uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Chagu wa Malunde

    JamiiForums Tanzania Uhusiano wa India na CCM wazidi kuimarika. CCM kushinda uchaguzi mkuu 2025 kwa kuimarisha diplomasia .

  2. Gemini AI

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 LGE2024 Jaji Warioba: Waliosimamia Uchaguzi wa 2019 na 2020 wataendelea na je wanaaminika?

    Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema Chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 zilikuwa kama ajali kwasababu hazikuwa katika utaratibu wa kawaida ikiwemo Mawakala kusambaratishwa wakati wa Kuhesabu Kura Ameongeza kuwa hali hiyo imeanza kuibua hoja na maswali kuhusu...
  3. Mwanamwana

    JamiiForums Tanzania Ndolezi Petro: Polisi waache kutumika kisiasa kwenye michakato ya uchaguzi, wawaachie wanasiasa kunadi sera zao

    Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, anayeshughulikia masuala ya Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira, Mhandisi Ndolezi Petro, amekosoa uchaguzi wa mwaka 2020, akidai kuwa haukuwa huru na haki. Akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni Bumbuli, Mkoani Tanga...
  4. A

    JamiiForums Tanzania Sifa za Kiongozi Bora: Zitakusaidia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu

    Sifa za Kiongozi Bora: Zitakusaidia Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ___________________ 1. Kiongozi bora ni mjuzi, siyo mjuaji. Mjuzi ni muelewa. Mjuaji ni mbabaishaji! Chenga! 2. Anaishi kwa maono na siyo maneno! Maono ni kuona kesho ukiwa leo! Maneno na hali ya...
  5. A

    JamiiForums Tanzania Ili kuweka Shinikizo la Katiba Mpya wananchi wakikatae Chama Tawala kwenye Uchaguzi wa 2024 na 2025

    Ndugu wananchi hususani "Paskali" kumekuwa na juhudi mbali mbali za kukitaka Chama Tawala kuweka mazingira mazuri ya uongozi Kwa kuwa na Katiba Mpya na yenye kuakisi Hilo. Zaidi ya hadithi njoo uongo koleaau kwakuwa wao ndio waneshikulia siri zao na uwazi wa kila moja wetu (mpini Sisi...
  6. Mwanamwana

    JamiiForums Tanzania Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi mkuu mpaka 2026

    Serikali ya Sudan Kusini imeahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 2024 hadi Desemba 2026 kutokana na changamoto za maandalizi. Ofisi ya Rais Salva Kiir imetaja hitaji la muda zaidi kukamilisha sensa, uandishi wa Katiba mpya, na usajili wa vyama vya siasa. Uchaguzi huo umeahirishwa...
  7. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Hivi ndivyo CCM huiba kura na CHADEMA wasijue wameibiwaje kura

    Mwaka 2020 wakati wa Kampeni za uchaguzi Mkuu, nilikuwa nawaambia viongozi wangu kuwa ni lazima CCM watatuibia kura kwa mtindo Mpya kabisa. Sababu ya kusema hivyo ilikuwa ni jinsi CCM walivyopunguza matumizi ya mabavu ya dola dhidi ya CHADEMA kwenye Kampeni za uchaguzi ule. Hapo chini nimeweka...
  8. Mr-Njombe

    JamiiForums Tanzania Je ni kwanini Tanzania hairuhusu mgombea binafsi?

    Habari waungwana! Je ni kwanini nchi yetu haimpi nafasi mgombea binafsi kugombea na kushika nafasi mbali mbali za kisiasa ikiwemo ubunge na Urais. kwani kwa maoni yangu hii ya kua lazima uwe mwanachama kwanza kunamfanya kiongozi kuweka kwanza maslahi ya chama mbele kuliko mahitaji ya wananchi...
  9. TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

    JamiiForums Tanzania Kwanini serikali ya CCM haitaki uchaguzi wa serikali ya mtaa usimamiwe na TUME HURU YA UCHAGUZI?

    kipara kipya, Lucas Mwashambwa, the big boss, CHAWA, ChawaWaMama na wengine. Naomba majibu. Kwanini hamjiamini? Je ni kweli bila figisu CCM haishindi?
  10. Webabu

    JamiiForums Tanzania Vita vya Gaza vikifikisha muda wa uchaguzi wa Marekani hakutakuwa na kusitishwa vita tena bali kutangaziwa ushindi Hamas

    Kwa ufundi na subira za hali ya juu Hamas wameweza kuhimili kipigo kizito cha Israel na washirika wake mpaka umefika mwaka mmoja hapo Septema 7. Uzito wa vita hivyo umeonekana na kila upande ambapo mpaka sasa kikwazo kikubwa ni waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu ambaye anaona aibu...
  11. GENTAMYCINE

