Watoto wawili wa familia moja, Ester Hillary na Eliana Hillary, ambao walikuwa wanafunzi wa shule za msingi na wakazi wa Mtaa wa Ikindwa, Kata ya Mapambano, Manispaa ya Tabora, wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia Septemba 13, huku mtoto mmoja akinusurika...