1st Anniversary: JF Assault | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

1st Anniversary: JF Assault

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Feb 5, 2009.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mwezi February mwaka 2008 nikiwa Jijini Mwanza nilipata habari za kushtusha na kushangaza kuhusu JF. Wakati nikiwa Arusha nilijaribu ku-access JF lakini bila mafanikio na nikadhani kuwa huenda ni matatizo ya mandao.

  Jioni moja nikiwa Jijini Mwanza nikiwa nasikiliza BBC Dira ya Dunia nikapata habari kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia Wamiliki wa mtandao wa Kompyuta wa JF! BBC kupitia Abdalla Majura walimhoji Kamanda wa Polisi Dar na akathibitisha hilo na pia alimhoji Mwanakijiji kama mdau wa JF. Naamini kabisa Polisi walitumika kama silaha ya ukandamizaji wa maoni huru na ilikuwa ni njia ya kuwatinsha ndugu zetu ambao wameifanya JF kuwa mahali pekee pa WaTZ kutoa maoni yao kwa uhuru mkubwa.

  JF imekuwa ni kisima cha habari na ni Jukwaa hili ndilo liliotumika mwanzo kabisa kuanika uozo wa Kifisadi wa EPA pamoja na vitisho kutoka kwa Wakili wa Jeetu huko Uingereza. Naamini kuwa Jeshi la Polisi lilitumika Kifisadi na Mafisadi ili kuwalinda Mafisadi dhidi ya Ushahidi uliokuwa ukianikwa dhidi yao kupitia Mtandao wa JF.

  Inasemekana kuwa Polisi waliwashikilia ndugu zetu hao (Wa JF) na kuwahoji kwa muda mrefu; kwa tabia ya Polisi wetu sidhani kama Wamiliki na Waendeshaji wa JF waliojikuta mikononi mwa Polisi waliepuka mateso ya kimwili ukiondoa ya kiakili maana Polisi wetu ni mahiri katika kutoa adhabu za vipigo kwa Watuhumiwa.

  Kwa bahati mbaya sana Ndugu zetu hao waliopitia madhira hayo ya Polisi hawajawahi kutueleza wanachama wao juu ya madhira waliyopata wakiwa mikononi mwa Polisi na nawaomba watuleleze kinagaubaga juu ya kilichojiri walipokuwa mikononi mwa Polisi. Walihojiwa nini, na tuhuma zilikuwa nini na je, kulikuwa na mateso yoyote?

  Kwa bahati mabaya mbinu waliyotumia Mafisadi ya kuwakamata ndugu zetu ilizidisha mara dufu umaarufu wa JF na kila Mtanzania aliyesikia habari ile alitaka kujua JF ni kitu gani na si ajabu kuona idadi ya Wananchama inazidi kuongezeka kila siku na namwomba Mod awe anatupa updates kila mwezi juu ya idadi ya wanachama.

  Mwisho. Pamoja na jitihada zilizofanywa na Mafisadi kupitia Jeshi la Polisi kuwanyamazisha ndugu zetu bado JF inaendelea kukua kila kukicha na natoa wito kwa wnachama wote kuendelea ku-share na Watanzania wengine juu ya Jukwaa hili la JF. Pia napenda kuwaomba wanachama wote wa JF kuiunga mkono JF kwa hali na mali-tutoe michango ya fedha kwani akaunti zote zimeshawekwa kwenye Mtandao, KUMBUKENI JF ndiyo silaha yetu Watanzania tuliopata bahati ya kuangaziwa na nuru ya elimu.

  Wakatabahu,
  Ibrah
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Aha kumbe
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kumbe nini???
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kumbe ilikuwa hivi
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  U never cease to astonish me!
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kwamba ulikuwa hujui ama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dogo ndo alipeleka uzushi police washikaji wakakamatwa.....Shy
   
 8. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Shy, mbona hujibu? Wewe ndiye uliyesababisha Washikaji wetu wadakwe na Polisi? Are you the one?
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Feb 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ibrah, kwanza niseme umefanya vema kuleta hili hapa.

  Ni mwaka umepita, na nadhani muda si mrefu (kwa taarifa nilizo nazo) kutatokea kama kilichotokea mwaka jana... Am well informed over that.

  Ni vigumu kueleza kwa sasa mpaka muone, ila kipo kinakuja.

  Kama si watatu basi wanne, nao wanaonewa tu. Si wao, ni watanzania. Nadhani kama kamatakamata hii ingefanywa kwa watanzania walau asilimia 50 hivi ambao wanakuwa na mawazo tofauti na wanavyotaka wenye nchi.

  Haijalishi kuwa mtanzania anakupigia kura ukiwa CCM ama CHADEMA au TLP, lakini hamwezi kufanana mitizamo, ni vema tukubali challenges, ni vyema tujifunze kutokana na yanayojiri (endapo hakuna matusi ya wazi na udhalilishaji usiokubalika mbele ya jamii).

  Mimi nipo, naangalia tu...

  Kuhusu stats za JF; nilifikiria kufanya hivyo Januari mwaka huu nikasita... Ndio mwezi ambao JF ilipata hits kuliko kipindi chote... 18mil hits (January Only).

  Nawashukuru watanzania kwa ushirikiano wenu, na namna mnavyoshirikishana mambo kadha wa kadha kwa kupitia JF. JF itasimama imara pamoja na yote yanayoikabili kwani ndiyo Jamii yetu!

  Invisible (Real One)
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ni vema wakumbuke kuwa jinsi wanavyotumia nguvu nyingi kunyamazisha watu ndivyo upinzani dhidi yao unazidi kuwa mkubwa. Wakifanikiwa kukunyamazisha wewe wataibuka wengine mamia ambao watafanya yaleyale waisyoyataka.

