KELVIN GASPER
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 1,066
- 454
Mwalimu nyerere wakati anaongea na wazee wa mkoa wa dar es salaam mwaka 1978 aliwaeleza kuwa serikali ya somalia ndio iliyosuluhisha mgogoro uliokuwepo kati ya tanzania na uganda. anaendelea kuwa hali ilikuwa ni tete kwani nchi zote mbili zilishasogeza majeshi hadi mpakani tayari kwa vita. ilifikiwa makubaliano kuwa majeshi pande zote mbili yarudishwe nyuma kilometa kumi kwa kila upande wa mpaka. Mwalimu Nyerere anadai kuwa wakuwahi hata siku moja kumpenda Idd Amini kwani nae alikuwa ni muuaji kama wazungu waliokuwa wanatawala zimbabwe na afrika kusini. Alishangazwa sana na baadhi ya viongozi wa afrika kumshabikia Amin eti kwa sababu tu aliwafukuza wahindi uganda. ilimkera sana kitendo cha viongozi wa afrika kumpa uenyekiti wa OAU Amin na Uganda kuwa mwenyeji wa kikao cha OAU kwa wakati huo.sikuamini kwani wengi tulio katika kikazi hiki tumeikuta somalia imeshaparaghanyika kumbe wenzenu enzi hizo walikuwa wako sawa hadi wanasuluhisha migogoro ya nchi majirani zao.