Sijui ni lini na mimi ntakuwa na furaha maishani, Furaha yangu ilitoweka pasipo kujua baada ya kumpoteza mama yangu miaka mingi iliyopita nikiwa bado mdogo sana.
Maisha niliyopitia kutoka kwa ndugu, mama wa kambo pamoja na baba asiyejali yananipa hasira sana, sijui hata nimlaumu nani kuzaliwa...