    JamiiForums Tanzania Kwa 'Dua Shtakia Mungu' itakayosomwa Afrika Mashariki huenda kuna Chama Kikakosa Mgombea Urais wake katika Uchaguzi Mkuu ujao

    Haya tuanze mapema kumtafuta wa Kumrithi.
  12. S

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Mtazamo: Wanamtengenezea mazingira ya kuchukiwa na umma ili 2025, kundi kubwa la CCM lijitenge ili wamuangushe kwenye uchaguzi

    Nikitazama mwenendo wa mambo, hii ndio picha ninyoipata kutokana na haya matukio hasa kwa jinai yanavyotekelezwa. Wanafanya ukatili mbaya na wa kutisha halafu wanaacha nafasi ya watu kushuhudia ukatili uliiofanywa kwenye mwili wa muathirika lengo ni kuamsha chuki na hasira na wanajua lawama...
  13. Tlaatlaah

    JamiiForums Tanzania Tatizo na sababu ya yote haya ni uchaguzi na nafasi za uongozi wa kisiasa tu hakuna kingine

    nawaombea kila la kheri wahusika na washiriki wa uchaguzi muhimu sana uliosalia kwa maendeleo ya ushindani wa ndani ya vyama vya siasa, na ustawi wa demokrasia nchini. Mwenyezi Mungu awaepushe na kila hila na shari ilopangwa dhidi ya maisha ya mshiriki au muhusika yeyote kwenye masuala haya ya...
  14. Suley2019

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Mahakama yatoa kibali Wadau wafungue Kesi kupinga Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Mahakama Kuu ya Tanzania leo September 09,2024 imesema kuwa waleta maombi kwenye shauri ambalo walikuwa wanaomba idhini ya Mahakama wana haki ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Sheria ndogo zilizotungwa kwa lengo la uratibu na uendeshaji wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 kupitia...
  15. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Waziri Masauni avitaka Vyombo vya Usalama kulinda Amani Uchaguzi Mkuu

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amevitaka Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo kujiandaa na chaguzi zinazokuja ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu (2024) na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani (2025) huku akivitaka...
  16. W

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Mongela: Tunaingia kwenye Uchaguzi na Uhakika wa Ushindi

    Wakati vyama na wadau wakianza kujiweka mguu sawa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kina hakika wa kupata ushindi wa kishindo. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu (CCM-Bara), John Mongella baada ya kupokea taarita ya...
  17. JET SALLI

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu watu husema wakiwahonga fedha zao chukueni au kuleni ila msiwachague je ni sahihi?

    Ndugu zangu kauli hz zimezoeleka sana tunapokuwa tunaelekea kwenye uchaguzi na tukiwa kwenye uchaguzi vilevile,je Hv ni kweli mtu anaweza kula pesa ya mtu na asimpe kura?,na je aliyetoa pesa hizo anajua kweli kwamba waliokula fedha zake hawakumchagua, je anaweza kuamini rahisi kiasi hicho. Mimi...
  18. S

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kauli ya Nape na Mkuu wa Wilaya ya Longido kuwa serikali ya CCM inalazimisha ushindi katika uchaguzi zinahalalisha kuindoa CCM madarakani kwa nguvu

    Kawaida, chama cha siasa kilichopo madarakani kwa kuchaguliwa ki-demokrasia, hakipaswi kuondolewa madarakani kwa nguvu. Uhalali wa kuiondoa serikali madarakani unapaswa uwe kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa kidemokrasia, na kama kuna ukiukwaji wa haki za uchaguzi, mfumo wa sheria wa...
  19. J

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Askofu Mwamakula: Kama kwenye chaguzi za ndani ya vyama Rushwa ilitawala itakuwaje kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu?

    Kichwa Cha habari ndio swali alilouliza askofu Mwamakula ukurasani X Kwenu CHADEMA 😄😄🔥 --- Kupitia ukurasa wake Rasmi wa Mtandao wa X (Zamani Twitter) Askofu Mwamakula anaadika: Kama katika chaguzi mbalimbali ndani ya vyama vya siasa, uwezo wa kifedha miongoni mwa wagombea ndio uliotumika au...
  20. M

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kauli ya DC Longido, Marco Ng’umbi imetibua kidonda cha Uchafuzi wa Uchaguzi sasa wanahaha kujisafisha

    Kauli ya aliyekua mkuu wa wilaya ya Loliondo mkoa wa Arusha Marco Ng’umbi kua serikali iliwezesha ushindi wa madiwani na baadhi ya wabunge nchini katika uchaguzi uliopita, imetibua kidonda cha madai kua mifumo ya sheria za uchaguzi ili viongozi wanaopatikana watokane na matakwa ya wananchi walio...
Back
Top Bottom