Siku nikifa maisha mapya yataanza, nuru ya macho yangu itapotea taratibu, tazama watu wanaonizunguka watalia na kuomboleza lakini haitasaidia nimelala siwezi kuamka tena.
Wataandaa kaburi langu, watalichimba kwa futi kadhaa waufukie mwili wangu, huzuni imetanda kwenye nyuso zao, mwili wangu...