10 years of Diamond Platnumz

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Kwanza kabisa na mpongeza kwa kufikisha miaka 10 ya mziki wake SI rahisi kuwa on top kwa miaka hiyo yote lakini huyu mwamba kaweza.Haya ni baadhi ya mambo aliyofanya kwenye kipindi chake chote Cha mziki

1.kutengeneza wasanii wakubwa from scratch kupitia label yake ya WCB Kama vile Rayvanny, Harmonize,Mboso na Lavalava

2. Kujiingiza kwenye biashara ya media nakuanzisha wasafi tv na wasafi fm

3.kusaidia Jamii mfano alitoa madawati 600 kwenye baadhi ya shule zenye madawati machache, kuchangia ujengwaji wa maabara sumbawanga ikapelekea moja ya shule kuitwa shule yake Kama sehemu ya heshima, kuwapa bima wamama 40 tandale, kutoa takribani bajaji 30 kwa walemavu kwenye birthday iliyofanyika tandale,kujitolea kusomesha watoto wa 3 nje ya nchi, kuchangia vitanda vya wagonjwa hospital ya kijitonyama n.k

4. Kutengeneza ajira mfano ameajiri wapigaji picha especially wa matukio ya show, bodyguards, IT wanaoendesha page ya zote za wasafi pamoja na YouTube,DJs, video production nfano zoom extra or zoom production, madancers n.k

4.music achievement mfano diamond ameshinda tuzo nyingi SI chini ya 100 zikiwemo za ndani na nje ya nchi Kama vile MTV EMA, CHANNEL O, AFRIMMA n.k, ngoma yake ya merry you ilifika platnum yaani ilinunuliwa na watu wengi Sana na kuwa ngoma yenye mauzo makubwa kuliko ngoma yoyote ya Africa kwa mwaka huo, kuingia makubaliano na label kubwa ya UNIVERSAL MUSIC wakutangaza kazi zake ya music, kufanya ngoma na mtu Kama Rick rose, Omarion na neyo, ngoma zake Kama Mdogodogo, Nana na Number one kuweka record ngoma zilizoshika number 1 kwenye chart za ngoma za Africa kwa muda mrefu kwenye chart za media za mziki Kama vile SOUNDCITY, CHANNEL O,MTV BASE.n.k

Aliyoifanya ni mengi Ila nimeweka machache ili Uzi usiwe mkubwa.

Baada ya mambo mengi aliyoifanya kwenye mziki wake ameona aje na idea ya kuenda kigoma na treni na watu kwa namna moja au nyingine wamechangia mafanikio yake

Binafsi nimependa idea yake cos kwenye hiyo ameajili watu watakao wapikia wageni wote kwenye treni bure na amechukua mabehewa 7.kutakuwa na behewa moja kwa ajili ya watu kula mziki na wametengeneza Kama disco fulani lakini pia kutakuwa na documentary yake ya mziki ambao watu wataona na pia watakapo fika kigoma wageni wake wote hawatalipa chochote gharama zote zitakuwa zake so amefanya Kama fadhira fulani

#biguptohim namtakiwa Mafanikio mema
 
Pale inno anajitahidi kumpamba domo
IMG_20191221_212653.jpg
 
Watanzania tuna shida moja kubwa kuna mambo hatukuwahi kutarajia mwenzetu afanye na akitokea anaethubutu na kufanikiwa tunapinga!

Nimeona comments muda huu kwenye insta kuhusu treni ya kigoma. Mchizi ka post kigodoro kwa treni watu wameingia kwenye dini sasa ooh ".....mondi utakufa tu", ".....mrudie mungu...oooh ".....dunia tunapita...."ooh "......treni ya maasi ikifika mswali"

Ila mambo kama haya yakifanywa na wasanii wa nje nigeria huko, ulaya au hata kenya utawaskia wananzengo ".....ona ubunifu wa treni...." "...bongo tumekwama wapi...?"

Dini ni dini na sanaa ya kidunia ni sanaa ya kidunia. Huwezi kuwa bongo fleva ukawa mdini at the same time sababu unachoimba na yanayofanyika club yanajulikana...

Kwa hiyo tusidanganyane kupiga tour huku tumevaa vaa kanzu na vibarakashia....aidha umche mungu au ufanye bongo fleva. Mondi kaamua kufanya bongo fleva. Kama upo katikati basi usi mjaji mwenzako..!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom