1 kg ya dhahabu

1 kg ya dhahabu

Kaisari

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2012
Posts
3,636
Reaction score
3,046
Naomba msaada waungwana nina kg 1 ya dhahabu naomba kujua wapi nitauza kwa bei nzuri kidogo.

Ninashukuru kwa mawazo niliopata, ila ukweli leseni sina na mimi sio mchimbaji, nimeipata kwa kuokotaokota taratibu kwa muda mrefu toka kwa wachimbaji wadogowadogo, (buter trade).
Bado ninasisitiza ninaomba kujua nitauza wapi,
wanaotukana na kubeza waendelee tuu, wana uhuru wa mawazo, ninachohitaji ni kujua nitauza wapi,

Naomba msaada wa hilo.
 
Alafu ujiandae na leseni vinginevyo kama wakikundua huna leseni wajanja wa mjini watakutapeli alafu ukienda kushitaki polisi kabla ya kufungua mashitaka unaombwa leseni ili kukuathiri kisaikolojia (dealers wa madini wanamkono mrefu inabidi ujipange vinginevyo unatakiwa uligawe katika mafungu mafungu)
 
Nenda kwa mwarabu yusufu kkoo hata kg 10 ananunua.
 
inatia shaka! dhahabu! kutafuta soko/ au unaekt mshamba fulani ili uingize watu mimba au/ hiyo ni famfa! mjini pana staili nyingi
 
papaa msofeeee!!!mmetapeli wasafiri ubungo sasa mmehamia jf
 
hata mi nashangaa dhahabu kupigiwa debe wakati inajiuza yenyewe haya bi maajabu,ungesema umeokota hapo sawa kumbe menunua ,unanunua kitu hujui pa kuuzia
 
1 gram = 80 000 tsh
Sa calculate mwenyewe ujue kg ni bei ngapi
 
When it comes to gold, never trust anyone! Hawa unaowaomba wakuelekeze wataku divert uingie kanya boya! Kama watu waliweza kum divert raisi akapita bara bara sio, kule Arusha, ndio watashidwa kuku divert wewe?
 
Asante kwa kunielekeza, ninajua kariakoo lakini ile mitaa inanitatiza mara kwa mara , ninaomba kama hautajali unielekeza ni mtaa gani anapatikana huyu ndugu.

Nashukuru.
 
hata mi nashangaa dhahabu kupigiwa debe wakati inajiuza yenyewe haya bi maajabu,ungesema umeokota hapo sawa kumbe menunua ,unanunua kitu hujui pa kuuzia


sio kosa kununua kitu halafu ukauliza nitauza wapi, tambua kwamba mtu yeyote anatafuta mahali kwenye bei nzuri kuliko pengine, ndiyo sababu ya kuuliza.
kama suala ni kuuza tuu unaweza ukauza hata kwa bei ya chini kuliko ulionunulia, lakini ninauliza ili kupata bei juu kidogo na bahati nzuri hapahapa wamejitokeza watu na kutaja bei, hivyo walau hata nikikaa katika meza ya mapatano ninajua mipaka ya bei.

kuuliza sio ujinga, inaongeza maarifa !
 
Back
Top Bottom