Naomba kufahamu Sheria ya Ardhi inasemaje kwenye hili

Dark mode

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
732
859
Miaka kama mitano nyuma mkoa fulani niliwahi kuandikishana mkataba na mtu fulani.

Nina kieneo ambacho ndani ya eneo hilo nilihesabu hatua kadhaa kumkatia mtu huyo kwa makubaliano ya kunijengea nyumba ya vyumba viwili na eneo lake ataliendeleza au kufanya lolote baada ya kumaliza ujenzi wa kile nilichokihitaji.

Mkataba ule aliniwakilisha mtu anaesimamia eneo kwa upande wa kusaini kwahiyo miezi kama miwili mbele nilipokwenda kuuchukua nilikuta kwenye mkataba hakuna ukomo wa muda(yaani akukua na ukomo kua mtu huyo asipotimiza masharti ndani ya muda tuliokubaliana basi eneo hilo nitakua na haki yakulichuku).

Ilipita miaka takribani minne bwana yule aliishia kujenga chumba kimoja kilichoishia kwenye linta na mbaka sasa ukuta umeweka ufa na hana dalili zozote zile zakutekeleza hilo kwa sasa kwa madai ya kwamba hali ni ngumu.

Alishawahi kusikika akisema yeye atajenga hata kama itachukua miaka 10 au 20 kwasababu mkataba wake hauna ukomo kwamba ni lazima amalize hilo mwaka fulani.

Sasa swali langu ni je sheria ya ardhi ipoje hapa,endapo mimi nitahitaji nimrudishie gharama zake kwa hapo alipofikia na mimi nibaki na eneo langu kutokana na muda tuliochukua na bado hakuna dalili za kutekelezwa hilo kwa kiburi cha mkataba tulioandikishiana.
 
Huo mkataba ulikuwa na mapungufu unaweza kumruka

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom