Kila nipitapo humu, nimekuwa nasoma upuuzi uitwao 'utabiri' wa baadhi ya mazwazwa yanayojikomba kwa bi kidude kutaka wageuzwe chawa na kutupiwa makombo.
Si hapa tu, hata huko mitaani, mchezo huu mchafu umeenea na kutamalaki. Ni kama tumegeuka taifa la wapiga ramli na washirikina kirejareja...