uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Wenyeviti na Wajumbe 1,953 wa Manispaa wala kiapo cha Uadilifu baada ya kushinda Uchaguzi

    Jumla ya wenyeviti na wajumbe 1953 leo Novemba 28.2024 wameongozwa kula kiapo cha uaminifu na uadilifu na Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Illuminata Lutakana mara baada ya viongozi hao kushinda uchaguzi uliofanyika Novemva 27 mwaka huu. Akizungumza baada ya zoezi la hilo liliofanyika katika...
  2. S

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Roho, damu na manung'uniko ya watu, vitajibiwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025

    Watanzania hawaandamani lakini wanamlilia mwenye mamlaka mbinguni na duniani awaadhibu wale wote wanaogiza, kubariki na kutekeleza mauji ya watu wasio na hatia pamoja na ukatili mwingine wowote unaomwaga damu za watu. Binafsi, naamini kwakuwa wanayafanya haya hasa wakilenga uchaguzi mkuu wa...
  3. Inside10

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Dar: BAKWATA yahimiza ushirikiano baada ya uchaguzi

    Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Watanzania wote kuungana na kushirikiana mara baada ya uchaguzi wa serikali kufanyika kwa amani. Akizungumza kwa niaba ya Baraza hilo, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Alhaji Nuhu Mruma, aliwasihi wananchi kuwapa ushirikiano viongozi waliochaguliwa...
  4. S

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Matokeo ya uchaguzi - Wapinzani wameshinda wapi?

    Naona kimya kingi. Sijaona hata sehemu moja wapinzani wameshinda. Naomba mwenye matokeo please... Hapo ulipo wewe chama gani kimeshinda?
  5. S

    JamiiForums Tanzania Hesabu ndogo sana; Kwanini Serikali iliwaamuru Polisi wasimtaje mmiliki wa jengo lililoporomoka Kariakoo hadi uchaguzi wa serikali za mitaa uishe

    Ndivyo watawala wa chama tawala wanavyoendesha nchi hii. Makosa yanayofanywa na watu wao huwa kila jitihada itafanywa kuyafunika. Na hawaoni aibu juu ya hili, huwa wanasema waziwazi ukiwa mtu wao watakulinda. Kwa maneno mengine kuwa mtu wao kunakufanya uwe juu ya sheria. Na kibaya zaidi, Polisi...
  6. Z

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mbowe ajiuzulu kwa kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

    Namshauri Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ajiuzulu kwa kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. Mwenyekiti asitafute kisingizio kingine, anachotakiwa ni kujiuzulu kwa maslahi ya Chama.
  7. R

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Anaandika Lyenda kutoka X: SHIDA ZA UCHAGUZI 2024

    LYENDA (iamLyenda) posted at 5:57 PM on Wed, Nov 27, 2024: Tunachukua fomu kwa SHIDA. Tunarejesha fomu kwa SHIDA. Tunateuliwa kwa SHIDA. Tunafanya kampeni kwa SHIDA. Tunapiga kura kwa SHIDA. Mawakala wanasimamia kura kwa SHIDA. Tunahesabu kura kwa SHIDA. Tunatangazwa kwa SHIDA. Yaani...
  8. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Njombe: Mwenyekiti wa CHADEMA, Rose Mayemba alivyoliamsha baada ya kubaini madudu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe Rose Mayemba amedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana, Novemba 27.2024 nchini kote haukuwa uchaguzi kama ilivyodhaniwa badala yake ilikuwa ni oparesheni kuwashughulikia wapinzani nchini Rose ameeleza hayo...
  9. Mwanamwana

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Kagera: Wananchi waipa CCM Katerero 100% uchaguzi Serikali za Mitaa

  10. Mindyou

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Arusha: Mgombea wa CUF ashinda Uchaguzi Kijenge Kusini, alalamikia kuzuiwa kwa mawakala wa chama chao

    Wakuu, Katika kipindi hiki ambacho matokeo yanaendelea kutangazwa, mengine mapya yanaibuka. Aliyekuwa mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) mshindi wa Uchaguzi katika mtaa wa Kijenge Kusini, kata ya Kimandolu, jijini Arusha, Shaaban Suleiman Mzava, ameeleza malalamiko yake juu ya mawakala wa...
  11. Mindyou

