Kampuni mama ya Facebook imetangaza uamuzi huo leo kwa maelezo kuwa inalazimika kuondoa 13% ya wafanyakazi wake ili kubana matumizi.
Mkurugenzi Mtendaji Mark Zuckerberg amesema katika robo ya 3 ya mwaka mapato yameshuka kwa 46% sawa na Tsh. Trilioni 13.
Wafanyakazi walioathiriwa watalipwa...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako amewagiza waajiri kuweka mifumo kwa wafanyakazi wao ya kuwewezesha kufanya mazoezi ikiwemo ‘gym’ ili kuwa na wafanyakazi wenye afya njema.
Waziri huyo amesema moja ya sababu ya kutaka gym ziwepo...
Mmiliki huyo mpya wa Twitter ametetea kufutwa kazi kwa takriban nusu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, akisema "hakuwa na chaguo" kwani Twitter ilikuwa ikipoteza zaidi ya Tsh. Bilioni 9 kwa siku.
Bilionea huyo alisisitiza katika ukurasa wake wa twitter kwamba wote waliopoteza kazi walipewa malipo...
Kupitia Barua Pepe iliyotumwa Novemba 3, 2022 kwa wafanyakazi 7500 imewaeleza kuwa watajulishwa kuhusu mustakabali wa ajira zao leo Novemba 4, 2022.
Hatua hiyo inakuja siku chake tangu Tajiri wa Dunia Elon Musk kukamilisha ununuzi wa kampuni hiyo kwa Tsh. Trilioni 102 ambapo alitangaza kufanya...
Wakati Rais Samia anatangaza kuongeza watumishi mishahara kwa 23% wengi walifurahia ila mwishoni wengi waliambulia Tsh 12,000 kwenye mishahara yao baada ya kukatwa kodi.
Sasa hii ya watumishi wenye kesi ya Jinai ya kufoji vyeti kulipwa mafao yao wafafanulie ni kiasi gani wanalipwa Ili...
Uteuzi huo unajumuisha watu 10 ambao watakuwa wakifanya kazi kwa karibu na Mkuu huyo wa Nchi.
Baadhi ya majina mashuhuri kwenye orodha hiyo ni pamoja na aliyekuwa mwanahabari wa Citizen TV Hussein Mohamed ambaye ameteuliwa kuwa Msemaji wa Ikulu na mwanauchumi David Ndii ambaye ameteuliwa kuwa...
Upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabiliwa washtakiwa 13, wakiwemo waliyokuwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), bado haujakamilika. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matano, likiwemo kuharibu noti 4.6 milioni kwa kuzichanachana na hivyo kuisababishia benki hiyo hasara...
Zamani ilikuwa ukifika ofisi za TRA au TANESCO basi ni lazima ukutanane na watu wanaoitwa vishoka, nina uhakika kwa sasa watu hao wamesambaa kwenye ofisi nyingi tu.
Binafsi sijawahi kufanya kazi na hao watu kwa kuwa naelewa wapo nje ya mfumo wa ofisi husika, lakini nimeshashuhudia mara kadhaa...
Wafanyakazi 150 wa Mradi wa ujenzi wa hoteli ya nyota tano Blue Amber, wamepoteza kazi baada ya Wizara ya Ardhi kusitisha mkataba wa ukodishaji ardhi kwa Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar licha ya kuwapo amri ya Mahakama ya kutaka ujenzi kuendelea.
Wakizungumza na waandishi wa habari, wafanyakazi...
Naandika hii taarifa kwa niaba ya wafanyakazi wa Uhuru Publications Limited ambao wapo na wale ambao walishaondoka hata waliokufa pia, pamoja na wastaafu.
Kampuni hiyo yenye gazeti la Uhuru na Mzalendo inadaiwa mamilioni ya fedha za malipo ya mafao pamoja na michango ya wafanyakazi tena ni ile...
Hadi sasa kuna kampuni nyingi za bima ya afya nchini ikiwemo NHIF. Cha ajabu, katika mazingira sawa ya kibiashara licha ya NHIF kuwa na upendeleo wa kuwa na wanachama wengi kuliko kampuni zote za bima nchini kwa kujaziwa wanachama lukuki kutoka serikalini na taasisi za serikali, ni NHIF pekee...
"ANDIKO HILI LIMETOLEWA NA WAFANYAKAZI WA RADIO 5 ARUSHA"
"Habari za wakati huu wanahabari wenzetu.
Sisi ni Wafanyakazi wa Radio5 Arusha iliyo chini ya TAN COMMUNICATION MEDIA ambayo inamilikiwa na Familia ya Mzee Edward LOWASSA kwa masikitiko kabisa tunalazimika kuandika ujumbe huu kueleza...
Hali ni mbaya kwa kweli laana inatutembelea kwenye Tozo
Hivi kweli Tozo mmeigeuza kama KODI jaman? Hadi akaunti za Shariah mnakata tozo? daah.
Nijuavyo mie kwanza ilitakiwa kila mwezi tuambiwe imepatikana kiasi gani hilo limeshapotezewa skuhizi.
Pili je hii tozo ni mpaka lini au ndio milele...
Aliyeleta wazo la Tozo za Bank transfer alilenga kila mshahara wa watumishi wa serikali ukatwe kwa sababu mishahara yote inapita benki lakini kasahau kuwa mshahara huo huo umeshakatwa PaYE na kwa sheria za kikodi upaswi kufanya double taxation,Kama ikiendelea wafanyakazi mtaumia
Rejea Gazeti la Mwananchi la May 27, 2022
Serikali imetoa kibali cha kurekebishwa kwa posho ya kujikimu safarini kutosha Sh120,000 hadi Sh250,000 kwa daraja la juu na Sh80,000 hadi Sh100,000 kwa daraja la chini.
Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 27, 2022 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais...
Tundu Lissu mwanasheria nguli tunakuombea uachike huko Ubelgiji kwa Amsterdam urudi Tanzania utetee wafanyakazi wanaoteseka na mfumuko wa bei na uongezwaji hafifu wa mishahara yao. Ukiwatetea kwa juhudi kama ulivyokuwa unawatetea Acacia wakati wakiibia madini watanzania hakika utabarikiwa sana...
Naomba kutoa Rai kwa serikali!
"Ukicheka na nyani Utavuna mabua" TUCTA must watch out!
Kuna HAKI na WAJIBU wa kila MTU
Haki ya mfanyakazi ni kulipwa ujira wake kama kanuni zinavyosema! LAKINI wajibu wa mfanyakazi ni kufanya kazi bora ili mwajili awe na sababu ya kulipa ujira huo hata Zaidi...
Natamani sana mabibi na mabwana shamba tuanzishe chama chetu. Ukiangalia wafanyakazi wenzetu kwenye wizara zingine wana vyama vyao vyenye nguvu kuwatetea katika mambo mbalimbali ya maslahi yao!
Sisi tumelala Sana hatuna hata wa kutusemea na badala yake tumegawanyika wengine wanajiona Bora...
HABARINI
Ninashida ya kujua nafasi za kazi zinazopatikana kwenye kiwanda cha kusindika maziwa mfano benki kuna afisa mikopo na wenge. Je, kwenye kiwanda cha maziwa ni nafasi gani zipo?
Asanteni
Hapa katikati naona kama bifu kati ya wafanyakazi hasahasa walimu na jobless inazidi kuota mizizi
hii nibbaada ya walimu wengi kupigana vikumbo na jobless kwenye kazi za sensa
ongezeko la mshahara wa 23.3% isiyoeleweka limefanya walimu wadhihakiwe kila sehemu,
sasaivi kila kitu wanaangushiwa...