15% ya Bodi ya Mikopo; Sheria inasemaje?

bface

Senior Member
Dec 22, 2010
128
19
Mtaani huku ni soo watu 15% ndo habari ya mjini, lakini mimi nilitaka kidogo wanasheria mtusaidie inakuwaje.

Mimi kama mteja nimesaini mkataba wa kulipa mkopo kwa 8% alafu baadae inakuja kuongezwa kwa 15% na unaanza kunikata bila makubaliano na wala mimi sijasaini mkataba wa 15% ya makato ila umeamua tu kunikata.

Sheria ya mkopaji hapo inasemaje? Mimi nadhani kama mabadiliko hayo yalitakiwa yaanze kwa wateja wapya na sio wa zamani.
 
nashindwa kuelewa-sijawahi sikia official statement kutoka kwa kiongozi yoyote kuwa makato yameongezeka na kwenye website ya Bodi ya mikopo hakuna tangazo lolote linalosema makato yameongezeka
 
Vyama vya wafanyakazi kila mwezi vinatukata alaf maslah ya watumishi hayafanyiwi kazi kah, wapo kimya tu km hawaoni
 
sasa ntafataje kazi wakati siwezi hata kulipa kodi ya nyumba wala kulipa nauli kwenda ofisini maana mshahara wangu umebaki 300,000 tu
kodi ya nyuma nalipa -250,000
nauli kwa mwezi-35,000
umeme nalipa-40,000
maji nalipa 20,000
chakula kwa mwezi-250,000
dah asante Magu na team nzima sina cha kuwaambia zaidi ya kusema umaskini umeniingia
 
Msaada wa Kisheria; Kuhusu suala la bodi ya Mikopo naomba wasomi wa sheria nisaidie. Wakati nakopeshwa pamoja na Wenzangu Miaka Hiyo, Sheria Iliniambia nitakatwa asilimia nane kama rejesho kila mwezi. Na nilipoanza kurejesha nilianza na hiyo lakini ghafla sheria imebadilishwa na kuwa marejesho yatakuwa asilimia 15% na mimi nikahamishiwa huku wakati mkataba wangu haukuwa hivyo, Sasa Nahitaji kufungua shauri dhidi ya sheria hii. Ila nahitaji pia msaada wa mawakili na walioumizwa ambao wanataka tufungue shauri lapamoja tuweze kupata tafsri ya kisheria kama ni halali au la? Karibuni kwa msaada ushauri na ushirikiano wa shauri hili
 
Mtaani huku ni soo watu 15% Ndo habar ya mjini, lakini me nilitaka kidogo wanasheria mtusaidie inakuwaje Mimi km mteja nimesaini mkatakaba wa kulipa mkopo kwa 8% zen badae inakuja kuongezwa kwa 15% na unaanza kunikata bila makubaliano na wala me cjasaini mkataba wa 15% ya makato Ila umeamua tu kunikata, sheria ya mkopaji hapo inasemaje? Me nadhani km mabadiliko hayo yalitakiwa yaanze kwa wateja wapya na sio wa zamani
"LHRC tunajiandaa kuandaa kesi kupinga malipo ya bodi ya mikopo ya 15% kwa waliopata elimu ya juu tutakuwa na kikao na mawakili jumanne next week saa 10 ofisi za LHRC karibuni mawakili pia mje kwa wingi."

Advocate Patience Mlowe
 
"LHRC tunajiandaa kuandaa kesi kupinga malipo ya bodi ya mikopo ya 15% kwa waliopata elimu ya juu tutakuwa na kikao na mawakili jumanne next week saa 10 ofisi za LHRC karibuni mawakili pia mje kwa wingi."

Advocate Patience Mlowe
Hili la kukatwa 15% kuna mdau mmoja aliwahi kulijadili,kuwa duniani hakuna sheria inayotungwa na kutumika kwa kipindi kilichopita.
Alitolea mfano sheria ya wahujumu uchumi iliyotungwa baada ya watuhumiwa kukamatwa.
Baada ya kutiwa hatiani walikata rufani wakipinga kuhukumiwa kwa sheria ambayo haikuwepo wakati wanatenda kosa, na mahakama iliwakubalia rufaa yao.
Jambo hili linashabiana na hilo la sheria mpya ya makato ya 15% kwa watu waliosaini makubaliano yakukatwa 8%.
 
Wanasheria na mawakili simamieni hili sasa maana hii nchi imekua kama sehemu ya majaribio kila siku, hivi mbona ile sheria ya uhujumu uchumi iliwaacha waliofanya kabla haijatungwa hii ianze na hawa waliopita? Hata ada zinapopanda huwaaffect wanaoanza mwaka husika si wanaondelea
 
Back
Top Bottom