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mwanza: Mawakala wa Uchaguzi wapongeza zoezi la kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Wakuu, Huko Misungwi mkoani Mwanza Mawakala wa Uchaguzi wapongeza zoezi la kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Soma pia: Matokeo ya Uchaguzi Mwanza yaanza kutangazwa, CCM yaongoza maeneo mengi ikifuatiwa na CHADEMA Ina maana kuwa hawa mawakala hawakuona changamoto zilizojitokea...
  12. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Matokeo ya Uchaguzi Mwanza yaanza kutangazwa, CCM yaongoza maeneo mengi ikifuatiwa na CHADEMA

    Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya mitaa Jijini Mwanza yameanza kutangazwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionesha kuongoza kwenye vituo vingi Wilayani Nyamagana. Aidha, licha ya baadhi ya Mitaa Wilayani Nyamagana na kushuhudiwa Wagombea wa CCM wakitangazwa kuongozwa Kwa...
  13. Burure

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Madudu kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2024

    Jana tumepata wasaa wa kushuhudia Uchaguzi wa Serikali za mitaa tuliosubiria kwa muda mrefu. Licha ya kuwa umefikia idadi ya chaguzi Tisa (9) Toka uanze kufanyika hapa nchini lakini bado kuna Mapungufu makubwa. Mosi ni msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni TAMISEMI ambaye na yeye anahusika kwenye...
  14. The Watchman

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mbeya: Mgombea CHADEMA akataa matokeo ya uchaguzi asema anakwenda kufungua kesi Mahakamani

    Mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Mtoni, Kata ya Ruanda, jijini Mbeya kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Elisha Chonya, ameyakataa matokeo akidai kanuni zilivunjwa huku msimamizi wa uchaguzi Bi. Winifrida Stanley akitangaza matokeo ambapo Bilali Gembe wa Chama cha Mapinduzi...
  15. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Rungwe: CHADEMA yashinda Uchaguzi Serikali za Mitaa katika Kata ya Ndato, Kijiji cha Goye

    Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata ushindi mkubwa katika Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe, hasa katika Kijiji cha Goye. Ushindi huu umeonyesha umaarufu na ushawishi mkubwa wa CHADEMA katika eneo hilo.
  16. econonist

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 CHADEMA, ACT Wazalendo na CUF tengenezeni Alliance kupelekea uchaguzi 2025

    Nilichokiona kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni kwamba wananchi Wana muamko wa kupigia kura upinzani shida upinzani umegawanyika. Nina shauri ya kwamba upinzani wafikirie kutengeneza alliance ambapo wataungana 2025 na kuwa na mgombea mmoja wa urais, ubunge na udiwani kwa kuangalia...
  17. Waufukweni

    JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Katibu Mkuu COTU, Francis Atwoli: William Ruto atakuwa Rais katika uchaguzi wa 2027 kufikia saa 4 asubuhi

    Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli, amesema kuwa itakuwa vigumu kumshinda Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027 nchini Kenya. Akiwa mgeni katika kipindi cha JKL Show usiku wa Jumatano, Atwoli alieleza kuwa hakuna mgombea anayeonekana kuwa na...
  18. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

    Wakuu, Ili kuzifikia nyuzi hizi kirahisi, hapa utapata orodha yote ya mikoa inayoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, ambamo ndani yake utapata links za matukio yote yanayojiri katika mikoa husika, mpaka kufikia kwenye matokeo ya uchaguzi huo. ==== Mwaka huu 2024 Tanzania Bara...
  19. Nigrastratatract nerve

    JamiiForums Tanzania ACT WAZALENDO kuwa chama kikuu cha upinzani kitakuwa mshindi wa pili kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2025

    Chama cha @ACTwazalendo kimeshinda Kijiji cha Nkoasenga kilichoko Kata ya Leguriki Jimbo la Arumeru Mashariki. ACT Kura 528 CCM Kura 417 Kwa hivyo Jotsun Mbise ndio Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkoasenga. #VijijiVyaWote #MitaaYaWote #MaslahiYaWote Chama cha ACTwazalendo kimeshinda Mtaa wa...
  20. G

    JamiiForums Tanzania Inaogofya sana kuona hakuna mtu wala taasisi inayokemea dhulma katika uchaguzi

    Kwa jicho la kichawa unaweza kufurahia yanayoendelea, lakini kiukweli upendo, umoja na mshikamano wa watanzania vinadhoofu kila siku. Historia itakuja kutuhukumu kwa kutochukua hatua stahiki. Ukimya na kutochukua hatua kwa:- 1. Watu wanaotekwa, wanaopotea na kuuawa. 2. Ubakwaji wa demokrasia wa...
Back
Top Bottom