SoC03 Mgogoro kati ya China na Marekani utakavyoiathiri Afrika(1)

Stories of Change - 2023 Competition

Ricky Mas

New Member
Aug 1, 2022
1
0
Tarehe ni 20 Februari,2023. Majeshi ya urusi yanaivamia Ukraini, moja ya nchi zilizounda umoja wa kisosholisti wa kisoviet (USSR).

Vita hii ilikamikisha utabiri wa wanasiasa wengi kutoka magharibi juu ya Vladmir Putin kiongozi wa nchi ya Russia na matamanio yake ya kuvamia na kidhibiti hata kwa nguvub katika eneo la baltiki lililopo ulaya ya kati zikiwemo nchi kama Latvia, Lithuania, Estonia na kadhalika.

Wanazuoni wengi wanaamini kuwa hii ndiyo vita kubwa amabayo huenda ikapelekea kuwa na vita kuu ya Dunia. Lakini kuna vita baridi ambayo inaweza kutupeleka katika vita kuu ya tatu ya dunia (VV3) nayo ni vita ya chinichini kati ya Marekani na China.

Kimsingi vita baridi ni vita isiyo na matumizi ya silaha za moto, bali hutumia njia za uchokozi,udukuzi,ujasusi na uhujumu wa vitu mbalimbali vya nchiadui ili kupumguza nguvu yake ya kukilinda au kujihami.

Wataalamu wa masomo ya kimkakati na kijeshi wanaamini kuwa chokochoko hizi kati ya China na Marekani ni vita ya baridi 2.0 ambayo itaweza kuathiri namna dunia itakavyokiwa katika karne hii ya 21.

Katika sehemu hii tutaangalia chanzo cha uhasama kati ya China na Marekani, uhusiano kati ya vita baridi 2.0(VB2.0) na vita kati ya urusi na ukraini na mwisho tutaangalia athari kwa Afrika hasa kwa nchi ya Tanzania .

CHINA VS MAREKANI;VITA YA BARIDI 2.0?
Vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC, WION, FRANCE 24 na kadhalika vimeweza kutuletea swala la hili katika mlengwa wa kimagharibi. Vita hii ilishika kasi sana wakati wa janga la uviko-19 mwaka 2020. Lakini uhudiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani katika dunia ya sasa ulianza mwaka Julai,1971 pale mabpo China iilikuwa chini ya itikadi za kikomunisti za Mao Ze Dong ambaye alifariki mnamo 9 septemba,1976.

Mkutano huu ulikuwa wa siri ambapo Marekani, mama wa demokrasia na ubepari katika upande wa Magharibi , ilikutana na Mkomunisti Mao. Tofauti kati ya itikadi na falsafa za kibepari na kikomunisti ( kisosholisti/ kiujamaa) ilikuwa ni moja wwpo ya sababu ya huu mkutano kuwa siri lakini sababu nyingine ilikuwa muhimu zaidi , na sabau hio ilikuwa ni umoja wa kisovieti wa Urusi.

Mnamo mwaka 1969 china na urusi ziliingia katika mzozo ambao ulipelekea mapigano kati ya walinda mipaka ya china na urusi hali hii ilitengeneza ufa katika upande wa mashariki ambapo nchi kubwa mbili ( china na urusi) hazikuelewana wenyewe kwa wenyewe hivyo Marekani akapata nafasi ya kukutana na China ili kuongeza ufa na kubomoa ukuta wa kikomunisti.

Mkutano huu wa maka 1971 ni wa siri kati ya katibu mkuu wa Marekani ( secretary of state ) Henry kissinger na Mai Zedong uliifungua mahusiano rasmi kati ya China na Marekani na kutengeneza njia ambayo China iliichukua baada ya anguko la ujamaa/ ukomunisti mwaka 1989.

Hivyo China ilikuwa rafiki wa Marekani , kwa mwanzo wa miaka ya 2000na kuendelea . Lakini hali ilibadilika baada ya China kukua kwa haraka sana kiuchumi miaka ya tisini na kutishia kuwa uchumi wa nguvu zaidi kuliko hata Marekani.

Hivyo Madekani ikaanza uhasama upya, kwa sasa kwa kutumia uchumi na kidiplomasia , hali ambayo imeweza kudhihirika miaka hii ya karibuni hata majeshi ya Marekani kuanza kutambiana na la China.

