17 Marhkila mwaka ni siku muhimu kwa Watanzania kukumbuka kifo cha Hayati Magufuli

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,159
11,474
Pamoja na kwamba taifa letu limewahi kuwa na viongozi katika ngazi ya Urais ambao wameishatangulia mbele ya haki! Kikatiba kumbukizi linalopelekea siku ya mapumziko ni kwa waasisi wa taifa letu (Nyerere & Karume).

Hata hivyo siku ya tarehe 17 March kila mwaka, ni siku ya majonzi kwa watanzania walio wengi! Mimi binafsi bado nikimtafakari natokwa na machozi kwa uzalendo na bidii ya kulitoa taifa hili kutoka katika makucha ya mafisadi, majangili, wabadhilifu, n.k.

Alionyesha kwa vitengo ndani ya muhula mmoja alileta mapinduzi makubwa kiuchumi, kijamii, kiteknologia, kiulinzi, kiafya, kielimu, kijamii, n.k.

Je! Wewe unamkumbukaje JPM?
 
Pamoja na kwamba taifa letu limewahi kuwa na viongozi katika ngazi ya Urais ambao wameishatangulia mbele ya haki! Kikatiba kumbukizi linalopelekea siku ya mapumziko ni kwa waasisi wa taifa letu (Nyerere & Karume). Hata hivyo siku ya tarehe 17 March kila mwaka, ni siku ya majonzi kwa watanzania walio wengi! Mimi binafsi bado nikimtafakari natokwa na machozi kwa uzalendo na bidii la kulitoa taifa hili kutoka katika makucha ya mafisadi, majangili, wabadhilifu, n.k. Alionyesha kwa vitengo ndani ya mwaka mmoja alileta mapinduzi makubwa kiuchumi, kijamii, kiteknologia, kiulinzi, kiafya, kielimu, kijamii, n.k. Je! Wewe unamkumbukaje JPM?
 
Kwa mimi binafsi naamini ndiye Rais aliyeirudiaha nyuma zaidi Tanzania kwenye uwazi na ukweli, nakumbuka walitunga sheria bungeni na yeye mwenyewe akaisaini iliyokuwa ikitaka kila utafiti unaofanywa nchi na taasisi mbalimbali upitie serikali I kwa ukaguzi kwanza kabla ya kuifikia hadhara, wakati wake ndipo ililetwa miswada ya mabadiliko ya sheria ya habari ambayo ni dhahiri ililenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

Ni wakati wa Magufuli huyohuyo ambapo ripoti ya CAG ilionyesha kulikuwa na ubadhilifu mkubwa sana wa mali za umma, ni wakati wake ndipo watu waliokotwa baharini huko wakiwa wamefungwa kwenye mifuko ya sandarusi (Maiti) watu wakatekwa na kupotezwa, wengine wakapigwa risasi na mamlaka zikanyamaza hadi leo hii, Demokrasia na uhuru wa maoni ulididmia kiasi ambacho tulirudi nyuma miaka 30, Alikuwa mtu wa hovyo kuwahi kutokea na ndiye alisababisha zao hili tulilonalo sasa na tutatumia miaka mingi sana kufuta makovu ya unyama alioutenda jiwe.
 
Back
Top Bottom