Wakuu,
Kama alivyotuahidi jana, siku ya leo Mwanaharakati nguli Afrika Mashariki, Maria Sarungi atazungumza kinaga ubaga kuhusu namna alivyotekwa mpaka kupatikana kwake.
Bado haijaeleweka hadi sasa kama atazungumza kwa kujirekodi video kueleza nini hasa kilitokea, atatengeneza thread ya...
Wakuu,
Kupitia ukurasa wake wa X, Fatma Karume ameweka post ya kuwashukuru wote waliyohakikisha Sarungi anakuwa salama, na kwamba ameambiwa Sarungi amerejea nyumbani kwake.
Soma Pia: Mwanaharakati Maria Sarungi adaiwa kutekwa na watu wenye silaha Nairobi, wakiwa na Noah nyeusi
TAARIFA za hivi punde kutoka Nairobi ni kuwa Maria Sarungi ametekwa na watu wenye silaha na kuondoka naye pasipo julikana. Tunaendelea kufuatilia.
Inasemekana ametekwa na wanaume 3 wenye silaha waliokuwa kwenye gari aina ya Noah nyeusi, katika mtaa wa Chaka kaunti ya Kilimani, Nairobi...
Wakuu,
Mnakumbuka ile story ya wale vijana watano waliotekwa Desemba 2021 kule Kariakoo.
Hivi karibuni wazazi wa vijana hao wamejitokeza tena kuomba msaada kwani mpaka sasa hakuna kitu kimefanyika ili kujua vijana hao walipo.
================================================
Miaka mitatu...
Wakuu,
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimelaani tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa mwanachama wake Wakili Joseph Masanja lililotokea Babati Mkoani Manyara.
Kupitia taarifa iliyotolewa na chama hicho Disemba 28, 2024 imeeleza kuwa mwili wa marehemu Wakili Masanja uliokotwa eneo la Bwalo...
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Magharibi Tabora, Isaac Laizer, ameonya juu ya ongezeko la matukio ya utekaji na mauaji, akiwataka wakristo kote nchini kufunga na kuomba kwa dhati ili kutokomeza matukio hayo.
Akizungumza jana, Desemba 8, 2024, katika maombi ya...
Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesisitiza jeshi la polisi kuwa wafanye uchunguzi kufuatia vitendo vya mauaji na utekaji na pale wanapopata taarifa watoe kwa jamii ili wajue kinachoendelea.
Mwenyekiti ameyasema hayo tarehe 04 desemba 2024 akitoa...
Tangu atekwe Nondo wa ACT Wazalendo, hakuna gazeti lolote la serikali, chama dola au vigazeti vinavyofadhiliwa na serikali lililoandika kuhusu habari hiyo. Kwa vyovyote vile ile ni habari kubwa iliyostahili kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti. Hata habari za utekaji mwingine uliofanyika...
Wakuu,
Nimekutana na video ya mke wa Mgombea kupitia Chadema wa Kitongoji cha Stand, kata ya Mkwese, Jimbo la Manyoni Mashariki George Juma Mohamed akielezea namna ambavyo polisi walimkamata na kumuua mume wake kwa kumpiga risasi nne.
Mama huyu anasema kuwa aliwaomba polisi wasimuue mumewe...
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.
Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu
====
UPDATE
JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na...
Wakuu,
Hivi karibuni mwanaharakati wa haki za binadamu na mwanamitandao maarufu nchini Tanzania Godlisten Malissa amefanya mahojiano na kituo cha Jambo na kugusia mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.
Katika mahojiano hayo, Malissa amegusia sarakasi za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa...
Katika siku za karibuni, kumekuwa na matukio ya watu kutekwa na kupelekwa kusikojulikana, hali inayozua hofu kwa Watanzania wengi pamoja na familia, ndugu, jamaa, na marafiki.
Hivi karibuni, mnamo Oktoba 29, 2024, majira ya saa tatu usiku, watu wasiojulikana walimteka mfanyabiashara Joseph...
Familia ya Mzee Ali Kibao kupitia Mohamed Ali Kibao ambaye ni mtoto wa Mzee Kibao, imeomba uwepo wa uwazi na haki katika uchunguzi wa mauaji dhidi ya wahusika wa utekaji na mauaji ya Mzee Ali Kibao huku ikimsihi Rais Samia Suluhu Hassan, kutoa kauli kali dhidi ya wahusika ili kurejesha imani kwa...
Hapa ndipo Tanzania ya Nyerere ilipofikishwa na Watukufu aliowaachia ambao wamejipa Uungu Mtu, Ngoja tuone Mwisho wao.
================
Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Aisha Machano, ambaye anadaiwa kutekwa na kuteswa na baadae kuokotwa kwenye pori la Kibiti, akizungumza tukio...
Dr. Ulimboka alikuwa anatetea haki ya huduma za Afya kwa wote lakini malipo yake alitekwa na kuumizwa sana. Toka tawala zilipofumbia macho kutekwa na kuteswa kwake ndipo wanasiasa wakaona njia pekee yakuwatisha wananchi wanaotaka haki nikuteka ring leaders.
Hali ya utekaji ikaanza kushamiri na...
Haya mambo ya kuteka na Kutekwa tukiyachekea huwa Tabia na yatahamia kila mahali hadi Kwa akina Simba na Yanga, hadi kwa Wafanyabiashara tena hadi Kwa viongozi wa Dini
Mungu wa Mbinguni aingilie Kati Siasa za Teka Teka zifike mwisho
Wenzetu Kenya sasa wanateka Raia wa kigeni (Watalii) hali ni...
Kwa masikitiko makubwa, nashangaa kuona eti maisha na uhai wa watu unaweza kukatishwa kwa sababu zinazoitwa ni Siasa!
Ni ujasiri uliopita kiwango cha Rehema za Mungu, mtu anapoamua kumdhuru mtu, kumtesa na kumwaga damu yake kwa madai ya kuendelea kubaki kwenye nafasi za kisiasa huku akijua...
Wadau mkopoa? Nisiwaxhoshe niende mojakwamoja kwenye swali.
Pamoja na Katibu wa CCM Dr Emmanuel Nchimbi kuonekana hafurahishwi na utekaji na mauaji ya raia,
Lakini yalipoitishwa maandamano ya kupinga vitendo vya utekaji na mauaji ya raia yaliyoitishwa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA, CCM...
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imekemea vitendo vya utekaji, ukatiili na mauaji yanayofanywa na genge la watu wasiojulikana na kulaani tukio la kuchukuliwa na kuuawa kikatili kwa kada wa Chadema, Ally Kibao.
CCT ni Taasisi inayowakilisha Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotestanti pia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.