Kiuchumi, marekani na china zimeweza kujieneza katika dunia huku zikishandana katika kila nyanja , hasa za Uchumi wa kidijitali na uwekezaji pia. Hapa ndipo Afrika inapokuja katika mwangaza wa hizi nchi mbili kubwa kiuchumi .

Na sasa tuangalie jinsi gani mataifa haya yameweza kuwekeza katika Afrika na sehemu nyingine duniani na jinsi walivyotengeneza mandhari mahususi ya kuleta kutokea kwa vita ya urusi na ukraini .

UHUSIANO KATI YA VB2.0 NA VITA KATI YA URUSI NA UKRAINI
Tarehe ni 31Julai, 2023 na bado vita inaendelea kati ya Urusi na Ulraini . Lakini swali la kujiuliza ni kwanini Vladmir Putin ameamua baada ya karibia miaka 30 tangu anguko la kisovieti , kuwavamia nchi jirani ya ukraini na jinsi marekani vs china inavyoingiliana na vita hii.

VB2.0 imeingia kwenye hatua za juu kabisa kama ilivyo kwa mgogoro wa makombora wa Cuba miaka ile ya 1962. Leo hii mgogoro huo umejitokeza katika mgogoro juu ya Taiwan , kisiwa kidogo chenye historia ambayo china inatamani kuifuta historia ndefu ya China.

Marekani inaamini kuwa katika kusapoti nchi zilizoko kwenye himaya yake kiuchumi. Lakini umuhimu wa sapoti hiyo unakuja na ulazima wa nchi hizo kufuata masharti ya Marekani bila kuuliza na bila kuzingatia maoni yao wenyewe.

Mfumi wa Marekani wa kuongoza himaya yake kupitia uchumi ni kupita dola za kimarekani. Hii ni kwa kuifanya dola ya kimarekani kuwa ndio kipimo cha kubadilishia fedha na kufanya biashara duniani na kuiacha ile ya kutumia dhahabu ambayo ilikuwa ndio ilikuwa ikitumika kabla ya 1973. Hatua hii iliifanya dola za kimarekani kuwa silaha yenye nguvu zaidi katika ghala la silaha za Marekani.

Hivyo katika Afrika , nchi nyingi hupokea misaada katija dola za Kimarekani, hununua na kuuza kwa kutumia dola za Kimarekani hivyo kupunguza nguvu kwa pesa za Kiafrika mfano Zimbabwe na Sudani kusini. Hali hii huipa nguvu Marekani aghalabu katika kuipa nguvu ya kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa nchi zingine ambazo haziendani na matakwa yake.

Mfano Jamhuri ya kiislamu ya Irani na utusi ni nchi zilizowekewa vikwazo vya kiuchumi vingi katika miaka hii ya karibunib.

Hivyo ndivyo Marekani hutengenza himaya yake. Ata umoja wa ulaya (EU) nao wanamtumikia Marekani ambapo waliweza kuamrishwa kutonunua gesi na mafuta ya Russia wakati wa vita vya Urusi na Ukraini kwa vikwazo vilivyoshinikwiza na Marekani. Lakini pale ambapo msimu wa baridi kali ulipoanza, walishindwa kufanya maamuzi hayo kwa kuhofia Marekani japo walibadilisha sera na kuweka bei ya chini ya kununua mafuta hayo kutoka kwa urusi .

Hivyo ata mataifa ya Afrika kama Tanzania hupewa mikopo yenye masharti yanayotaka kuiumba Tanzania kwa sura na mfano wake. Hivyo ndivyo Marekani hupata nguvu katika himaya yake.

China kwa upande wake hutumia njia ya 带 路 , (Belt and road initiative)
Hii iko chini ya mpango wa 2045 ambapo China inajiona kuwa nchi yenye nguvu zaidi duniani. Na moango huo umeundiwa sera ya BRI, belt and road initiative .

BRI inahusisha China kutoa mikopo ya masharti nafuu amabayo ambayo huitoa kwa nchi ambazo hazitakuwa na nguvu ya kiuchumi kama nchi za Afrika. Mikopo hii huingia katika ujenzi wa miundombinu kama viwanja wya ndege , bandari, barabara na hata kujenga madaraja.

