Wale mnaokurupuka kuja kutoa Kwetu taarifa za Mgonjwa Mahututi au Kifo muwe makini kwani kuna Siku tutawasindikizeni na Vipigo tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,536
Kuna Mtu Kanikera mno leo asubuhi kaja haraka haraka kunipa Taarifa ya Mtu aliye Mgonjwa Mahututi huku akiniharakisha Kuvaa ili twende Zahanati ya Awali ili Kumuona na tutoe Msaada Kwake cha Kushangaza kufika pale nikakuta Maelezo yake na nilichokikuta kwa Mgonjwa Mahututi husika ni Vitu viwili tofauti yaani Dhambi na Pepo.

Tunaingia hapo Zahanati ili Kumuona huyu Mgonjwa (niliyeambiwa kuwa ni Mahututi) tunamkuta Mgonjwa ameshika Simu anaangilia Goli la Feisal Salum 'Fei Toto' aliloifunga (alilotufunga) Simba SC hivi majuzi huku Mkono mwingine ameshika Kikombe cha Uji wa Ulezi amekaa na anaonekana kuwa ni mwenye Furaha na kama vile hakuwa na huo 'Umahututi' wowote.

Nilipandwa mno na Hasira zangu za Utatu wa Kizanaki, Kimakuwa na Kitutsi juu ya hili mpaka nikataka Kumkumbuka Mwalimu wangu wa 'Martial Arts' Hayati Bruce Lee na nimpe Pigo moja la Kichina Mleta Taarifa za Mgonjwa Mahututi ila kilichomuokoa ni kwamba ni Mtani wangu wa Kihaya kutoka Mkoani Kagera ila angekuwa si wa kutoka huko leo ndiyo angejua kwanini Nyoka hana Ugoko.

Niwaombeni tu nyie mnaopenda Kukurupuka kuja kutoa taarifa za ama Mgonjwa Mahututi au hata MsIba wa Mtu (Ndugu, Jamaa na Rafiki) kuwa jaribuni Kwanza kuwa Watulivu, kuweni na Uhakika wa Taarifa na ikiwezekana basi nenda kwenye Tukio kahakikishe ndipo uje utuelezee vinginevyo Siku zingine mtakuwa mkija kwa Kukera na Kukurupuka hivi basi tutawaacheni Kwanza mtupe hizo Taarifa kisha tuwasindikizeni na Vipigo.

Ana bahati sana huyu Mhaya hakyanani japo Kanikera kweli kweli. Jamani nawatakieni Alhamisi Njema mbarikiwe wote.
 
Ungepiga kofi moja la mdomi linaitwa kelbu hatorudia mpuuzi huyo hiyo ishantokea Aisee tena asubuhi nimelala kaja bwege mmoja hivi linaita dirishani basi nikaamka mbio paramia ndoo za maji mpaka nikajikwaa aisee niliumia kufika nje linaniambia Oyaa mwanaidi karudi aiyaaa piga ngumi moja ya shavu na ushkaji uliishaga.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom