uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Wananchi wa Lupembe wako tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Wananchi wa jimbo la Lupembe wameeleza utayari wao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika leo Novemba 27, 2024 Nchi nzima huku wakiweka wazi Matarajio yao kwa viongozi wapya watakaochaguliwa Wananchi hao akiwemo Fikiria Vicent Kisogole, Salvina Barton Mpolo na Martina Isdol...
  2. Mindyou

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Tundu Lissu anazungumza kuhitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Ikungi Singida

    Wakuu. Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu anazungumza muda huu huko mkoani Singida kuhitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Fuatilia uzi huu kujua nini kinaendelea Tundu Lissu amesema kuwa mara ya mwisho Tanzania kufanya Uchaguzi ilikuwa nwaka 2014 kwani mwaka 2019...
  3. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Dkt. Philip Mpango awahimiza Wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba 2024. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na abiria...
  4. Mindyou

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mkuu wa mkoa wa Dodoma: Atakeyevuruga Uchaguzi Dodoma atachukuliwa hatua

    Wakuu, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya mwananchi yeyote atakayeonesha viashiria vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika kesho Novemba 27, 2024 nchini. "Siku ya kesho ya kupiga kura kila mtu atunze amani...
  5. T

    JamiiForums Tanzania LGE2024 CHADEMA wanashiriki uchaguzi wakitegemea nini? Hatutaki malalamiko

    Msije baadaye mkasema mmedhulumiwa kura au kura zimeibwa. Mnapoingia uwanjani ni kuwa mmekubaliana na sheria na taratibu za mchezo. Hakuna excuses za kipuuzi. Ni kupambana na kukubaliana na matokeo. Hakutakuwa na excuses ni mapambano. Mshindi apatikane. Maana hamchelewi kusema mlinyanyaswa...
  6. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Dorothy Semu amuonya Mtendaji wa Kijiji kutoipendelea CCM Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amemuonya mtendaji wa Kijiji cha Angalia kutopendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) wajibu wake nikutumikia wananchi sio ubaguzi wa itikadi katika uchaguzi. Kauli hiyo ameitoa baada ya mtendaji huyo kuzuia mikutano ya chama hicho kutumia maeneo ya Umma, Semu...
  7. Political Jurist

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Shemsa asisitiza umuhimu wa Uchaguzi katika maendeleo

    Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Ndg.Shemsa Mohamed ameendelea na ziara yake yenye jina la Siku Saba za Moto ambapo tarehe 25 Novemba, 2024 aliweka kambi katika Jimbo la Kisesa akitembelea Kata ya Bomani ,Kata ya Isengwa na Mwasengela. Ndg.Shemsa amekutana na kuzungumza na...
  8. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 CCM hatutegemei dola, tutawashughulikia watakao vuruga Uchaguzi

    Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimesema kimejipanga kwa njia zote kuhakikisha kinalinda amani kabla ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi ikiwemo kuwadhibiti wale wote wenye nia mbaya (ovu) ya kutaka kuvuruga Uchaguzi kwa kuanzisha Vurugu. "Asitokee mtu yeyote au kundi kupanga njama za kutaka...
  9. G

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Sielewi lengo la CHADEMA kushiriki uchaguzi huu

    Inajulikana wazi kuwa CCM hawawawezi CHADEMA katika sanduku la kura, hivyo imeweka nguvu kubwa kwenye figisu na dhulma. CCM tayari wameonesha taa nyekundu ktk hatua za mwanzo kwa kuwaengua wagombea wa chadema 16,0000, na baada ya rufaa wagombea 5,000 tu ndiyo wamerejeshwa. Pia viongozi wa...
  10. Mzee Mwanakijiji

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 LGE2024 Wazo Jipya: Sema Mambo 3 CHADEMA wafanye sasa kwa Uchaguzi Mkuu 2025

