamko mbalimbali ya kutaka kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar al Bashir kwa sababu amevunja haki za binadam.

  Aliziomba jumuiya hizo na mabalozi kupitia mswada wa sheria ya uchaguzi na ule wa sheria ya matumizi ya fedha katika uchaguzi na kuitolea matamko, kwa kuwa serikali itafanikiwa kuipitisha, itakuwa kaburi la demokrasia nchini.

  Mwenyekiti mstaafu wa Chadema Bob Makani alisema onyo la rais Kikwete litakuwa ni sahihi endapo litakua na maana ya mabalozi kutowachagulia watanzania viongozi.

  "Kwa mimi onyo lake, ni sahihi endapo linalenga katika mtazamo wa mabalozi hao kutowatuchagulia wananchi viongozi, wasituchagulie wabunge wala rais wawaachie watanzania kufanya maamuzi yao wenyewe kuhusu viongozi wao,"alisema Makani.


  Chanzo: Mwananchi
   
 20. M

  Mundu JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  duh, hii ni kali, ni sawa na mbwa kumbwakia/kutishia kumng'ata tajiri yake. Kikubwa atakachomfanyia ni kumnyima chakula, afu atabaki kuwa mbwa koko.
   
Loading...