Mikopo huwa inapendwa kwasababu ni ya bei chee na masharti ya kawaida hivyo huweza kutoathiri uhuru wa nchi hiyo lakini huwa na kipengrle cha kuruhusu makampuni ya China kuleta wafanyakazi wa kichina lakini pia kama hawatalipwa, aghalabu hutokea mara nyingi , China huweza kuichukua na hata kuifanya ikawa na matumizi ya kijeshi .

Hivyo China imehenga miundombinu katika sehemu nyingi kama Tanzania , Kenya na hata Djibouti .Hivyo China hutengeneza himaya yake kutumia mikopo ya bei nafuu na kifungu cha kuzichukua na kuzimiliki kutika kwa nchi iliyosaidiwa. Mfano mzuri ni nchi kama Zambia ambayo uwanja wwke wa ndege wa Lusaka umechukuliwa na China ,hivyo kupelekea nchi za magharibi kukodolea macho china na kuiangalia kwa jicho la tatu.

Hivyo Marekani kuisapoti ukraini huenda ikawa ni hali ya kuivuta china kumsapoti Urusi na hata kuwaingiza katika vita hii ya sasa. Putin huenda alikuwa na uhakika wa kuwa hata atakapoingia katika vita hii China atamsapoti katika steji ya kimataifa .

Na hivyo china ilifanikiwa kufanya hivyo pale ambapo nchi kama Tanzania , Uganda, nchi za visiwa za pasifiki zilikataa kuisapoti ukraini. Hii inaweza kuonekana kwamba nchi hizi hazikutaka kujihusisha katika mzozo huo lakini hii ilikuwa ni ushindi kwa China na Urusi kwani kwa kupitia BRI China iliweza kishawishi nchi kutokuwa na upande wa Ukraini amabayo Marekani walikuwepo na afadhali kukataa kusapoti nchi za magharibi kuliko kuwaunga mkono. Hali hii ilitengenza tena dunia yenye makundi mawili makubwa ya kijiopolitikia , magharibi na upande mwingine wa China yaani , Mashariki.

Hivyo kupitia vita hii ya ukraini na Urusi , kunaletea dunia pande mbili zisizo na utofauti katika falsafa za uzalishaji na siasa lakini tofauti katika hali ya uchumi na nguvu katika Dunia hii ya sasa . Hivyo basi, vita vya ukraini na urusi ni uaandaji wa pande mbili ili kupigana katika vita vya bahari ya china kusini katika visiwa vya Taiwan

ATHATRI ZA VITA BARIDI KWA AFRIKA
Mataifa ya Kiafrika yanaingia katika mzozo huu katika ukurasa mpya na kitabu kipya katika historia ya Afrika. nchi nyingi zilikataa kuunga mkono upande wa magharibi.

Hii itaiathiri Afrika kiuchumi , kisiasa na hata kijamii. Mataifa mengi ya kiafrika yanasukuma kuchagua upande na hivyo tunaelekea kuwa lulu kwa mataifa makubwa. Hivyo ile “scramble” na “partition “ ya Afrika kwa mara ya pili inarudi na inashika kasi sana kwa sasa .

Viongozi wa nchi kubwa kama Marekani Uingerza, Ujerumani, Ubelgiji ,Uholanzi na Urusi huanza ziara kuja kujinadi na kupata sapoti kutoka kwa nchi za kiafrika hali hata kumgeuka China na kukata diplomasia nayo.

Kutamatisha , Afrika inahitaji kuchagua upande sahihi. Upande utakaoruhusu Afrika kujijenga kwa kutumia haliya kisiasa ya Dunia, kwani vita ya mbali huweza kutuathiri pia kiuchumi ,kisiasa na hata kwa malengo yetu ya baadaye.

Ni muda wa Afrika kufanya uamuzi na kuuusimamia bika kuwa na shinikizo kutoka kwa magharibi au mashariki.

Kila bara huweza kuleta nchi yenye nguvu zaidi duniani kasoro Afrika hivyo kuna uhitaji wa kuleta Afrika katika viwango vya juu kabisa katija historia ya Dunia
 
Back
Top Bottom