    Ukiniuliza mimi ntasema mambo yangu matatu; siyo mageni sana lakini naamini yanaweza kuisadia CHADEMA kujiandaa na uchaguzi mkuu mwakani. Na wewe kama unayakwako yaweke labda katika wastani yatapatikana mambo matatu makubwa. 1. Itangaze mapema kama msimamo wa chama kuwa wagombea wote wa ubunge...
  11. The Watchman

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Chalamila: Kwa atakayetishia usalama siku ya uchaguzi tutamnyakua na hatokuwa salama

    Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza jijini Dar es salaam kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo mwezi Novemba 27, 2024 amesema hali ya usalama mkoa wa Dar es salaam ipo vizuri na mtu yeyote atakayejaribu kuharibu amani iliyo siku ya uchaguzi hatoachwa salama na...
  12. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Dkt. Doto Biteko ahimiza Watanzania kupiga Kura Novemba 27, 2024 asema ni Haki ya Kikatiba

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewahimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024. Dkt. Biteko ametoa rai hiyo leo Novemba 25,2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia...
  13. Mwanamwana

    JamiiForums Tanzania LGE2024 ACT Wazalendo Tunduru: Kuna vijana wamepangwa kupiga kura za mapema, tunawaonya...

    Mwenyekiti wa ACT Wazalendo wa Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma, Yasin Mohamed Mawila, ametoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la udanganyifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Akizungumza Jumapili, Novemba 24, 2024, kwenye mkutano wa kampeni...
  14. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mussa Zungu ajitosa kampeni za Mtaa kwa Mtaa, awaombea Kura Wagombea CCM, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Mussa Azzan Zungu, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, ameendelea na kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Upanga Magharibi, jijini Dar es Salaam. Amengia kuogea na wananchi mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba, Zungu amewanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika...
  15. The Watchman

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Askofu Tanga: Siku kabla ya kupiga kura msisahau kuombea Uchaguzi wa mwaka huu kwani ni maandalizi ya uchaguzi wa mwakani

    Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa vitongoji na vijiji unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu, Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Maimbo Mndolwa ametoa wito kwa watanzania kuchagua viongozi wakufaa bila kujali itikadi za vyama vya siasa. Askofu Mkuu Maimbo...
  16. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Tamko la CCM kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

    TAMKO LA CCM KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandaa tamko maalum kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024. Uchaguzi huu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, kwani utahusisha kuchagua wenyeviti wa mitaa, vijiji, vitongoji, wajumbe wa kamati za...
  17. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Samia Kagera CUP Yahitimishwa kwa Kuwahamasisha Vijana Kushiriki Uchaguzi Serikali za Mitaa

    Mashindano ya Samia Kagera Cup 2024 yaliyowakutanisha vijana na wananchi wa Mkoa Kagera kwa kuwahamasisha kushiriki kikamilifu na kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024, kushiriki shughuli za maendeleo, kuonyesha vipaji pamoja na kuongeza ushiriki...
  18. Nehemia Kilave

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Tamko la kutangaza siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa siku ya mapumziko la mwaka 2024

    TAMKO LA KUTANGAZA SIKU YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA SIKU YA MAPUMZIKO LA MWAKA 2024 KWA KUWA kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa, Sura ya 35, kinampa Rais mamlaka ya kutangaza siku yoyote kuwa siku ya mapumziko kama nyongeza ya siku zilizoainishwa kwenye Jedwali la Sheria...
  19. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wapewa mafunzo na kula kiapo

    Kuelekea siku ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi 1,213 wamepewa mafunzo na kuapishwa kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo utakaofanyika siku ya Jumatano ya Novemba 27, 2024. Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda M. Kawawa amewasihi...
  20. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 DC Malinyi, Waryuba awahakikishia wananchi Usalama na Amani kipindi cha Uchaguzi

    Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba ameyasema hayo wakati aliposhiriki uchaguzi marathoni Wilayani Malinyi kwa lengo la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura Novemba 27, 2024. DC Waryuba amesema kuwa huu ni wakati sahihi kwa wananchi kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba...
Back
Top Bottom