  Mungu Ibariki JF, Aluta Continua, Mapambano yanaendelea na Mafisadi watashindwa. JF itaendelea kuwa njia ya kumkoma Nyani na Evidence zikipatikana zitaanikwa kama kawa.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Feb 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ah, wewe waninyamazishe kwani nimeongea? Labda wawanyamazishe watanzania (nyote mnaoitembelea JF kwa kuwa mmeongea).

  Invisible (Real One)
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Yap, hii nimeipenda sana! Tuongezee hii Invisible the Ghost.
  Who can touch the ghost now? Kama ni hivyo: kwisha habari yao!
   
 13. G

  Guantanamo Bay Member

  #13
  Feb 6, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mungu ibariki Jf
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Bandugu, hivi mwajua kuwa JF iko hatarini? Invisible, hebu tujuze wanachama wako kama kuna jambo tunaweza kufanya ili JF isalimie. Je, ni michango kwa ajili ya kuweka Wakili pindi watakapofanya kama mwaka jana? Au tusiwe na wasiwasi mambo yako na yataendelea kuwa shwari?
   
 15. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145

  Mzee ni vipi tena?Naelewa unaposema wawili watatu.... lakini pia hao wanaokamata nao wengi si ni wanachama hapa?......You know what I mean
   
 16. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wafilie mbali hao. Yaani sisi tunalala vichwa vinauma jamii inaangamia na tunajitahidi kuleta maoni halafu wanataka kukamata au kuua JF. Atakayewaza kunyamazisha JF na afe tena afe na afe tena fiiiiiii. Sijawahi kupata forum ambayo inanielimisha kama hii. Atakeyetushika basi anatuogopa. Wasiwasi wao wa nini??? Wangekuwa waadilifu katika utendaji wao wala hatungepata cha kuchangia humu. Hii JF siyo forums za udaku bali ni jukwaa la maendeleo where we dare to talk openly. Watakapoacha ufisadi na rushwa zao na sisi tutawaacha na tutaweka tu mambo ya burudhani.
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Bado nakumbuka manumba na kauli zake......nilijiuliza hivi yule ni DCI na ni mtu mzima anatamka maneno yale.....eti JF ni mtandao wa kigaidi......JF haifi na itadumu....
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,575
  Likes Received: 18,491
  Trophy Points: 280
  Udumu Invisible!,
  Udumu Maxene Melo!
  Wadumu Wanachama Waanzilishi wa JF!.
  Wadumu Wana JF wote!
  Idumu JF!.
  Mungu Ibariki JF.
  Mungu Ibariki Tanzania.
  Aluta Continua!.
  inua.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sikuijua JF mpaka siku serikali ilipojaribu kuizima JF mwanzoni mwa mwaka jana - hicho kitendo ama jaribio la serikali kilizaa neema kubwa kwangu. Kwa mara ya kwanza nilifarijika kujua kuwa sikuwa peke yangu katika kusononeka kila nilipofikiria uongozi na hatma ya nchi yangu niliyoipenda. Kama lengo la serikali ilikuwa ni kuidhoofisha JF, basi ilishindwa na uongozi wake ulionyesha udhaifu mkubwa wa kukurupuka bila mpangilio -ila safari hii kukurupuka kwao kulileta faraja tele.

  Leo naweza nikasema kwa kujiamini kuwa serikali imeipa, inaipa na itaendelea kuipa umaarufu JF kama itandeleza vitendo kama hivyo vya kijinga. Binafsi nawashukuru na kuwapongeza mzalendo/wazalendo waliokaa chini wakabuni hili jukwaa lisilo mfano wake - vizazi kwa vizazi vitawakumbuka kwa huo ujasiri wenu. Nachukua nafasi hii kuwaomba wanachama wote kila moja kwa wakati wake kuutambua mchango wa hawa wazalendo na tufikirie tuzo tunaloweza kuwapa.

  Idumu JF mpaka Tanzania itakaporejesha hadhi yake si Afrika tu bali kote duniani. Tumedanganywa, tumenyanyaswa, tumedharauliwa, tumetukanwa na tumeibiwa vya kutosha na sasa JF twasema basi. Atakayedharau nguvu ya JF, atakayefikiria kuinyamazisha JF na atakayedhani moto uliowashwa na JF utazimika, anaota ndoto kama Idi Amin aliyeamini anaweza kuitwaa sehemu ya Tz na akabaki madarakani - alikuja kuikimbia nchi yake bila kuaga.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,195
  Trophy Points: 280
  We have something very special kinachotuunganisha Watanzania ndani na nje ya nchi bila kujali dini zetu, rangi zetu na itikadi zetu za kisiasa. Tuienzi, tuidumishe na tuisadie JF kwa hali na mali. Tusiifanye JF sehemu ya kujenga uhasama na uadui kati yetu, kutokubaliana katika mijadala mbali mbali hapa ukumbini ni kitu cha kawaida kabisa, lakini tunaweza kutokubaliana kistaarabu bila kutumia matusi wala kejeli.

  Katika baadhi ya mijadala hapa ukumbini nimewahi kutumia lugha ambazo nazijutia maana sikujiunga JF ili kujenga uhasama, uadui au kutumia lugha ambayo si ya kiungwana lakini kuanzia sasa nitajitahidi kutotumia tena lugha ambayo kwa maoni yangu haistahili hata kidogo nawaomba wanachama wengine mjitahidi hata kama mna tofauti katika majadiliano kutumia lugha ambazo zinakubalika.

  Mungu ibariki Tanzania na JF
   
Loading...